ACT Wazalendo: Tunalaani kutekwa kwa Vijana Wanne Wafanyabiashara Darajani na Askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar

ACT Wazalendo: Tunalaani kutekwa kwa Vijana Wanne Wafanyabiashara Darajani na Askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
1751115777989.png


Tarehe 26/06/2025, Vijana wanne (4) wafanyabiashara katika eneo la Darajani walitekwa na askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar, na kuwachukua na kuwafungia kwenye chumba kichafu sana katika ofisi ya Mamlaka ya Mji Mkongwe, Forodhani na kuwaingiza kwenye matangi ya maji machafu huku wakiwapiga na baadaye usiku kwenda kuwatupa maeneo ya Chukwani Buyu.

Tukio hili la kinyama ni miongoni mwa matukio ambayo hujirudia kila kukicha kwa vijana wa Kizanzibari, jambo ambalo linaonesha taswira mbaya na kushindwa kwa Serikali ya Awamu ya Nane, inyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, kutekeleza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi na badala yake kuwaumiza na kuwadhalilisha.

Sisi ACT Wazalendo tunalichukulia tukio hili la kutekwa kwa vijana hao kwa mshituko mkubwa. Tukio hili linatuonesha sura na rangi halisi ya watawala na mamlaka wanazozisimamia kuwalinda waovu kwa maslahi binafsi au labda kwa malengo ya kisiasa, jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 11 (2) inayosema: “Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake”. Pia Ibara ya 13 (3) inayosema: “Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha”.

Kutokana na kukithiri matukio haya ya kinyama na kishenzi kila kukicha, ACT Wazalendo tunataka kuona hatua zifuatazo zinachukuliwa:-

1. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe ajiuzulu ili kupisha uchunguzi wa kadhia hii.

2. Iundwe Kamati maalumu ya kuchunguza matukio yote ya utekeji na mauwaji yanayaoendelea Zanzibar.

3. Tunaitaka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora kuweka hadharani ripoti za uchunguzi na kuwataja wahusika wa matukio ya mauji yaliyotokea Kidoti, kisiwani Unguja, na Kiungoni na Mkoani, kisiwani Pemba.

Imetolewa leo tarehe 28/06/2025 na:


Mohamed Khamis Bussara
Naibu Msemaji Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar.


1751115601591.png

Pia soma ~ THBUB: Tukio la Vijana wa Darajani Zanzibar kupigwa na wanaodaiwa ni Polisi lina taswira ya uvunjifu wa Haki za Binadamu
 
Wakiteka shxxxga kama Lucha wala siwezi hashag yoyote

Maaana atafurahia kupigwa mtongo na jamaa wa noah nyeusi

🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom