Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Nimezinyaka nyepesi nyepesi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na ACT-Wazalendo wanapanga mkakati wenye nia ovu, eti kuanzia Jumatatu Novemba 2 mwaka huu wanapanga kuitisha maandamano ya kitaifa.
Mpango ambao utatangazwa kwenye Press Conference ya kesho iliyoitishwa na ACTWazalendo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo Mtaa wa Ufipa Jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi (4:00) pamoja na kutangaza maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi uliomalizika juzi na matokeo kuendelea kutangazwa pia wanapanga njama za uvunjifu wa amani Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Ili kukamilisha mpango wao huo wa kuitisha Press Conference ya kutangaza maandamano ya nchi nzima, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameshauri Maalim Seif Shariff Hamad aje Bara na watakapomaliza mkutano wao huo siku hiyo hiyo baada ya mkutano wapande Ndege waelekee Zanzibar kufanya mkutano kama huo saa nane mchana kwenye Ofisi za ACT Wazalendo Zanzibar utakaohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Kuu na wa Halmashauri Kuu ya ACT waliopo Unguja.
Maalim Seif atawasili Tanzania Bara kesho na Boti ya saa moja asubuhi na yeye pamoja na Zitto Zuberi Kabwe, Freeman Mbowe na Tundu Lissu kwa pamoja watakuwa wazungumzaji katika Press Conference hiyo.
Ajenda nyingine iliyotolewa na Zitto Kabwe ni kwamba hakukuwa na Uchaguzi na hivyo wanapanga kuitisha Uchaguzi Upya huku Maalim Seif akidai kuwa hakukuwa na Uchaguzi kwa sababu kila kitu kilipangwa na Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Niwakumbushe tu kuwa Watanzania hawawezi kusikiliza upuuzi mnaoupanga, Watanzania wa sasa sio wajinga na hizo ajenda zenu za kijinga mtaishia kuaibika tu.
Akina Zitto, Mbowe, Lissu na Maalim Seif mpango wenu mnaouleta Jijini Dar es Salaam kwa kuwa kuna idadi kubwa ya watu ambao mnalenga kuwavuta katika maandamano yenu hauwezi kufanikiwa hata mkiwatumia Madereva bodaboda kwa kuwapa mafuta na posho ili wawaunge mkono umefeli.
Hakuna uchaguzi ulikuwa wazi, huru na haki kama wa mwaka huu Tanzania, na hautawahi kutokea, tena kwa bajeti ya fedha za walipa kodi.