PreGE2025 ACT Wazalendo: Kufungia mitandao ya X, Clubhouse na Telegram ni mwendelezo wa ukandamizaji wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 ACT Wazalendo: Kufungia mitandao ya X, Clubhouse na Telegram ni mwendelezo wa ukandamizaji wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Wakuu

ACT wazalendo wametoa msimamo wao na kuonesha kukerwa na kitendo cha kufungwa kwa baadhi ya mitandao ya kijamii hususan kwa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
===

Kufungia mtandao wa X (twitter), Clubhouse na Telegram ni kuvunja katiba

ACT Wazalendo inaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufungua kufungulia kabisa mitandao ya kijamii ya X (Twitter), Mtandao wa Club House na Telegram na kuruhusu wananchi kupata habari na taarifa mbalimbali kupitia mitandao hiyo.

Kufungiwa mitandao hiyo ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 (1) na (2) inayotoa uhuru wa kutoa mawazo, kutafuta na kutoa habari bila kujali mipaka ya nchi na uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati, pamoja na haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani ambayo ni muhimu kwa shughuli za wananchi na muhimu kwa jamii.

Serikali kupitia waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari ndg. Jerry Silaa akihojiwa katika kipindi cha One on One cha Wasafi media Juni 03, 2025 amenukuliwa akisema kuwa Serikali Imedhibiti mtandao wa X (Twitter). Mtandao wa X ni miongoni mwa vyanzo vya taarifa rasmi za serikali zinazotolewa kupitia wizara, idara na taasisi za serikali ambapo wananchi hutumia mtandao huo kupata habari, mitandao ya kijamii sasa sio tu ni sehemu ya kuvinjari bali ni jukwaa linalosaidia watu kujiajiri na kufanya biashara mbalimbali.

Inashangaza wakati Serikali inafungia mtandao wa X kwa kisingizio kuwa inachapisha maudhui ya ngono, bado Ukurasa wa Ikulu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jeshi la Polisi, vyombo muhimu vya habari vinaendelea kuweka taarifa zake kwenye mtandao huo. Hivyo Kufungia mitandao hiyo kunasababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kupata taarifa muhimu za nchi.

Mpango wa kuufungia mtandao wa X (Twitter) ni mwendelezo wa ukandamizaji wa habari hasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2025, CCM na serikali yake haitaki uhuru wa habari na haki ya wananchi kupata taarifa na ndio sababu inafungia Mtandao wa X na mitandao mingine.
ACT Wazalendo tunataka hatua zifuatazo zichukuliwe;
Mosi, serikali ifungulie mara moja mitandao yote ya kijamii yaani X (Twitter), Clubhouse na Telegram ili wananchi waweze kufikia habari na taarifa mbalimbali.

Pili, ikiwa serikali haitafungulia mitandao hii chama chetu kitafungua kesi mahakama kuu kupinga hatua hii ovu ya Serikali ya CCM na serikali yake.

Mwisho, hatua hii ni mwelekeo wa Serikali kutaka kuficha matukio, taarifa na habari mbalimbali zinazohusu uchaguzi mkuu 2025 na michakato yake yote, jambo hilo halikubaliki.

Imetolewa na;
Ndg. Ntobi, Emmanuel R. Naibu Waziri Kivuli Habari, Mawasiliano na TEHAMA. June 25, 2025.
1750839262193.png
 
Dawaa ya yote hayo n hii km utatamkaaa Kwenye huu usingizi wa maiti tulio lalaa cc watanzaniaa.
FB_IMG_1749799584761.jpg
 
Back
Top Bottom