Hiki chama kimejaa uzalendo mtupu. Zitto atleast tunaona kwenye makosa anakosoa kwenye mazuri anasifia hizi ni siasa mpya kabisa za upinzani Tanzania na nna uhakika kwa uongozi huu wa Magufuli Zitto ndio mpinzani atayeeleweka na raia.
CHAMA cha ACT- Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, umeandaa maandamano ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano yake dhidi ya rushwa, ufisadi na kusimamia ukusanyaji kodi kama ilani ya chama hicho inavyosema.
Katibu wa chama hicho, mkoani humo, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ili kumuomba ayapokee maandamano hayo ya amani.
"Tumepanga kufanya maandamano hayo Desemba 16 mwaka huu, tukianzia katika ofisi zetu za Mkoa eneo la Keko Maduka Mawili na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma," alisema.
Alisema lengo lingine la kufanya maandamano hayo ni kumtaka Rais asimamie uongozi bora wenye lengo la kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na wazee Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.
Aliongeza kuwa, ilani ya chama chao ukurasa wa saba inaelezea ndoto ya ACT-Wazalendo ni kuona Taifa linajitegemea kiuchumi, kiutamaduni, kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, uongozi bora.
Mhandisi Ngulangwa alisema chama hicho kinaamini kuwa, mambo hayo yatatekelezwa vizuri kama nchi itajiwekea miiko ya uongozi kama inavyoelezwa na Azimio la Tabora lililohuishwa kutoka Azimio la Arusha.
"Lengo lingine ni kumuomba Rais ahakikishe nchi kupitia mamlaka husika, inasimamia mfumo wa matumizi ya fedha kama inavyosema katika ilani ya chama chetu ukurasa wa 23.
"Hata hivyo, yote hayatakuwa na maana kama mfumo wa fedha kupitia benki utakuwa umeshikwa na wageni kwani nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa benki kubwa zitakuwa zimebinafsishwa," alisema.
Alisema uanzishaji benki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ni maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi.
Hivi jeshi la polisi limeshaanza kuruhusu mikusanyiko ya kisiasa? Maana tuliambiwa imepigwa marufuku hadi itakapotangazwa maana hali nchini bado ni tete kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Kwakuifurahisha ccm hata chizi akihitaji kuandamana anapewa kibaliww jamaa ebu wacha ACT wafanye yao umeandika utumbo mtupu au kugombea maiti kumekuchanganya
CHAMA cha ACT- Wazalendo, Mkoa wa Dar es Salaam, umeandaa maandamano ya kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika mapambano yake dhidi ya rushwa, ufisadi na kusimamia ukusanyaji kodi kama ilani ya chama hicho inavyosema.
Katibu wa chama hicho, mkoani humo, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kuongeza kuwa, wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ili kumuomba ayapokee maandamano hayo ya amani.
"Tumepanga kufanya maandamano hayo Desemba 16 mwaka huu, tukianzia katika ofisi zetu za Mkoa eneo la Keko Maduka Mawili na kuishia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ilala Boma," alisema.
Alisema lengo lingine la kufanya maandamano hayo ni kumtaka Rais asimamie uongozi bora wenye lengo la kuirudisha nchi kwenye misingi iliyoasisiwa na wazee Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.
Aliongeza kuwa, ilani ya chama chao ukurasa wa saba inaelezea ndoto ya ACT-Wazalendo ni kuona Taifa linajitegemea kiuchumi, kiutamaduni, kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, uongozi bora.
Mhandisi Ngulangwa alisema chama hicho kinaamini kuwa, mambo hayo yatatekelezwa vizuri kama nchi itajiwekea miiko ya uongozi kama inavyoelezwa na Azimio la Tabora lililohuishwa kutoka Azimio la Arusha.
"Lengo lingine ni kumuomba Rais ahakikishe nchi kupitia mamlaka husika, inasimamia mfumo wa matumizi ya fedha kama inavyosema katika ilani ya chama chetu ukurasa wa 23.
"Hata hivyo, yote hayatakuwa na maana kama mfumo wa fedha kupitia benki utakuwa umeshikwa na wageni kwani nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa benki kubwa zitakuwa zimebinafsishwa," alisema.
Alisema uanzishaji benki uliofanyika mwaka 1967 na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benki ya Nyumba na Benki ya Maendeleo Vijijini ni maamuzi ya msingi kwa maendeleo ya nchi.
Afande Sele Mtoe....sidhani kama ni Mwana ACT kwasasa.View attachment 310657