ACT ndani ya Star TV hivi sasa

ACT ndani ya Star TV hivi sasa

wanaongea vizuri sana, utadhani ndio viongozi wa kitaifa, wewe unayesema wanaongea pumba ujui unachosema coz umeshazoea pumba za lema za kuandamana na za mboye nitafia angani, wakati dr. Silaa yeye anasema bomba la gesi limeanzia mtwara hadi ulaya, hivyo umeshaadhirika
mtu akiongea mambo ya msingi hauelewi
ninyi wanashirika la act ni wajinga sana!mme wenu kawaingiza choo cha kike,amepewa pesa kuvuruga chama imeshindikana then naninyi mnadandia gari kwa mbele poleni sana,ndo maana ujio wa chama chenu ni kuiponda chadema,eti muwe mbadala nyoo mbumbavu zenu,mtashinda lakini hamtashinda.
 
wala cyo ugomvi mimi natangaza hazarani nimwanachama wa ACT.
siwezi kukubari kushikiwa akili na hao wachaga
 
wala cyo ugomvi mimi natangaza hazarani nimwanachama wa ACT.
siwezi kukubari kushikiwa akili na hao wachaga

mwenye macho haambiwi tazama. ya kalenga ni dibaji tu. bad chalinze.
 
[h=2]Maigizo ya viongozi wa chama cha act na sera ya uwazi.[/h]
Jana katika kipindi cha medani za siasa na uchumi kinachorushwa na Star Tv walikuwa na mada juu ya Ujio wa vyama vipya kuelekea uchaguzi 2015 ambapo waliwaalika mwenyekiti na katibu wa muda wa ACT Mwanza. Katika maelezo yao hawa viongozi wa muda walisema miongoni mwa hoja zao kuu zilizowapelekea kuanzisha chama cha ACT ni kukosekana kwa uwazi ktk uendeshaji wa vyama vyama vyote vilivyopo. Katika mjadala huo mwanzoni tu mtangazaji alitaka kujua waasisi wa chama cha ACT.

Aliuliza swali rahisi sana na linaloeleweka vizuri akisema: Waasisi wa chama chenu ni akina nani? Viongozi hao walibabaika sana na kubakia kuzunguka tu huku wakiuma maneno wakisema mara ni watanzania, mara ni wanafunzi wa vyuo vikuu, n.k. Lakini M/kiti wa muda kwa kubanwa na mtangazaji alisema huku akibabaika kuwa viongozi wa juu wa muda wa chama hicho kwa maana ya Samson Mwigamba na wengineo katika uongozi wa juu ndio anaowajua kama waasisi japo hakuwa wazi.

Suala la kuanzisha chama sio suala la siri maana tena ni jambo la kifahari! Wakati vyamama vya kupigania ukombozi wa bara la Afrika vinaanzishwa licha ya kukabiriwa na upinzani toka kwa wakoloni lakini waliweka wazi waasisi na wanajulikana mpaka leo maana lilikuwa ni jambo la ukombozi kwa waafrika. Mfano waasisi wa vyama vya SWAPO, ANC, FRELIMO, LENAMO, ASP na TANU wanafahamika mpaka leo. Hata vyama vilivyoanzishwa baada ya ukombozi wa bara la Afrika vingi viliweka wazi na uanzishwaji wa vyama hivyo unafahamika vema. Mfano waasisi wa Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, na vinginevyo wanafahamika. Sasa kama viongozi wa ACT wanaamini chama chao ni chama cha ukombozi wa watanzania chenye sera kuu ya uwazi, nilitegemea suala la kuanzishwa kwa chama chao liwe la wazi, wanahabari waalikwe maana ni jambo la kujivunia na la fahari la kuleta chombo kitakachowakomboa watanzania kutoka ktk kile walichokiita “kukosekana kwa uwazi na ukiritimba wa vyama vilivyopo”.

Sasa jambo la kujiuliza ni kwa nini viongozi hawa wa ACT wanawaficha watanzania waasisi wa chama chao? Kama kweli chama hicho kitakuja kuwa chama cha wananchi ni kwa nini wanawaficha waasisi wa chama chao? Kama wanashindwa kuwa wawazi kwa jambo rahisi tu kama hilo la kutaja majina ya waasisi wa chama chao hicho cha ACT, hivi itakapokuja ktk masuala nyeti yanayohusu chama chao na ya watanzania kama vile rasrimali zao, uchumi, na mambo mengine kwa ujumla wataweza kuwa wawazi? Na kama hoja yao kuu ni Uwazi, je ni uwazi gani wanaoueleza na kuuhubiri kama jambo hilo dogo tu la kutaja majina ya waasisi wa chama chao wameshindwa kuwa wawazi?
 
Back
Top Bottom