Kuna taarifa za chinichini kwamba ATC wanakusudia kujiunga na UKAWA ili kuongeza nguvu ya upinzani dhidi ya CCM. Hii ni kwa sababu ACT wanaamini katika umoja na mshikamano na wanatambua kwamba UMOJA NI NGUVU. Nakumbuka siku Zitto alipozindua ACT alisema chama hiki hakina uadui na chama chochote. Nadhani alikuwa anajenga mazingira ya kutaka kuungana na UKAWA baadaye ili kuongeza nguvu katika safari ya kuelekea Magogoni.
MAONI YANGU
Kwa kuwa viongozi wa ACT wana chembechembe za usaliti, nawashauri UKAWA wasiwakubalie ACT kujiunga nao. Nina hofu huenda ACT wanatumiwa na CCM kutaka kuwavuruga UKAWA. Kuweni na hao wasaliti.
:israel:
Wazalendo ni ya Zito, ile nyingine ya Limbu.Ivi tofauti ya ACT WAZALENDO na ACT TANZANIA ni ipi?
Mie pamoja na kwamba sipendi mienendo ya Zitto kisiasa lakini napingana na wewe kumtakia maisha mafupi, wewe huna ubia na Mungu ningeomba ufute kauli yako.Maisha,Ukawa hawawezi kuungana na ACT wanajishumbua tu,intelejisia ilishakamilika zitto na chama chake ni ccm B
Bahati mbaya afya ya zitto inaendelea kudorora baada ya kuona mpango unazama
Asipoangalia huyu kijana ataishi maisha mafupi sana sababu ya mawazo.
tpaul, kama usipokuwa makini na hizi siasa utapata shida sana maana siku zote utakuwa wakuburuzwa.mkuu kwanini usiwashauri wajiunge CCM?
tpaul, kama usipokuwa makini na hizi siasa utapata shida sana maana siku zote utakuwa wakuburuzwa.
nisome vizuri nilichokiandika;
cuf na nccr waliitwa ccm b and c respectively. leo hii ni washirika wakuu wa kadima-nilini hao cuf na nccr wameache kuwa ccm b na c? kama ni serikali ya umoja kule nchi jirani (zenji) bado upo vile vile? au ni nini kimebadilika kwa hivyo vyama?
kafulila. machali na mkosamali walifukuzwa kwa usaliti na kuitwa ni sisimizi tu, leo hii kafulila yupo kwenye baraza kivuli lililoundwa na chadema, Prof safari na lwakatare waliitwa vibaraka wa ccm kule cuf leo hii ni viongozi waandamizi chadema/ukawa?
achilia mbali akina hamad rashid na wengineo. HUJIFUNZI KITU HAPA? Kwa michango yako unayotoa humu I'm sure you can do more than that.
achana na akina molemo na washirika wao wanaopiga propaganda humu. unless na wewe si miongoni mwao.
Umeshaweka msingi imara wa nondo na kokoto umepandisha ukuta wako Kwa matofali madhubuti ya umeme, ili nyumba yako iwe imara then ghafla mtu anakuja kukushauri eti uweke rinta ya fito na matope!! inakuja akilini hiyo!!