ACT inapopenya Kati Kati ya vitanda vyenye kunguni

ACT inapopenya Kati Kati ya vitanda vyenye kunguni

JOHN WA MARWA

Senior Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
100
Reaction score
61
UWEZO WA KITANDA KIPYA TUNAO

Habari zenu ndugu wasomaji na watanzania wote kwa ujumla, naamini mnaendelea vyema na joto la kisiasa linazidi kukua miongoni mwa watanzania. Naamini kwa muitikio wa mwaka huu, ni kweli kabisa watanzania tunayahitaji mabadiliko na tupo tayari kuhakikisha yanapatikana kwa njia yoyote iliyo salama.

Mchuano wa mwaka huu unaonekana mkali na wa kibabe kati ya vyama vitatu ambavyo ni CCM iliyomsimamisha Mh Magufuli, Chadema/Ukawa iliyomsimamisha Edward Lowassa na ACT iliyomsimamisha mwanamke pekeee Anna Mgwira.

Wakati kampeni zikiendelea kuna mengi sana yameongelewa ila kwa leo naomba makala yangu iongelee zaidi kwa lile alilolisema mh Magufuli alipokuwa wilayani Bunda alhamis iliyopita, Mh Magufuli alikiri Ccm ni kitanda kilichojaa kunguni na kukiri pia kuwa wapo kunguni waliokimbia kitanda na kuhamia kitanda cha jirani huku akiuomba umma wa wana Bunda wasikichome kitanda kisa kina kunguni bali wawaue kunguni.

Kwa mtazamo wangu na wa wengi, Kitanda kikishajaa kunguni walioshindikana na uwezo wa kununua kipya upo ni kwanini tusikichome au kukipa mapumziko hicho kitanda na cha jirani kasha tukajaribu kutumia kipya maana uwezo huo upo mikononi mwa mmiliki wa kitanda ambaye ni mwananchi.

Kunguni waliobaki ndani ya kitanda kikuu (CCM) na wale waliokimbilia jirani (UKAWA) sio sahihi kuendelea kukumbatiwa wakati uwezo wa kuweka kitanda kipya kisichokuwa na kunguni tunao (Shahada ya mpiga kura).
Kila mtanzania akiitumia vizuri nafasi yake aliyopewa kisheria kuhakikisha vitanda vyote vyenye kunguni pamoja na kunguni wote wanaangamia basi inawezekana, haina haja kuendelea kuumizwa na Kunguni ilihali uwezo wa kitanda kipya tunao.

Baada ya kusema yote hayo, napenda sana watanzania wakielewe hicho kitanda kipya kisichokuwa na kunguni, ukirejea juu nimeongelea vyama vitatu vyenye nguvu pamoja na wagombea wake pia nimeongelea kitanda kikuu chenye kunguni wengi zaidi na kitanda cha jirani kinacho shambuliwa kwa kasi sana na kunguni wanao kimbia ukame wa kitanda cha mwanzo. Nadhani mpaka hapo mnapata picha ya kitanda salama.

Kitanda salama kwa watanzania mpaka sasa anacho mama Anna Mgwira wa ACT ambaye anaamini katika kukomesha mashambulizi ya kunguni (Ufisadi) ndani na nje ya chumba chake (Chamani hadi taifa). Na katika hilo historia ya kitanda chake haina mahali popote palipo dalili ya kuwahi tembelewa na kunguni.
Wakati safari hii ikiendelea tunamuona mama huyu akiendelea kuhubiri yale tuliyotegemea yahubiriwe na kitanda cha jirani ambacho nacho kimevamiwa na kunguni kiasi cha walioshiriki kukinua kuamua kukikimbia na kuachana kabisa na kitanda hicho, hii inatupa nafasi sisi wananchi kuamua kipi kitanda sahihi kwetu.

Nimebahatika kupitia ilani za wote hawa watatu na bila kusitasita nadiriki kusema ni Ilani pekee ya ACT yenye vipaumbele na mikakati yenye kuonekana inayoweza kutekeleza wayasemyo. Watanzania wengi hupenda kushabikia siasa kama Mpira wa miguu ila kwa mwaka huu nawaommba waishabikie siasa kama mustakabali wa maisha yao.

Watakuja wengi, wenye maneno matamu wengi na ahadi nyingi zenye kututoa mate ila kila mmoja anatakiwa ahojiwe atawamalizaje kunguni walioshindikana ndani ya miaka hamsini katika kipindi cha miaka mitano au kumi? Akija na wa kitanda cha jirani naomba nae aulizwe anawezaje kutukinga na kunguni ilihali na yeye ni kunguni? Akija huyu wa kitanda safi na yeye aulizwe kajipanga vipi kuwaangamiza kunguni toka vitanda vyote. Kisha tutumie dhamana tuliyopewa kuhakikisha tunanunua kitanda kipya ifikapo Oktoba 25.

Ndatama H Mafuru
 
Back
Top Bottom