Acheni siasa, Shule hizi si utamaduni wetu!

Acheni siasa, Shule hizi si utamaduni wetu!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,939
Reaction score
51,061
Kuna watu wanadai kwamba mtoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni si utamaduni wa Kiafrika. Lakini hawasemi kama hizo shule wanazokataza mtoto wa kike kurudi kusoma kama ni utamaduni wa Kiafrika.

Mnaletaje utamaduni wenu wa "kiafrika" kwenye mambo ambayo si utamaduni wa Kiafrika. Kabla ya kuja kwa wazungu afrika tulikuwa na shule za aina hii na mifumo ya elimu inayofanana na hii. Inakuwaje waliotuletea shule leo wanaonekana wanataka kuingilia "tamaduni" Yetu wakati wao ndiyo wenye mfumo huu tunaoutumia?

Ni kabila gani lilikuwa linaweka vipindi vya kukaa shuleni na kupata tuzo (Cheti) baada ya kumaliza masomo na kuwa ni sifa ya kupata ajira? Ni lini makabila yetu yalikuwa yanatengeneza mitaala na kuweka mfumo wa kutoa alama kwa masomo yanayofundishwa? Hizo A-stashahada, Diploma, Shahada, shahada za Uzamili na Uzamivu mlizo nazo ni utamaduni wa Kiafrika?

Hao watoto wakipata mimba na kurudi shuleni baada ya kujifungua kitatokea nini ambacho hakikutokea wakati wanafanya Ngono zilizosababisha wapate mimba? Kwa nini kwanza msifute ile sheria inayosema kwamba mtu akitembea na Msichana mwenye Umri chini ya chini ya miaka 18 anatenda kosa la jinai?

Kama ni jinai kutembea na Msinchana chini ya Miaka 18, ni kwa nini basi msichana huyo akipata mimba na yeye anahukumiwa kufukuzwa na kukataliwa kurudi shule baada ya kujifungua. Inawezekanaje kosa moja likawa na adhabu kwa mtenda na mtendewa?

Kwa mfano Juma kafungwa kuwa kutiwa hatiani kwa kufanya ngono na Eliza mshichana aliye chini ya miaka 18. Miezi miwili baadaye Eliza naye anafukuzwa shule kwa kugundulika ana mimba ya Juma. Hivi mtoto atakayezaliwa anaandaliwa maisha ya aina gani? Ndiyo tanzania tuitakayo huko tuendako. Kwani kuna jambo gani la ajabu limetokea hadi tuhamanike kiasi hiki?
 
whatever its wapeleke private schools na padri wa katoliki wa songea naye kakataa
 
Back
Top Bottom