Acheni Magazeti yafungiwe Waandishi Wamezidi Unafiki.

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,293
Tangazo la Rais la kuyaonya magazeti mawili yaliyoandika habari za ujio wa njaa na ukame nchini kuwa ni Uchochezi na yako mbioni kufungiwa si jambo la kushangaza Kwa Sababu Rais wetu amekuwa mtu wa aina yake kabisa.
Hataki kusikia kuwa serikali yake kuna mahali inavurunda, ajabu zaidi ni kwamba baa la njaa linatokana na ukame na haliletwi na serikali lakini hata janga la asili bado tu rais wetu anasema halipo.
Sasa narudi kwenye mada, Waandishi wengi sana wa magazeti hapa kwetu Tanzania wamekuwa wanafiki kupindukia, sote tunajua sheria mbovu ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo iliachwa na wakoloni na kuendelea kutumika miaka yote utadhani hatujapata, na sheria hii ililenga kunyanyasa vyombo binafsi vya habari ambavyo vinakosoa Watawala.
Kana kwamba hiyo sheria haitoshi, serikali ya ccm kupitia uwingi wa wabunge wake mwaka jana tena ikaleta sheria mbaya zaidi ya habari na rais akaisaini haraka haraka.
Waandishi Kwa umoja wao wanaishia kulalamika kimya kimya tu bila kuchukua hatua za kukerwa na sheria kandamizi.
Walitakiwa wasuse kabisa kuandika habari za serikali Kama njia ya kushinikiza kukataa sheria kandamizi.
Wangeyaacha magazeti yao ya propaganda ya Uhuru, Habari Leo na Daily News yaandike.
Badala yake wamekuwa kimya tu huku Uhuru wa habari ukiwa tayari umefungwa kitanzi tayari Kwa kuuawa.
Sasa serikali imedai wazi kuwa magazeti hayo yamenunuliwa na wanasisa na wafanyabiashara na kutishia kuyafunga, hii yote ni Kwa Sababu ya unafiki wa waandishi.
Hawataki kushikamana kupinga unyanyasaji Wa habari.
Sheria ya mwaka jana ni mbaya zaidi, inampa mamlaka waziri wa habari kuyaamuru magazeti yote kuandika habari anazotaka kwa maslahi ya chama chake ccm na siyo Kwa maslahi ya taifa.
Tutaambiwa ni Kwa maslahi ya taifa, "Andikeni wote hakuna ukame Tanzania "
Na wote wataandika maana sheria inamruhusu.
Sheria ya huduma za habari 2016 ni sheria katili kabisa Kwa vyombo vya habari.
Inauma Sana kiongozi mkuu wa nchi kuingilia Uhuru wa habari,Ukame upo kwako macho yetu na matendo yetu wala si jambo la kusadikika.
Mimi binafsi nililima heka 12 za mahindi na zimeungua zote.
Waandishi badala ya kuungana na kukataa sheria mbovu mmebaki kuendekeza njaa kuliko kazi iliyowatuma.
Mnatia hasira Sana nyie watu.
Aliposema kuwa Siku za magazeti yenu zinahesabika alijua ni kifungu kipi kitawatoa barabarani.
Ukifika uchaguzi mnasahau madhira yote mnaanza kuandika habari za kupamba wanasisa, uchaguzi ukiisha mnaanza kulia.
 
Mwandishi kuandika kuna uhaba mkubwa wa chakula nchini - huo ndo uchochezi??
 
Waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari wote ni wanafiki kupindukia wacha awafungie akimaliza huko atahamia na huku kwetu kwenye social networks
 
umeandika point kubwa mwisho waandishi ni wanafiki namba mbili ,wakitanguliwa na wa wanasiasa ambao siku zote hushika namba moja
 
Back
Top Bottom