Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
ACHENI BLAH BLAH MWAKA HUU 2016 FANYENI KAZI
Naamini mpaka kufika sasa umeshauzoea mwaka huu mpya na tayari kwa kasi sana unafanyia kazi yale malengo makubwa uliyoweka mwaka huu. Kama bado hujaanza kufanyia kazi unasubiri nini? Mwaka tayari umeshazeeka na kadiri unavyochukua hatua mapema na kukomaa ndivyo utakavyoweza kuona majibu mazuri baadae.
Rafiki yangu naweza kukuhakikishia kitu kimoja, kama utaendelea na maisha yale uliyokuwa unaishi 2015, kufanya mambo yako kwa mtindo ule ule, basi mwaka huu 2016 hautakuwa na tofauti kubwa kwako. Utapata kile ulichokuwa unapata 2015.
Na kwa bahati mbaya sana utapata chini ya pale kwa sababu kwenye maisha hakuna kusimama, kuna kwenda mbele au kurudi nyuma. Na kama huendi mbele, moja kwa moja unarudi nyuma.Ndio maana nakusihi sana wewe kama rafiki yangu uchukue hatua.
Chukua hatua kwenye kile ambacho unataka kukifanya au kukipata mwaka huu 2016.
Unataka kuanza biashara? Basi anza, anza na wazo lolote, anza kidogo na utajifunza kadiri unavyoendelea kufanya.
Acha kuongelea kuingia kwenye biashara na ingia kwenye biashara. Acha kufikiria ni vitu gani unakosa ndio maana huingii kwenye biashara na anza kutumia vile ambavyo unavyo sasa kuanza biashara.
Unataka kuongeza kipato chako? Anza leo, anza kwa kuongeza thamani ya kile unachotoa, iwe ni kazi au biashara au umejiajiri. Jua ni kitu gani ambacho unakitoa na ongeza thamani yake. Kipato chako kinatokana na thamani unayotoa.
Kama una kipato kidogo maana yake unatoa thamani ndogo. Na ili upate kipato kikubwa anza kwa kuongeza thamani ya kile unachotoa.Unataka kuboresha mahusiano yako na familia? Hili ni muhimu sana kwa mwaka 2016.
Kwasababu familia yako inahusika sana kwenye mafanikio yako. anza leo kufanyia kazi lengo hilo, anza leo kwa kutenga muda wa kuwa na familia yako, anza leo kujali kuhusu familia yako.Chochote unachotaka kipo upande wa pili wa kuchukua hatua.
Unaweza kuchukua hatua sasa na ukafurahia matunda baadae au unaweza kuendelea kuongelea kuchukua hatua na ukawa mtu wa maneno tu.Mimi kama rafiki yako nakuambia kitu kimoja, chukua hatua, acha kuongelea sana ana anza kufanyia kazi.
Hiyo ndiyo njia pekee ya wewe kutoka hapo ulipo sasa.

Last edited by a moderator: