"Achana naye" Uzingativu uwe ni kinyume chake

Tariq Mimi

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
368
707
Habari wanaJF,

Naam kama title inavyojieleza hapo juu. Bila shaka sote tushakutana na ndugu, jamaa ama rafiki mwenye tabia ya namna hii, unapomuomba ushauri au kutaka kumshirikisha katika jambo atakujibu short tu "Achana naye", "Mpotezee" au "Potezea".

Kwa uelewa na uzoefu wangu mdogo nimegundua watu wa namna hii mara nyingi ni wanafiki tu katika maisha yaani marafiki wanafiki au watu wasiokutakia mema au mafanikio katika jambo au mambo yako.

Yani binafsi nikitaka kufanya jambo haijalishi la kisiasa, kiuchumi, kijamii au mahusiano napenda mtu kama atabahatika kupata fursa ya kushirikishwa nami basi bora akaniacha tu niamue mwenyewe au anipe udhaifu wa jambo au mtu (kama ni mtu) kuliko kuniambia nipotezee au nimpotezee tu bila kunipa sababu ya msingi au hata kugusia tu kwa ufupi.

Hii kwa vijana mara nyingi ukitaka kuhakikisha jaribu pale ambapo imetokea binti au mvulana umevutiwa naye ukapewa jibu la namna hii, mara nyingi huyo mwenzako utakuta baadaye yeye ndio anamfuatilia aliyekuambia mpotezee au anamfanyia mpango jamaa au binti mwingine.

Nimejaribu kuwasilisha mawazo yangu japo sina hakika kama naweza kuwa sahihi kwa asilimia zote.
 
Na wewe unaomba omba ushauri mno bana. Wenzako huwa tunaangalia vichwa kwanza. Wengine hafai hata kumuuliza muda atakuchanganya tu.
Hapa nimeambulia kitu mkuu huenda ndio kosa langu japo sio muombaji saana ila nimeguswa tu na watu wa namna hii wanavyowarudisha nyuma wengine
 
Labda unaomba ushauri kwa jambo lisilo na uzito ambalo hata ww waweza tu lifanyia maamuzi. Ili tusichoshane jibu linakuwa rais kama hilo.
Hapana mkuu kuna watu wengine ukikaa nao story mnazoenda sawa ni za anasa tu kwenye masuala mtambuka hawasomeki kabisa
 
Inategemea na jambo ila kama una hitaji zaidi, usipotezee
Ndio maana nikaona uzingativu uwe ni kinyume chake kwa maana kwa msingi huu huyu alonambia nipotezee ndio nampotezea yeye halafu nachanganya na zangu
 
Back
Top Bottom