Acha kutudharau shemeji zako, sisi ndio tunajua ukweli kama utaolewa au unapotezewa muda tu

ndegemzungu

Member
Mar 10, 2019
92
240
Habari za humu wakuu, poleni na majukumh lakini tusichoke kumsaidi Rais kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati wa viwanda

Twende kwenye mada ni msichana wa mshkaji wetu flani hivi yaani haonekani kabsa kuwa wife material kwa maelezo ya mshkaji ingawa hata sisi tulilinote hilo mapema lakini tulimuacha mwana a-decide mwenyewe

Msichana anamashauzi kino, dharau ndio usiseme kwa mashemeji zake ambao ndio sisi, siku moja mwamba aliomba aazime gari yangu ampeleke bi mkubwa wake airport lakini akaniambia nikiwa namletea nimpitie mpenzi wake eneo alilonitajia niende naye nikafanya kama mwamba alivyonuomba. Sasa tukiwa njiani wese likakata kabla sijafika sheli shem akaanza maneno ya kidwanzi pale akampigia sim na mwamba akamwambia rafiki yako hajielewi kama hakuwa na pesa ya mafuta si angesema tumchangie.

Mimi nikashuka kwenye gari nikavuta bodaboda nikaenda kuchukua mafuta fasta nikarudi safari ikaendekea sasa shem njia nzima anamind ilibaki kidogo tu nimshushe sema kwa heshima ya mwamba nikamkaushia.

Mwamba anasema hawezi kumuoa huyo msichana hata iweje ingawa hajamuweka bayana ana pretend sana akiwa na bi mkubwa wa mwamba,

Wanawake msitudhara mashemeji zenu sisi ndio tunajua ukweli kama utaolewa au unapotezewa muda tu.
 
Gari yako, umempa lift, analeta nyodo unashindwa kunshusha? Kama ni mimi namwambia "shuka kachukue boda pale, jamaa yako atakulipia*. Wanawake wengi ukishakuwa na gari tu. Hata kama bovu, wakiliona limepack wanajua mtu mzito huyu. Sembuse kuishiwa mafuta ukiwa umempakia demu wa mshikaj!
 
hiyo itakua sio gari yako。。yaani mtu akuletee dharau kiasi hicho halafu bado una muacha tu apande gari lako 😓😓
 
hiyo itakua sio gari yako。。yaani mtu akuletee dharau kiasi hicho halafu bado una muacha tu apande gari lako
Kwa heshima ya mshkaji nikaona acha tu nimfkishe jamaa anajua dem wake alivyo so haikunipa shida coz najua anapotezewa muda tu
 
Ukute rafiki ni mnafiki tu ujui anapewa nini,
Pengine anakuambia ivyo ulidhike mwisho wa siku atamuoa,
Moyo wa mtu kichaka mkuu.
 
pamoja na ushauri wote uliompa, usije ukashangaa huyo jamaa akaja kumuoa huyo dem. mapenzi ya ajabu sana
 
Ha ha ha ,,usimuani mtu mkuu ukute jamaa kamwambia demu kuwa wewe ni dereva wake,hivyo demu alitaka utambue kuwa yeye ni bosi wako pia,ungemshusha tu ili kulonda heshima yako ya kumiliki gari mkuu
 
Ulishindwaje kumshusha ooh wait

Kumbe we ni mwanaume wa dar lazima uwe muoga hata ukidharauliwa
 
Back
Top Bottom