karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,800
- 3,261
NANI ALIYEKUAMBIA UCHUMBA NI NDOA..
Nawasalimu kwa jina la TOZO za jamuhuri Ya muungano wa Tanzania
Kuna mambo mengine hata kama sikuataka niseme yananibidi tu niseme. Hivi ni nani aliyesema kuwa swala akiwa mkubwa anaweza kumfikia ngamia? Hivi mbuyu unaweza ukawa mchicha? Hata kama wanasema mbuyu ulianza kama mchicha lakini hata siku moja mchicha hauwezi kuwa mbuyu.
Kila kitu kina wakati wake na nipaka yake lakini vijana wengi wa sasa wameshindwa kuzingatia hili. Unakuta binti yupo tu kwenye uhusiano wa awali na kijana wa kiume basi anajiachia kama vile kaolewa. Huku kijana naye anavyohangaika na kujitoa kama ndugu wa familia vile.
Tayari ameshaanza kwenda kwa kijana wa kiume, sijui kupika, kumfulia nguo na mbwembwe nyingine kibao. Dada Hivi hiyo ndoa ilifungwa lini? Lini umetolewa mahari? Mbona una kihelehele..!
Hata kama ni mapenzi siyo kwa namna hiyo, Kila jambo na wakati. Tena binti wa kipendwa kabisa unafanya mambo kama hayo? Mbona hayo ni maisha ya kipagani? Kwanin usifuate utaratibu? kwanin usisubiri wakati ufike?
Mara ooh, baba fulani, sijui mama fulani.. Mmmh, hao watoto mmezaa lini? Naona mnaota ndoto Za mchana mchana tena mkiwa macho. Tangu yule mpenzi wako wa kwanza uliyemuita baba fulani, sijui mama fulani mpaka huyu wa sasa uliyenaye, ukijumlisha hao watoto wakina fulani fulani utakuwa na watoto wangapi? Mbona unajizeesha kabla hujazeeka.!
Sasa bora hao wanaoishia kuitana tu hayo majina labda ndio ujana wenyewe na vionjo vyake. Lakini wapo wengine ambao wao wanakula tunda tena bila hata kunawa, hawana hata imekuwa ni tatizo, subira hakuna, wanajiendea tu kienyeji-enyeji.
Hivi hiyo miili haiwezi kutulia? Imepakwa upupu unaowasha? Ebu ufike wakati muwe na hofu ya MUNGU. Mnasema kama mimba mtatoa, UKIMWI mnasema eti Mbona sawa na Malaria, Je vipi hukumu ya dhambi mnayoifanya? Hivi mnafikiri Mungu ni mwanadamu au haoni hayo manayofanya? Ndugu kila unalofanya liwe jema au baya hakika UTAHUKUMIWA.
Sasa mambo yanakuwa mazuri pale wanapopigana chini, si majonzi hayo na kilio kisichoisha, Mara ooh umenisaliti, umenipotezea muda wangu, najuta kuwa na wewe. Hahahaha..! Ngoja nicheke, Hivi ni nani aliyekuambia Uchumba ni Ndoa? Ulijiachiaa mwenyewe ukadhani umefika, ukajiona umepaaata kumbe umepatikana.
Sasa unalia nini? Zile hubby, sweetie, laaziz zimeenda wapi? Ulikuwa unaota umejenga ghorofa angani wakati hauna hata kibanda. Unakumbuka ule msemo usemao kuwa Uyaone? Basi ndio hayo unayojionea Sasa.
"NADHANI SIKU NYINGINE UTAFAHAMU HATA SWALA UMKIMLISHA VIPI HAWEZI KUWA NGAMIA NA SIKIO HALIWEZI KUZIDI KICHWA".
KILA JAMBO NA WAKATI WAKE.. UCHUMBA SIO NDOA..!
Kama hujaelewa soma tena