Accusations zilizopo sasa: Ushauri kwa wahusika

infinite_

Senior Member
Sep 10, 2013
127
125
Kwanza kabisa napenda ku-declare interests:

1: Mimi sio Mwanachama wa Chama chochote cha Siasa.

2: Kwamba mwaka 2015 nilipigana kwa hali na mali kuhakikisha Ushindi wa Mh. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ilifikia hatua nili-risk ata maisha yangu kufanikisha ushindi wake kwa kuhamasisha watu wajue tofauti za wagombea (SIO CHAMA) ili wapige kura kwa manufaa ya Tanzania.

3: Sipo hapa kisiasa na wala hoja yangu isijadiliwe kisiasa bali kwa Misingi mipana ya Taifa letu.

4: Interests zangu zipo kwa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/Serikali/Watu wake tu.

---------------------------------------

Hivi karibuni tumekuwa tukipata taarifa mbalimbali (Accusations) kwenye Social Media na News Prints:

1: kwamba inasemekana Mkuu wa Mkoa alifeli Kidato cha nne.

2: Kutokana na kufeli huko inasemekana pia ametumia cheti cha mtu mwingine kinyume cha Sheria kujiendeleza Kielimu na kupata mafanikio makubwa.

3: Inasemekana Amebadilisha jina la cheti alichopewa na kuongezea jina la lingine.

4: Inasemekana kwamba pia ametengeneza vyeti vya kuzaliwa na kutengeneza passport ya kusafiria kwa jina ambalo sio lake kinyume na sheria.

5: Inasemekana kwamba Mh Mkuu wa mkoa enzi za nyuma alikuwa pia hana uwezo mkubwa kielimu kabisa.

6: Inasemekana kwamba Mh Mkuu wa Mkoa ana mali nyingi kuliko nafasi aliyonayo na vivile ametuhumiwa kujihusisha na Kampuni/Wafanyabiashara fulani kwa maslahi yake binafsi.

HOJA YA MSINGI

1: Watu wengi (Raia wa Tanzania) wametoa Serious Accusations ambazo ni nyingi na very crucial, na mpaka sasa Sio Mh. Mkuu wa Mkoa wala Taasisi yoyote husika ya Kiserikali iliyoweza kujibu hizi tuhuma ambazo ni za msingi.

2: Accusations ina pande mbili, kuwa ni kweli au SIO kweli na inabidi iweze kutolewa taarifa yenye vielelezo kujibu hizo tuhuma ili kufahamu usahihi wa hizo Accusations.

IMPLICATIONS

1: Kukaa kimya kwa Mkuu wa mkoa bila kujibu tuhuma hizi inaleta picha kwa Watanzania kwamba tuhuma zisemwazo uenda ni za kweli na kama sio kweli inabidi zikanushwe.

2: Kukaa kimya kwa Serikali bila ya kutoa maelezo yoyote inaleta picha kwa Watanzania kwamba tuhuma zisemwazo uenda ni za kweli na kama sio kweli zikanushwe.

3: Mpaka sasa Serikali ilibidi ijisafishe na hizi tuhuma; at least kwa kutoa tamko kwamba "tumepokea hizo tuhuma na tunazifanyia kazi/uchunguzi" na sio kukaa kimya mpaka sasa.

4: Ikumbukwe ndani ya Tanzania nchi nzima Operation ya kusaka vyeti feki kwa wafanyakazi imefanyika na wengi wamekamatwa, kushitakiwa na kufukuzwa kazi; Je Serikali na taasisi zote husika kukaa kimya mpaka Sasa inaleta picha gani kwa Watanzania?? Inaleta muonekano gani kwa wale waliofukuzwa na kushitakiwa kwa kuwa na vyeti feki?? Inaleta picha gani kwa Taifa kwa ujumla??

USHAURI MUHIMU.

1A: Washauri wote wa Rais; Washauri wa taasisi nyinginezo zote; pamoja na wizara zinazohusika mkikaa kimya pia bila ya kutoa ushauri ili maamuzi yafanyike au mkikaa kimya bila ya kuwafanya wahusika kutoa maelezo kwenye ili swala (kukana au kukubali shutuma) pia inaonesha waziwazi kwamba nafasi zenu kuwa Washauri haziwafai na mnatakiwa muache kazi mara moja. Washauri wa kweli (competent) wanatakiwa kutoa ushauri ata kama ushauri huo utaonekana mmbaya mbele ya mhusika kwa manufaa ya Taifa.

1B: Serikali pamoja na Mh Rais wote kwa pamoja walitakiwa kulindwa since day one ili wakae mbali na hii skendo (Accusations); Kulindwa kwao ungefanyika only kwa kutoa kauri/tamko
kwa vielelezo au kumfanya mhusika kutoa kauri/tamko kwenye hii shutuma na SIO KUKAA KIMYA.

2: Watanzania wanasubiri tamko kutoka kwenu (Wahusika) la eidha kukanusha au kukubali kwamba makosa yalifanyika. Kuwa wawazi kwenye jambo hili italeta picha nzuri na kuleta matumaini kwa Watanzania kwenda kwa Serikali yao waone kwamba hakuna mtu aliye juu ya Sheria, vilevile itaongeza imani kwa Serikali yao; na kama sio kweli basi Watanzania watafurahi zaidi wakisikia kauri zenye vielelezo kujibu tuhuma zilizopo.

2B: Wahusika msipuuzie hizi tuhuma na kusema eti wanaopiga kelele ni watu wa mitandao tu peke yao; fanyeni utafiti na mtagundua ni nchi nzima, mpaka ata mimi leo nimeamua kutoa ushauri huu lakini tukiishia kusema eti tukae kimya tu ndio jawabu au hatutaki kusema lolote au kelele zipigazwo sasa (tuhuma zilizopo) ni za wauza unga tu basi tutajidanganya na kutengeneza mazingira Magumu 2020.

3: Tatizo hili mbele yenu ni kipimo tosha kwa kila anahehusika kuonesha umahiri wake kwenye kuongoza, kwenye ufanisi wa utendaji wake na kufanya maamuzi magumu kwa Maslahi ya Taifa. Kukaa kimya Sio jibu na nawashauri wahusika mtoe kauri za uongozi kuwaweka Watanzania wamoja bila ya kuonesha kubagua kama hizi tuhuma ni za kweli au SIO za kweli.

This is like a Mini-Watergate of Tanzania. It needs to be handled with care.

-----------------

Pls toeni comments zenye tija na sio comments zenye kubeba vyama vyenu, chuki au kutumia kauri mbaya sababu tunataka kujenga na SIO kubomoa. Asante

Tanzania comes first.
 
Arrogance trolls our conscious, sisi ni nani wakutujibu, na sasa ishakua main stream, watu wanazihaki, wanatunga nyimbo na hata mchezo wa kuigiza.

Wao kimya! That's arrogance at high level!
 
Hata Mimi natamani kuona hatua inayochukuliwa na serikali kwenye hili sakata
 
Shida ni ukanda, uchama, visasi!

Tulishasema urais ni TAASISI, sio mtu. Ulipoamua kurisk maisha yako ili unaempenda atawale umeona utawala wake sasa?

Kinachofanyika sasa hivi ni kwamba acha waongeeeeeeeeeeee mimi ndio nimekuweka hapo ulipo, so usiwaze, fanya mambo yako.
 
Ukizichambua kwa makini tuhuma dhidi ya Makonda utagundua kuwa jina na vyeti vyote ni halali.Ndomana hujamsikia hata Tundu akiliongelea hili.Labda itumike ile kanuni ya Nyerere kwamba kiongozi wa Umma hatakiwi kuwa ni mtu mwenye tuhuma tuhuma!
 
"Tanzania comes first" you have correctly commented.

Umeandika kwa ufasaha na mtiririko wa kiungwana.

Niongezee tu, kama nilivyoandika humu JF, alipozaliwa (kuna wanakijiji wapo, wazee kwa vijana wa rika lake), shule na vyuo alivyosoma vipo (kuna wanafunzi wenzake na waalimu), sehemu alizofanya kazi bado zipo (kuna marafiki na wafanyakazi wenzake).

Hata bila uchunguzi wa kina, katika 'vetting' hao niliowataja hawakuhusishwa hadi kuwepo kwa maswali ya msingi

1) Je, Daud Bashite ndiye Paul Christian au Paul Makonda, au ni watu watatu tofauti?"

2) Kama ni watu tofauti wako wapi? Na uhusiano wao ukoje katika sakata hili, km kufahamiana?
 
Ukiokota mbwa alafu ukamfuga.......!!!
Mbwa huyo akawa mtiifu hata kuwauma na kuwajeruhi hata wasio na hatia na ugomvi wako ukamuamrisha akulipizie visasi.....

Siku unatambua kabla ya kuwa na mbwa yule alikiuka misingi ilompelekea kuwa mbwa wako....
Lazima ukae kimya na ukimya wako ni kwa sababu ya maovu na dhulma ulomuamrisha mbwa ayafanye kwa jina lako.....
 
Umetoa hoja kistarabu.Kwa maoni yangu kuna sababu mbili kubwa kwanini serikali iko kimya.
1_Hulka ya mkulu ya arrogance,yaani anawaza ...acha waseme mimi ndiye nilikuteua na mimi pekee ndiye naweza kukuondoa.Hii inaambatana na mahaba yaliyopitiliza juu ya kijana wake
2_Kumuondoa ni kama kuudhihirishia umma kuwa vetting huwa haifanyiki kwa umakini.As long as ni kada mtiifu,basi anatufaa.Mkuu anaona aibu kukiri udhaifu huu hadharani wakati ameshajipambanua kama mtu makini asiyekosea.
 
...Ata mimi Nimekaa nikitafakari bado nashindwa kupata majibu ni wapi kunapofanya ugumu wa kutoa kauli eidha Kukana au Kukubali Shutuma? Sio tu kwa mhusika aliyepewa shutuma bali ata kwa Serikali, taasisi za Serikali na wizara husika wote wapo kimya!

Shutuma hizi zinaachwa kuendelea kusambaa kama vile moto wa nyikani. Imefikia ata watoto wadogo nao wanaliongelea na kulisema mitaani!

Swala hili linaonekana dogo lakini likiachwa na kubakia kimya basi ni lazima litatoa output mbaya hapo baadae as Consequence.

"Tanzania comes first" you have correctly commented.

Umeandika kwa ufasaha na mtiririko wa kiungwana.

Niongezee tu, kama nilivyoandika humu JF, alipozaliwa (kuna wanakijiji wapo, wazee kwa vijana wa rika lake), shule na vyuo alivyosoma vipo (kuna wanafunzi wenzake na waalimu), sehemu alizofanya kazi bado zipo (kuna marafiki na wafanyakazi wenzake).

Hata bila uchunguzi wa kina, katika 'vetting' hao niliowataja hawakuhusishwa hadi kuwepo kwa maswali ya msingi

1) Je, Daud Bashite ndiye Paul Christian au Paul Makonda, au ni watu watatu tofauti?"

2) Kama ni watu tofauti wako wapi? Na uhusiano wao ukoje katika sakata hili, km kufahamiana?
 
hongera kwa ujenz mzur wa hoja, mi pia naunga mkono hoja kuwa mamlaka znazohuska NECTA na mamlaka ya uteuz wamalz utata huu. Ili kuuaminsha uma kuwa wako silias na ish ya uhakik, kma mkulu alivojpambanua
 
Ukizichambua kwa makini tuhuma dhidi ya Makonda utagundua kuwa jina na vyeti vyote ni halali.Ndomana hujamsikia hata Tundu akiliongelea hili.Labda itumike ile kanuni ya Nyerere kwamba kiongozi wa Umma hatakiwi kuwa ni mtu mwenye tuhuma tuhuma!
una maanisha nini? kwamba yeye ni Paul Christian Makonda na pia ni Daudi Albert Bashite? kwamba yote hayo ni kweli na ni halali?
Contradiction!
lakini hata hivyo, ama akae kimya kabisa, yaani: ACHITEME, ACHIMUNG'UNYE, ACHIMEJE, ACHICHEME, ACHILIE KANICHANI WALA NCHIKITINI
maana inatuchanganya kwamba ni kama analilia huruma za watu. ooh, vita hii ni kubwa sana ina maadui wengi, ooh,nk. bullshit! kama hataki kuonesha vyeti vyake kama walivyofanya wengine, kina Zitto na Mwigulu, au kama Rais alivyoguswa kuhusu tuhuma za kielimu dhidi ya mteule wake mmoja, alimwambia aoneshe vyeti vyake. mbona kwa hili la Makonda a.k.a Bashite, ameuchuna? hapo ndipo watu wananusa harufu ya nyama iliyooza inafichwa mahala, pafyumu zinapulizwa lakini wapi
 
Serikali haiendeshwi kwa social media

...Unatakiwa uwe na kipawa cha kuona mbali kujua Consequences za Kukaa kimya hapo baadae.

Jambo hili sio la kucheka nalo, sio la kucheza nalo wala sio la kulikalia kimya; Kauli ya Serikali; Wizara zote husika na Taasisi za Serikali zilitakiwa kusema neno kwa Wananchi eidha wanafanyia uchunguzi, wanakana kwamba SIO kweli au ni kweli.

Tuhuma ni tuhuma tu na Kamwe hauwezi kukalia kimya tuhuma kama hii eti kisa imetokea kwenye Social Media, Social Media imetumika kama njia ya kupaza sauti (Whistleblower). Crucial matter here, Government transparency and accountability need to take into effect.

Jinsi utakavyopanda mbegu kwa Watanzania kwa Kukaa kimya leo hii bila ya kusema chochote; basi ujue itakuwa sheria baadae maana siku zote mazoea ujenga sheria na ukienda tofauti wengine watalalamika wakitaka kufanyiwa kama Mh Mkuu wa Mkoa.

Washauri/Wahusika wote kwenye hizi taasisi; ebu naombeni mtumie hekima na busara kutoa ushauri sahihi na kuiomba Serikali izungumze chochote/kutoa tamko kwa manufaa makubwa ya Serikali; Tazameni mbali nawaomba cause output of this will have consequential negative impact as maneno yasemwayo mtaani na wananchi sio mazuri kwa Serikali yetu.

Kama mnashindwa/mkishindwa kutoa ushauri sahihi now; Je itakapokuja kuhitajika kutoa Ushauri kwenye matters of NS / serious economic aspects mtakuwa huru kutoa ushauri sahihi??

Hili tatizo ni kipimo tosha kwa kila anahehusika kuonesha umahiri wake kwenye kuongoza, kwenye ufanisi wa utendaji wake na kufanya maamuzi magumu kwa Maslahi ya Taifa. Kukaa kimya Sio jibu; na nawashauri wahusika mtoe kauri za uongozi kuwaweka Watanzania wamoja bila ya kuonesha kubagua kwa kujibu/kuzifanyia kazi hizi tuhuma kama ni za kweli au SIO za kweli. Each individual needs to be treated with fairness regardless of their positions.

This is like a Mini-Watergate of Tanzania. It needs to be handled with care.
 
Ukizichambua kwa makini tuhuma dhidi ya Makonda utagundua kuwa jina na vyeti vyote ni halali.Ndomana hujamsikia hata Tundu akiliongelea hili.Labda itumike ile kanuni ya Nyerere kwamba kiongozi wa Umma hatakiwi kuwa ni mtu mwenye tuhuma tuhuma!
unatia huruma sana yaani mpaka Tundu aseme ndo uamini,Tundu yeye ni msemaji wa serikali?shame on you nina wasiwasi na upeo wako
 
unatia huruma sana yaani mpaka Tundu aseme ndo uamini,Tundu yeye ni msemaji wa serikali?shame on you nina wasiwasi na upeo wako

Usishangae mdukuzi inabidi tuombe Mungu tu, inashangaza sana...

Wenzetu kwenye skendo yoyote tu utaona Actions sahihi zitafanyika bila ya kigugumizi na Wahusika wenye kufanya maamuzi / Taasisi zao zote zilizopo zinajua majukumu yao 110%.

Majuzi tu; US National Security Advisor (Michael Thomas Flynn) alifukuzwa kazi baada ya Accusations kuwekwa wazi na Washington Post kwamba alikuwa na mawasiliano na Viongozi wa Russia kabla na baada ya Uchaguzi wa Marekani kufanyika.
 
Back
Top Bottom