The minister, in his article, claimed to have authentic and reliable data from the regulator, Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), to back his claims that mobile phone companies have been evading paying taxes for some years nowthanks to a lack of technology to detect their actual revenues.
Kama kweli hayo maneno hapo kwenye red yamesemwa na naibu waziri basi tuna matatizi makubwa. Wengine wanaweza kusema kuwa January Makamba analalamika lakimi mimi nasema huo ni 'umbeya'. Inawezekena huyu ndugu amezoea kuvizia habari na kutoa kwa watu na sasa amejisahau anaendeleza mchezo ule ule. Nitaaeleza;
Telecom sector pamoja na TCRA iko chini ya wizara ya science na technology na kimpangilio wa kazi responsibilities zote za telecom ziko chini ya Naibu waziri. Sasa kama January kama naibu waziri amechunguza kuhusu ukwepaji wa kodi na kupata taarifa, tena anasema "authentic and reliable data" nilitegemea moja kwa moja achukue hatua za kisheria na sio kukimbilia kuandika article kwenye magazeti!
Kelele kuhusu ukwepaji kodi wa haya makampuni ya simu zimedumu sana na hapa jamvini watu wameandika kwa muda mrefu including jinsi makampuni ya simu yanavyolipa kodi kubwa nchi jirani. Hivyo January hana jipya zaid ya kukusanya notes za watu na kuziita article. Anatakiwa/alitakiwa kuchukuwa hatua haraka maana that's what is being paid to do, na kuhakikisha serikali inapata kodi yote iliyokwepwa huko nyuma. yote.
Vodacom hawapo kwenye top 15 tax payers hapa Tanzania for the last 5 years! Vodocom wana customers zaidi ya milion 10, Kenya Safaricom wana wateja around the same figure. Lakini Tanzania watu wanatumia muda mwingi zaidi kwenye simu kuliko Kenya, so why hawapo kwenye top 15 tax payers list?
But we know, kuna unywaji juice wa mara kwa mara hapo Magogoni. Kila leo magogoni wanatembelewa na mkubwa wa vodacom, siku mbili zilizopita ilikuwa ni zamu ya chairman wa Vodacom - Peter Moyo! Wanatafuta nini Ikulu? Na rais anajua kama hawa watu hawalipi kodi?
Pia nategemea January Makamba aanze ku-deal na haya matatizo ya kodi kwa kuhakikisha shareholders hawamuingizi mfukoni kama bado hawajamuingiza. Najua huu ni mtihani maana upo uwezekano wa yeye kukata mkono unaomlisha, lakini hicho ndicho anatakiwa kufanya na sio kutuandikia umbeya kwenye magezeti. Naibu waziri mzima unaambiwa kuna madudu kwenye sector unayosimamia badala ya kuchukuwa maamuzi ya kukomesha tatizo unakimbilia kuandika kwenye magezeti? Hebu turekebishe hili.
Rai yangu ya mwisho. Ningeshukuru kama viongozi wetu (hawa hili kundi la blackberry) wangetambua umuhimu wa kutumia lugha ya taifa - Kiswahili ili kila mwananchi awe sehemu ya maamuzi/uongozi nchi. Inachosha kila siku kuona hawa 'wateule' wanaandika mambo muhimu yanayogusa wananchi wa kawaida lakini wanatumia lugha ya kiingereza! Wanamfurahisha nani?