Acacia wakubali yaishe kwa Magufuli, makinikia kuchenjuliwa hapa hapa Tanzania

Watatoa kwa 85% maana yake kodi itapungua kwa kiwango hichohicho, hapo kopa na silva watatupa jalalani, hapo tutegemee kupata mvua yenye maji ya kijani sio muda mrefu.
 
Makanikia yapi wakati migodi mikubwa inayotoa makinikia Tanzania ni miwili tu, Buzwagi gold mine, bulyanhulu gold mine..

Bulyanhulu wamesimamisha uzarishaji na wameshatoa kazini wafanyakazi 1200.
Buzwagi inafungwa 2020, kuanzia January 2018 wanaanza process ya kufunga kuelekea 2020 na tayari wameshaanza kupunguza wafanyakazi...
 
Hii mizungu ni mijizi sana

Hivi hii nchi toka imepata uhuru 2015 ndio imeanza kuwa na serikali na uhuru imepata 2015?

Hawa tunaowaita majizi walikaa na serikali mezani tukakubaliana nao na wao wakaanza kuchimba, Walisafirisha haya madini kwenye viwanja vyetu vya ndege na barabara zetu wakilindwa na polisi wetu na watu wetu wa usalama wakiitwa Task force kule maeneo ya migodi waliwalinda 24hrs,,, Tunaazaje kuwaita majizi??
 
Hivi hii nchi toka imepata uhuru 2015 ndio imeanza kuwa na serikali na uhuru imepata 2015?

Hawa tunaowaita majizi walikaa na serikali mezani tukakubaliana nao na wao wakaanza kuchimba, Walisafirisha haya madini kwenye viwanja vyetu vya ndege na barabara zetu wakilindwa na polisi wetu na watu wetu wa usalama wakiitwa Task force kule maeneo ya migodi waliwalinda 24hrs,,, Tunaazaje kuwaita majizi??
Ni kweli udhaifu wa viongozi wetu wa kutokuwa na elimu ya mikataba ya madini au kwa makusudi ya ufisadi, ulisababisha hao wawekezaji kuwa huru kuiba madini na maliasili za nchi.
Wakulaumiwa ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kulinda maliasili zetu na wao wakadababisha huu mwanya mkubwa wa wizi.
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Hamna namna hatuwezi kurudisha mali tulizoibiwa hata tukiwashitaki na kuwafunga jela.
Tugange yajayo
 
Thread hii pamoja na kuwa inaonyesha mwanga wa TZ kufaidi hutaona wenzetu wakichangia...utumwa wa akili umewafunika
 
Yule wa "tutanyolewa bila maji" ameipata hii? Au yupo bize anafakamia mabakuli ya uji?
 
Thread hii pamoja na kuwa inaonyesha mwanga wa TZ kufaidi hutaona wenzetu wakichangia...utumwa wa akili umewafunika
Hawakanyagi hapa uzi ni mchungu,na hii inaonesha kabisa kwenye mazungumzo tutashinda kama majaribio wamejifanyia wenyewe kwenye mitambo yao na wamekiri kuna dhahabu nyingi maana yake tupo sahihi kusema tuliibiwa
 
Rai
Acacia wakubali yaishe kwa JPM
WAMEKUBALI yaishe! Pengine hivyo ndivyo inavyoweza kuelezwa kuhusiana na taarifa iliyotangazwa na kampuni ya Acacia juu ya mafanikio waliyopata katika jaribio la kuokoa kiasi
kikubwa zaidi cha dhahabu kutoka katika mchanga wa madini (makinikia) wakiwa hapa hapa nchini.
Tangu Machi, mwaka huu, usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi ulisitishwa na
serikali kwa maelekezo ya Rais John Magufuli, aliyetaka uchunguzi ufanyike ili taifa
linufaike na rasilimali zake.
Zuio hilo la serikali limeendelea hadi sasa baada ya ripoti za kamati teule mbili
zilizoundwa na Rais Magufuli kubaini kuwapo kwa upotevu mkubwa wa mapato utokanao
na tofauti ya taarifa juu ya kile kilichokuwa kikiripotiwa na kilichomo kwenye makontena
277 yaliyozuiwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Hata hivyo, wakati mazungumzo kuhusiana na makinikia baina ya serikali na kampuni ya
Barrick Gold yenye migodi miwili inayosafirisha makinikia ng’ambo ni miwili ya Bulyanhulu
na Buzwagi, kampuni ya Acacia ambayo inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Barrick,
imetangaza mafanikio makubwa ya mfumo mpya wa uchakataji wa dhahabu kwa kutumia
vitendanishi.
Taarifa iliyotolewa na Acacia kupitia tovuti yake rasmi jana, ikiwa na kichwa cha habari
kisemacho ‘Matokeo chanya ya Jaribio la Uchakataji Buzwagi’, ilionyesha kuwa kuna dalili
nzuri za kuwezesha kupatikana kwa kiwango kikubwa zaidi cha dhahabu kutoka kwenye
makinikia kulinganisha na ilivyokuwa awali.
Sehemu ya taarifa hiyo ilieleza kuwa Acacia inayo furaha kutangaza matokeo chanya ya
jaribio la uchakataji wa dhahabu kwenye mgodi wa Buzwagi ambalo limeandaliwa kwa nia
ya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa madini hayo kutoka mgodini.
Taarifa hiyo ilieleza zaidi kuwa mwaka 2017, makinikia ya dhahabu na shaba yalikuwa
yakichangia mapato kwa kiasi kinachokadiriwa kuwa asilimia 65 ya uzalishaji wa dhahabu
yote ya mgodi wa Buzwagi.
Aidha, ilieleza zaidi kuwa hata hivyo, tangu Machi 3, 2017, mgodi huo haukuweza tena
kusafirisha nje ya nchi na kuuza makinikia yake, hivyo kujikuta ikiuza kiwango kilichobaki
cha dhahabu kinachokadiriwa kuwa asilimia 35 tu ya uzalishaji wote wa dhahabu, wakati
huo huo mgodi ukiendelea kubeba gharama za uzalishaji kwa kiwango kilekile cha asilimia
100.
“Matokeo ya jaribio la uchakataji kufikia sasa yameonyesha kuwa Buzwagi itakuwa na
uwezo wa kupata dhahabu inayokadiriwa kuwa asilimia 85,” ilieleza sehemu ya taarifa
hiyo, ikitaja nyongeza ya matumizi ya vitendanishi kuwa msingi wa jaribio hilo.
Kadhalika, Acacia ilieleza katika taarifa hiyo kuwa awali, Buzwagi ilipanga kusitisha
uzalishaji wa makinikia katika robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2018, lakini kutokana
na mafanikio ya jaribio hilo, mgodi huo sasa utaendelea na uzalishaji hadi mwisho wa
maisha yake ambao ni mwaka 2020.
Taarifa hiyo ilieleza zaidi kuwa kutokana na mafanikio ya jaribio hilo, mgodi wa Buzwagi
utakuwa na uwezo wa kuuza wakia (once) za nyongeza kati ya 8,000 hadi 10,000 kwa
utakuwa na uwezo wa kuuza wakia (once) za nyongeza kati ya 8,000 hadi 10,000 kwa
mwezi katika kipindi kiliochobaki cha mwaka.
Kwa mujibu wa soko la dhahabu jana, wastani wa bei ya wakia moja ya dhahabu ni dola
za Marekani 1,300, hivyo nyongeza hiyo ya uzalishaji dhahabu ni sawa na mapato ya
ziada ya kati ya dola za Marekani milioni 10.4 na milioni 13 (Sh. bilioni 23 na bilioni 30)
“Kwa sababu hiyo, mrabaha wa serikali na tozo ya huduma (ambayo hutokana na
mapato) kutoka Buzwagi vinatarajiwa kuongezeka zaidi ya mara mbili kwa kipindi
kilichobaki cha mwaka kutokana na kuongezeka kwa mauzo kulinganisha na miezi sita
iliyopita,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo, ikiongeza kuwa Acacia inaamini jambo hilo
litawezesha kuimarika kwa mtiririko wa fedha mgodini kwa mwezi kutoka kuwa hasi na
kuwa chanya, hivyo kuimarisha pia urari wa taarifa zao za fedha na kulinda maelfu ya
ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja.
UFAFANUZI ZAIDI
Acacia walifafanua zaidi jana kuwa taarifa ya jaribio lao hilo haihusiani na makontena yao
ya makinikia yaliyoshikiwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
“Yale makinikia ya bandarini bado yanasubiri muafaka wa mazungumzo baina ya serikali
na kampuni ya Barrick… ila wakati tunasubiri muafaka, mgodi wa Buzwagi umefanya moja
ya maboresho ya mfumo wa kuchakata dhahabu,” ilieleza kampuni hiyo katika taarifa
yake ya ufafanuzi zaidi kwa Nipashe, hatua iliyotokana na swali la mwandishi kama wana
mpango wa kuomba wayarudishe mgodini makinikia yanayoshikiliwa ili kiasi cha dhahabu
iliyomo kiondolewe zaidi kupitia mfumo huo mpya wa uchakataji.
Acacia wakubali yaishe kwa JPM - Acacia wakubali yaishe kwa JPM via @Shareaholic
Rais wangu, Tanzania yangu. Umeanzisha njia, wengine watakaofuata watapaswa waendeleze utakapoanzia. Tutashangaa aje Rais mwingine aje na mikakati ya "kuwashwawashwa" na kubadilisha hayo mazuri yaliyoonyeshwa na JPM.
 
Rai, hayo mazuri unayoyazungumza ni yapi? Kutupa kopa na silver na kubakiza gold pekee ni mazuri? Kupungua kwa mapato na kubaki 85% hujui hapa wataongeza gharama za uzalishaji badae waseme wanapata hasara, kwani hayo madawa watayanunua hukohuko kwa washirika wao na kuweka cha juu

hivi unajua madhara ya taka zenye kopa? Hayo madini mengine aliyogundua mruma itakuwaje?
 
Back
Top Bottom