Acacia vs Tundu Lissu

Kokolo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2008
Posts
2,021
Reaction score
3,354

Mwandishi aliyeshinda Tuzo ya CNN ahoji nini kimemtokea Lissu?Aliwatukana Acacia/Barrick kwa miaka 20, leo anawatetea? Ataka uchunguzi wa kina.

@ Lissu, aliwatukana kwa miaka 20, baada ya magufuri kuingia madarakani na kukata mirija ya makinikia, Lissu akaanza kuwatetea, hapo ndo shida ilipoanzia kupelekea kutaka kumalizwa kabisa kidogo. Kwa nini hakuwatetea kipindi cha kikwete cha Shamba la Bibi, kitu gani alipewa na hao wazungu, pia kwenye share za Acacia 36.1% ambazo kampuni mama Barrick ilitaka kununua, Acacia walikataa katakata kuziuza kwa Barrick, wenye hizo share ni akina nani, pia kipindi cha mwanzo kabisa cha timbwili la makinikia, kuna viongozi wa juu kabisa awamu ya nne walipanda ndege hadi Toronto Canada kuweka mambo sawa yasije bumbuluka. Je Lissu alitumwa na nani awatetee Acacia pamoja na kuwaponda zaidi ya miaka 20. Ukifumbua hiki kitendawili utajuwa ni kwa nini Lissu alitaka kumalizwa kabisa. Je ni kwa upande aliokuwa anatetea au upande wa pili. Ndo maana hata akipiga kelele kiasi gani wazungu wanaojua kwa undani jambo hili watakuwa wanampa mkono Lissu kwa mbele wakimpa mgongo wanasema idiot guy.
Pia nyoka waliyoko ubarozi wetu Canada, je ndo walimtoa barozi kidatu kutaka kuingizwa kwenye pay slip ya hao jamaa wanaomiliki hizo asilimia 36.1% za Acacia.
 
Tulijua hili, binafsi nilitamka siku tatu kabla hajapigwa risasi kuwa yafaa auawe na huenda atauawa. Niliowatamkia walinijibu kuwa naota ndoto za mchana. Siku ya tatu nafika kijiweni tu, jamaa waliniambia nahusika na mpango wa kumwua LL. Kwa bahati mbaya sijawahi hata kumwona zaidi ya video na magazetini.

Lissu ilikuwa halali auawe. Undumila kuwili ndo chanzo.
 
Mimi ninavyoelewa TL hakuwatetea kabisa ACACIA/BARRICK, alichokuwa anapinga ni kuunda tume ya maprofesa halafu ikajikita kwenye makanikia na kucha dhahabu super ikiondoka kwa madege kila siku huko migodini, kilio chake kingine ilikuwa ni kuhusu sheria na mikataba iliyopkuwepo, aliona watakuja kutuliza zaidi wakikimbilia kwenye mahakama za biashara ambazo zimetajwa kwenye mikataba na alilaumu mara nyingi kwamba wapinzani tulikataa kupitisha sheria hizo zilizoletwa kwa hati ya dharula upande wa waliowengi hawakukubali sheria zikapita!!!. nilivyomwelewa mimi
 
Ngoja nivute kiti nisubiri wajuzi zaidi katika uchambuzi huu
 
Hii thread bado ipo? Nashanga. Kwa sababu thread inayoexpose ushenzi na uovu wa Lissu huwa haidumu humu JF. Inawezekana zile contribution zinazounga mkono hoja hazipostiwi ila tu zinazopinga
 
Undumila kuwili kivipi Mkuu!?funguka ueleweke
 

Mbona kaongelea legislature na utaalam wa negotiations kwa zaidi ya 80% ambayo kimsingi Lissu hahusiki. Sikiliza mantiki nzima ya video uliyopost ukiwa na independent mind. Ukiwa na sentiments kwenye kusikiliza na kuona ukweli hutapata point nzuri anazotoa za kujifunza. Tutabaki kuendelea kuharibu tu kwa sababu macho yetu yana majibu ya shortcut kwa kila point. Msemo wa kwamba kipofu akigusa kitu akaambiwa ni tembo basi kila kitu kikubwa atajua ni tembo tu na kuinyims sehemu kubwa ya akili yake kujifunza. Maendeleo ni multifactorial so tunapaswa kuwa na macho ya kujua kila kinachokwamisha na especially vikubwa zaidi badala ya kuwa excuses.
 
Imebidi niisikilize mara mbili nisije nikakosa kitu.
Mwandishi aliyeshinda Tuzo ya CNN ahoji nini kimemtokea Lissu?Aliwatukana Acacia/Barrick kwa miaka 20, leo anawatetea? Ataka uchunguzi wa kina.
Mgamba alisema yeye na "Lissu" walikuwa pamoja lakini alishangaa "Lissu" alipo anza "kuwatetea" hayo makampuni ya madini. Akaulizwa na Dr Mumbi "Je jamaa alipewa kitu kidogo?" akasema yeye hajui. Lakini ni kitu kina amsha maswali mengi na kinastahili kuchunguzwa. Kwa sasa yeye Mugamba hafanyi hiyo kazi tena. Hii haipishani sana na mleta mada alivyo ileta.

Haya yote ni ya mleta maada na siyo ya Richard Mgamba. Kama mleta mada kuna analofahamu aliweke hapa kwa uwazi sio kuunga unga maoni yake binafsi yaonekane kama ni ya Mgamba. Cha ajabu kuna kulishana matango pori kuhusu hili toka juu hadi kwa wapambe. Ni kweli Lissu alilaumu hatua kadha alizochukua JPM na akashauri nini cha kufanya. Je huku ni kuwatetea ACACIA waendelee kutulamba mali zetu? Je kosa lake ni kutoa ushauri tofauti na maamuzi ya JPM. Mgamba alipoulizwa kuhusu $190 B alielezea kiaina-akasema hiyo reporti hajaisoma, lakini ana amini kodi hiyo iliyotajwa ni ya kushtusha. Ukimsoma vizuri anajua $190B haikuwa sahihi lakini yeye kaona hiyo ni kama msingi wa majadiliano etc.

Sioni sababu zako za msingi kwa kuhalalisha jaribio la kumuua Lissu. Sikiliza vizuri hiyo video na mwisho utamsikia Mgamba akilaumu waliokuwa bungeni kwa miaka hiyo. Jiulize hao wapendwa wetu walikuwa wapi? Mbona hakuna anesema nao wanastahili kufa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…