Abiria na bastola kwenye ndege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria na bastola kwenye ndege

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Seacliff, Dec 9, 2011.

 1. S

  Seacliff Senior Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nimeshangaa kusikia kuwa abiria ameweza kuingia na silaha kwenye ndege pale JKN airport bila kugundulika. Lakini cha kushangaza zaidi ni kwa jinsi ambavyo hii issue inachukuliwa kiwepesi. True uzembe umefanywa na authorities wanaoitakiwa kucheki na hopefully watawajibishwa, lakini, kwa nini abiria huyo aruhusiwe kuendelea na safari? Responsibility yake kwenye hii ni nini? Sababu zimetolewa kwamba kwa kuwa ameigundua hiyo bunduki kwenye mfuko akiwa ameondoka nayo kwa bahati mbaya na akaitoa kwa wahudumu, ilibidi asamehewe. Wengi waliowahi kusafiri safari kidogo watakumbuka kwamba siyo rahisi kushindwa kujua kuna nini kwenye mfuko wako hasa wakati unasafiri kwenda overseas. Hata kama huyu abiria angekuwa mwanajeshi au askari ambaye yuko na bunduki muda wote, sioni kwa nini ameshindwa kujua kuwa iko kwenye mfuko wake. Na ule muda wote wa kungojea ndege baada ya kuingia kwenye lounge ina maana kuwa haikumtokea kabisa yeye au mumewe kwamba hiyo bunduki anayo? Ninachojua ni kwamba ni wajibu wa kila msafiri kujua kuwa kwenye furushi lake kuna nini. Hiyo ni common sense. Kwa wale wote ambao wameshasafiri kwenye viwanja vya ndege vya wenzetu, majawapo ya mambo unayoulizwa ni kuwa hili begi umepaki mwenyewe? Meaning kwamba ni wajibu wako kujua kuwa kwenye furushi unalosafiri nalo unajua kilichoko ndani. Kwenye issue ya kusamehewa, ni mara ngapi umeshasikia mtu anashikwa na drugs na kutumia hiyo line kuwa kuna mtu aliyeniwekea hizo drugs akasamehewa? Kama watu wangesamehewa kwa kuwa hawakujua kuwa wamebeba mzigo haramu, si kila mtu angetumia kisingizio hicho? Kuna possibility kuwa huyu msafiri hakujua anayo hiyo silaha kwenye furushi lake, lakini amefanya uzembe na kuhatarisha maisha ya wasafiri wenzake kwa kushindwa kucheki kabla hajaondoka. The least the authorities couldÂ’ve done was to ground her at least for that day, ili kuonyesha kuwa wako makini kwenye issue kama hii. Angekuwa grounded angepoteza ticketi yake lakini nina uhakika next time atakaposafiri ataangalia furushi lake mara mbili mbili kabla ya kuelekea airport. Ni uzembe kushindwa kuikamata hiyo silaha pale uwanjani lakini ni uzembe zaidi kumwachia mhusika bila responsibility kwa kisingizio kuwa hakujua silaha hiyo ilikuwa kwenye mfuko wake. Tunatakiwa kuondoa uzembe kama huu kwenye system zetu.
   
 2. k

  kindafu JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Ndo tulikofikia baada ya miaka 50 ya uhuru! Sio tu kwamba hatuna ndege zetu kama Taifa kutua ktk viwanja vya ndege,bali hata kusimamia usalama kwa ndege za mataifa mengine yanayotua kwenye viwanja vyetu tumeshindwa!!! Kama security system ya viwanja vyetu imeshindwa kugundua kitu kikubwa na hatari kama bastola,sembuse madawa ya kulevya? sembuse vito vya thamani vinavyotoroshwa bila kulipiwa kodi? Lakini wasemavyo waswahili ukishangaa ya Musa,utayaona ya firauni - kama vyombo vyetu vya usalama vilishindwa kuona hata "Twiga" wetu wakipakiwa kwenye ndege,tunatarajia nini? Kama kwenye kituo chenye udhibiti kama uwanja wa ndege,silaha imeweza kupitishwa bila kugundulika - je vipi huko mipakani? vipi kwenye njia za panya? Kwa mtindo huu tutashangaa majambazi kumiliki silaha kubwa tena za kivita? Al shabab je???
  My take: hili si jambo la kufumbia macho! Ni swala linalohusu usalama wa Taifa na Taswira ya Taifa ktk Jamii ya Kimataifa! Hivyo wahusika ktk ngazi zote wanapaswa kuwajibishwa bila longo longo na bila siasa!
   
Loading...