Abiria chukua tahadhari: Basi hili la Sai-Baba ni hatari kwako

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,670
Picha hizi ni kwa hisani ya RSA mmoja ambaye ameona kasoro hii ya tairi na kutoa tahadhari kwa wasafiri. Basi lilikuwa limeegesha Ubungo Stand na linaelekea Arusha.

d1569c3893d5e56d34b180890315ef08.jpg


2bc0370c40436116028790f37fd71269.jpg


Usikubali kuhatarisha maisha yako; ukiweza kukagua basi unalokaribia kupanda ni jambo la maana katika kuulinda uhai wako. Uhai ukitoweka haurudi!
 
Hilo basi nalikumbuka sana.... nilishawahi kulipanda nikitokea Same.... yaani ni balaa... ni bovu kama yale magari ya taka taka.... yaani nilishaangaa kuona mpaka toyo na sunlg zinatupita kama tumesimama...

Yaani hilo basi nimeshalikariri kabisa na namba nimeshaziandika mahali... kwa ajili ya kuweka kumbu kumbu sawa...
 
Nilipanda hili gari mwaka jana mwezi wa September nilipata dharura ya kwenda Arusha saa saba mchana, nikaambiwa lipo gari la Saibaba linaondoka saa nane, aisee gari lilikuwa limejaza watu kama daladala ya Mbagala

Linanuka hatari, ikawa mwisho wa kupanda hilo Saibaba
 
Hatari tairi ya mbele tena kipara hawa SUMATRA wako busy kugawa namba wapigiwe viashiria vya ajali sijui haya mabasi mabovu bara barani huwa hawayaoni...
 
Hata madereva wa hilo gari wanakuaga na mawenge mawenge linatokaga mchana, sijui wanakuaga wameshaonja vitu
 
Nalijua hilo basi ni kimeo balaa, mara ya mwisho nimepanda tuliondoka Ubungo saa saba mchana na tulifika Arusha saa saba usiku. Yaani sitasahau hiyo safari
 
Hili basi maarufu kama chausiku, ni nouma yaani ili basi halina tofauti na daladala ni zoazoa balaaa
 
Na huwa yanakuwa ya mwisho ili ukifika pale utaambiwa hakuna jingine ni hilo lililobaki kwa siku hiyo
 
Wakati fulani abiria tunajitafutia matatizo wenyewe kwa kutochukua hatua na kutojali hata uhai wetu!!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom