Abiria asafiri katika ndege akiwa pekee

Abiria asafiri katika ndege akiwa pekee

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322

Mwanamke aliyelipa nauli ya ndege ya £46 kuelekea Crete ameshangazwa baada ya kujipata kuwa abiria wa pekee katika ndege.

Karon Grieve kutoka Dunlop mjini Ayrshire aliitaja ndege hiyo aina ya Jet2 inayosafiri kutoka Glasgow hadi kisiwa cha Ugiriki ambayo kwa kawaida huwabeba abiria 189 kuwa ya kushangaza.

Alihudumiwa kama mtu muhimu sana VIP baada ya abiria wawili waliotarajiwa kuabiri ndege hiyo kukosa kufanya hivyo.

Jet2 ilisema kuwa sio jambo la kawaida kwa ndege ya mwisho ya msimu kuwa na abiria wachache.

Bi Grieve aliyekuwa akisafiri kuelekea Crete ili kuandika riwaya alisema kuwa ilikuwa wazi kwamba kulikuwa na abiria wachache wakati alipowasili katika uwanja wa ndege ili kuabiri ndege hiyo siku Jumapili.

Aliambia BBC kwamba: Niliwasili katika eneo la kukaguliwa na kwa mzaha nikawauliza wafanyikazi wa ndege , ni watu wangapi waliabiri ndege hiyo.

Tulianza na watu 10 hadi kufikia watu wanne na akasema huwezi kudhania kuna watu watatu pekee.

Lakini nilipoingia katika lango la mwisho la kwenda kuabiri ndege , watu wengine wawili hawakujitokeza.

Bi Grieve alisema kwa kuwa yeye ni abiria wa pekee wafanyikazi wote wa ndege hiyo walikuwa wakilijua jina lake.

Alisema: Tulikuwa marafiki wakubwa hata kabla ya mimi kuingia katika ndege.Rubani wa ndege alikuwa mzuri.

Baada ya ndege kupaa angani bi Griev aliniita kwa jina langu akiwa katika chumba cha urubani.

Alisema hujambo Karon, utaona Croatia upande wako wa kushoto na tutasafiri katikati ya kimbunga hiki na baadaye alikuja na kusema.

Tafadhalini Karon na wafanyikazi jaribuni kwenda upande mwengine wa ndege na mutazame ''ni kitu cha kushangaza''.

Bi Grieve alisema kuwa alipanga kusalia mjini Crete kwa mwezi mmoja akiandika kitabu chake kabla ya kurudi Uskochi, Hatahivyo amesema ni vigumu kujipata katika hali kama hiyo atakaropejea Uskochi.


Muungwana
 
Mi nishawahi panda bus toka Buja mpaka ngara, nikiwa alone, raha sana
 
Nilishawahi kupanda bus la TRL kutoka Iringa hadi Moshi peke yangu na Dereva. Ilikuwa raha ya ajabu na muujiza wa kipekee
 
Nimesoma shuhuda kadhaa za aina hii. Mara zote abiria husika hupata raha ya kujichagulia pa kukaa na kuhudumiwa kama V.I.P

Ila lazima yale maelekezo ya usalama ya kufunga mikanda e.t.c yafuatwe kama kawaida
 
I
Nchi na kampuni zenye pesa zao na kujali wateja. Hapa kwetu haiwezi kutokea.
INAWEZEKANA NA IMEWAHI KUTOKEA.
...
...
Si kwa ndege ILA mabasi tumekuwa na kampuni kadhaa mojawapo ni Scandinavia Express wamewahi kusafirisha single passenger in country.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Mm nilishawahi panda fisi ya babu yangu peke yangu na abiria wengne hawakupata siti kwani nilikalia siti zote mpaka kwenye mkia
 
BONGO IKIFIKA HATUA KWENYE DALADALA UMEBAKI PEKE YAKO, BASI KONDA ANAKUULIZA, KWANI UNASHUKA WAPI JOMBA? UKIMWAMBIA MWSHO WA GARI, ANANUNA, WANAKUFAULISHA KAMA KUNA MAGARI MENGNE.

NB
KUFAULISHWA NI HIYARI ya abiria.
 
BONGO IKIFIKA HATUA KWENYE DALADALA UMEBAKI PEKE YAKO, BASI KONDA ANAKUULIZA, KWANI UNASHUKA WAPI JOMBA? UKIMWAMBIA MWSHO WA GARI, ANANUNA, WANAKUFAULISHA KAMA KUNA MAGARI MENGNE.

NB
KUFAULISHWA NI HIYARI ya abiria.
 
Ulaya seat 200 tupu moja ina abiria ndege inapaa...

Bongo seat 199 zinawatu, moja haina mtu safari inahairishwa...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom