Abiria aamua kuishitaki Emirates Airlines Kwa kukaa karibu na mtu mnene Kwenye siti

Kuna kijana Fulani hivi (marehemu kwa sasa) nakumbuka alikuwa mgonjwa ni mdogo lakini alikuwa na uzito mkubwa sana, ITV walikuwa wakimripoti alivyokuwa amelazwa Muhimbili, alitakiwa kwenda India lakini ndege zikawa zinamkataa, japo mwishowe Wizara ya Afya ilisaidia akapelekwa India.
Interesting
 
Duh, duniani kweli kuna mambo..
Mi sikujua kuwa mtu anaweza anzisha complaints za namna hii..!!
 
Hee
kuna wamama wana vyura ukikaa nae kwenye basi hun bahati chura anakula siti zote mbili halafu unakuta chura mgumuu mimi napenda sana safarini nikae na mwanaume unakaa comfortable pia lunch na drinks ni free
Heeee...
Unasafiri lini tena tusafiri wote..!?
 
Kuna siku nilikuwa natoka Iringa na basi la Upendo...lile linaloondoka saa kumi na mbili asubuhi.

Nikapata siti ya mwanzo kabisa nyuma ya dreva.

Baadae si ikaja njemba inanuka pombe halafu imelewa. Harufu ilkuwa kali hadi nikamwomba konda anitafutie siti ingine na bahati nzuri aliipata.

La sivyo hata mimi ningeshuka na kwenda ofisini kwao hapo hapo stendi na kudai hela yangu.

Pata picha safari ya masaa 8 umekaa na mtu mwenye harufu mbaya!

Na hizi pua zangu zilivyo nyepesi kunusa harufu mbaya kwa kweli ingekuwa ni jehanamu kwangu.
Unatudanganya kila siku uko marekani kumbe uko Iringa?
 
Si kama ubaguzi ila hili nalo ni la kuangalia upya kwa mfano juzi nilipanda basi nikitokea arusha sasa jirani yangu kuna jamaa bonge na mm nilikuwa upande wa dirishani na basi lenyewe ni la 3x2 seats safari nzima jamaa kanibana kichizi seat ya katikati kakaa mmama naye ni mnene kiac imagine tumefika kia jamaa anataka nisogee tena dirishani the sametime karibu 20% ya seat yangu ni yy kaikali na steal anataka na %flani kwenye hiyo ilobaki ilibidi nimwambie nisogee kuelekea wap sasa maana huku nimefika mwisho!!!!!!
Nimecheka sana kwa hii sentensi.!
 
Inakera sana unasafiri kwenye basi siti ya pembeni yako kuna mama ana mtoto anajinyea kila saa halafu mara mtoto akukanyage na kukugasi...ni haki bhana awadai.
 
Kuna kijana Fulani hivi (marehemu kwa sasa) nakumbuka alikuwa mgonjwa ni mdogo lakini alikuwa na uzito mkubwa sana, ITV walikuwa wakimripoti alivyokuwa amelazwa Muhimbili, alitakiwa kwenda India lakini ndege zikawa zinamkataa, japo mwishowe Wizara ya Afya ilisaidia akapelekwa India.
Alifariki kabla ya kupelekwa India. ITV walionyesha
 
Kama siti zina armrest katikati, huwa nawahi kuzifungua na bonge akidai nirudishe hatuelewani kudadaeki.
Ningependa vyombo vya usafiri waweke kitu kama hii. Siti ziwe na armrests kuzitenganisha!!
 
Back
Top Bottom