Abdulwahid Sykes katika "The Making of Tanganyika" na Judith Listowel

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,551
31,223
ABDULWAHID SYKES KATIKA "THE MAKING OF TANGANYIKA" NA JUDITH LISTOWEL
Maggid Mjengwa:
Judith anaeleza pia kushindwa kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa T. A. A. Jambo hili ningependa Mwalimu wangu Mohamed Said alitolee maoni yake juu ya tafsiri ya jambo hilo.

Mwenyekiti,
Maggid Mjengwa Mwenyekiti kuna kitu kidogo umekosea katika swali lako.

Ulitakiwa uulize hivi, ''Judith anaeleza pia kushindwa kwa kura chache kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa TAA."

Ungeuliza hivi swali la kwanza kwa msomaji angejiuliza kwa nini Nyerere alishinda kwa kura chache?

Abdul laiti angegombea uchaguzi ule kwa nia ya kushinda angeshinda bila wasiwasi wowote.

Abdul angeshinda kwa kuwa Nyerere hakuwa anajulikana na mtu yoyote ukimtoa yeye mwenyewe Abdul, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Ukiangalia vipi uongozi wa TAA ulibadilishwa mwaka wa 1950 utaona Schneider ndiye aliyesimama kumwondoa kaka yake Thomas Plantan kwenye uongozi na akawaingiza Abdul na Dr. Kyaruzi.

Kabla ya uchaguzi ule wa April 1953 Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio,

Ukerewe kwa Hamza Mwapachu ili apate kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu Nyerere, kuwa bado ana fikra kuwa Nyerere atiwe katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 waunde TANU na Mwalimu aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika?

Jibu la Mwapachu lilikuwa Abdul amsaidie Nyerere kuingia katika uongozi wa juu wa TAA na amsaidie kupata ushindi na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Nyerere awe kiongozi wa harakati za uhuru.

Sababu aliyotoa kumpa Abdul ni kuwa yeye alikuwa anaona Nyerere anafaa zaidi kwa uongozi wa TANU kuliko Abdul lakini akaongeza kueleza kuwa Abdul kama Muislam kuongoza harakati za uhuru zitawazidishia Waingereza ukaidi kwani wanaweza wakachukua harakati za uhuru kama vurugu nyingine za Waislam mfano wa Vita Vya Maji Maji vya 1905.

Kwa siasa za nyakati zile bila ya Nyerere kukubalika na wenyeji wa Dar es Salaam Abdul akiwa mmoja wa hawa wanamji, Nyerere asingeweza kushinda uchaguzi ule.

Hivyo basi ndani ya ile ''inner circle ya inner circle,'' ya TAA ndani ya TAA Political Subcommittee uamuzi ulipitishwa kuwa Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule.

Laiti viongozi hawa wangefanya khiyana ya kumkataa Nyerere kwa sababu yeyote ile wangekuwa wamefanya kosa kubwa sana.

Nyerere aliiongoza TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kwa ustadi na ufanisi mkubwa sana.

Abdul Sykes hakumueleza Listowel haya na kwa miaka mingi historia hii hakuna aliyekuwa anaijua hata Nyerere mwenyewe hakupata kusema kuwa kwanza alipokelewa na Abdul Sykes na pili kuwa alipata kugombea urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes.

Siku Mwalimu alipotaja jina la Abdul Sykes hadharani katika hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985, Mwalimu alisema ''anadhani'' Abdul Sykes nafasi yake katika TAA alikuwa Katibu.

Mwalimu hakuwa na uhakika na historia ya uongozi wa Abdul katika TAA ilibidi adhanie.

Ningependa kuhitimisha kwa kusema kuwa aliyemweleza Listowel historia ya uchaguzi ule baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere alikuwa Denis Phombeah ambae ndiye alikuwa Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo ulipofanyika uchaguzi ule na yeye akawa ndiyo Returning Officer.

1572808788194.png

Denis Phombeah

1573701231143.png
 
Mohamed Said kwa nini usitoe kitabu kizima kuzungumzia wazalendo wote waliopigania uhuru, harakati zao wote mmoja mmoja , yaliyojiri n. k , kuliko kutulisha vionjo kidogo kidogo unatuacha tukiwa hatukushiba, toa kitabu kitakachobadili historia yote ya TANU
 
Laki...
Unadhani kitabu cha Abdul Sykes hakitoshi?
 
Mohamed Said, shida Abdul Sykes hakuwa kiongozi mkuu wa TANU kipindi cha uhuru, Nyerere anaonekana ndio aliongoza mapambano ya kudai uhuru kwa sababu alikuwa kiongozi mkuu wa TANU na ndie alieenda UNO kudai Uhuru. Abdul Sykes Sijui kipindi cha uhuru alikuwa na cheo gani hapo TANU, maana Nyerere alikuwa mwenyekiti na Oscar Kambona Katibu, Ni ngumu sana kumuaminisha mtu kuwa mchango wa Sykes ulikuwa mkubwa kupita Nyerere, wakati Sykes hakuwa na cheo chochote cha maana kipindi cha uhuru hapo TANU.
 
Inaonekana Abdul Sykes hakuwa na ushawishi ndani ya TANU hata kabla ya Uhuru, ndio maana nafasi ya makamu mwenyekiti aliondolewa, Rashid Kawawa akachukua nafasi yake
 
Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?
Inaelekea hujakisoma.

Abdul Sykes alikuwa katika "intelligentsia," na pia "financier," wa chama kuanzia enzi ya TAA.
Kubwa TAA na TANU vyama vyote hivi viwili vilikuwa vinaishi ndani ya nyumba yake.

Abdul na Hamza Mwapachu ndiyo waliopanga mipango yote ya kuunda TANU na mipango yote na mikutano ya siri ikifanyika nyumbani kwake.

Kadi yake ya TANU ni no. 3 no. 2 ni mdogo wake Ally no. 1 Julius Nyerere.

Abdul ndiye aliyempokea Mwalimu nyumbani kwake Dar es Salaam Stanley na Sikukuu Street na kumtia katika uongozi wa TAA 1953 na ikaundwa TANU 1954 na aliishi na Nyerere nyumbani kwake 1955 Mwalimu alipoacha kazi ya ualimu.

Baba yao ndiye muasisi wa African Association 1929 akiwa katibu ni kati ya "intelligentsia," wakati wake na pia "financier."

Historia hii ilifutwa kwa miaka mingi na jina la Abdul Sykes halikuhusishwa na historia ya TANU au historia ya Nyerere.

Haya kwa muhtasari ndiyo yaliyonisukuma kuandika kitabu cha maisha yake si hayo unayozungumza ambayo dhahiri inaonyesha hujasoma kitabu.

Itakuwa vyema endapo utasoma kitabu ndipo urejee kufanya mjadala.
 
Rashid Kawawa nitakupa historia yake ili umfahamu.

1950 Kawawa alikuwa katika uongozi wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA)pamoja na Ally Sykes, Dr. Wilbard Mwanjisi, Steven Mhando na Thomas Marealle.

Alikuja baadae sana katika harakati hizi.
Umenichekesha.

Ati Abdul "akaondolewa."

1953 baada ya ule Uchaguzi wa Arnautoglo Hall, Nyerere alichaguliwa President Vice President Abdul Sykes.

Chama kilikufa.

Tatizo linalokukabilieni wengi ni kuwa hamuijui historia ya TANU na Nyerere hakupata hata siku moja kueleza alifikafika vipi Kariakoo na nani walikuwa wenyeji wake.

TAA ilikufa si kwa kuwa Mwalimu alikuwa kiongozi dhaifu la hasha.

TAA ilikosa yale ambayo Executive Committee yalizoea kupata kutoka kwa Abdul kila alipoitisha mkutano.

Ilibidi kwa muda Abdul amsaidie Nyerere ili kurejesha imani ya wajumbe wahudhurie mikutano na chama kirejeshe nguvu na hadhi yake.

ABDULWAHID SYKES KATIKA "THE MAKING OF TANGANYIKA" NA JUDITH LISTOWEL
Maggid Mjengwa:
Judith anaeleza pia kushindwa kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa T. A. A. Jambo hili ningependa Mwalimu wangu Mohamed Said alitolee maoni yake juu ya tafsiri ya jambo hilo.

Mwenyekiti,
Maggid Mjengwa Mwenyekiti kuna kitu kidogo umekosea katika swali lako.

Ulitakiwa uulize hivi, ''Judith anaeleza pia kushindwa kwa kura chache kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa TAA."

Ungeuliza hivi swali la kwanza kwa msomaji angejiuliza kwa nini Nyerere alishinda kwa kura chache?

Abdul laiti angegombea uchaguzi ule kwa nia ya kushinda angeshinda bila wasiwasi wowote.

Abdul angeshinda kwa kuwa Nyerere hakuwa anajulikana na mtu yoyote ukimtoa yeye mwenyewe Abdul, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Ukiangalia vipi uongozi wa TAA ulibadilishwa mwaka wa 1950 utaona Schneider ndiye aliyesimama kumwondoa kaka yake Thomas Plantan kwenye uongozi na akawaingiza Abdul na Dr. Kyaruzi.

Kabla ya uchaguzi ule wa April 1953 Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio,

Ukerewe kwa Hamza Mwapachu ili apate kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu Nyerere, kuwa bado ana fikra kuwa Nyerere atiwe katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 waunde TANU na Mwalimu aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika?

Jibu la Mwapachu lilikuwa Abdul amsaidie Nyerere kuingia katika uongozi wa juu wa TAA na amsaidie kupata ushindi na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Nyerere awe kiongozi wa harakati za uhuru.

Sababu aliyotoa kumpa Abdul ni kuwa yeye alikuwa anaona Nyerere anafaa zaidi kwa uongozi wa TANU kuliko Abdul lakini akaongeza kueleza kuwa Abdul kama Muislam kuongoza harakati za uhuru zitawazidishia Waingereza ukaidi kwani wanaweza wakachukua harakati za uhuru kama vurugu nyingine za Waislam mfano wa Vita Vya Maji Maji vya 1905.

Kwa siasa za nyakati zile bila ya Nyerere kukubalika na wenyeji wa Dar es Salaam Abdul akiwa mmoja wa hawa wanamji, Nyerere asingeweza kushinda uchaguzi ule.

Hivyo basi ndani ya ile ''inner circle ya inner circle,'' ya TAA ndani ya TAA Political Subcommittee uamuzi ulipitishwa kuwa Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule.

Laiti viongozi hawa wangefanya khiyana ya kumkataa Nyerere kwa sababu yeyote ile wangekuwa wamefanya kosa kubwa sana.

Nyerere aliiongoza TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kwa ustadi na ufanisi mkubwa sana.

Abdul Sykes hakumueleza Listowel haya na kwa miaka mingi historia hii hakuna aliyekuwa anaijua hata Nyerere mwenyewe hakupata kusema kuwa kwanza alipokelewa na Abdul Sykes na pili kuwa alipata kugombea urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes.

Siku Mwalimu alipotaja jina la Abdul Sykes hadharani katika hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985, Mwalimu alisema ''anadhani'' Abdul Sykes nafasi yake katika TAA alikuwa Katibu.

Mwalimu hakuwa na uhakika na historia ya uongozi wa Abdul katika TAA ilibidi adhanie.

Ningependa kuhitimisha kwa kusema kuwa aliyemweleza Listowel historia ya uchaguzi ule baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere alikuwa Denis Phombeah ambae ndiye alikuwa Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo ulipofanyika uchaguzi ule na yeye akawa ndiyo Returning Officer.

View attachment 1253270
Denis Phombeah
Mohamed Said unataka kumaanisha kuwa vita ya Maji Maji ilikuwa ni vita ya kidini?
 
Huu ni uongo, na inaonekana huwa unarudia mara kwa mara huu upotoshaji, wala haikuwa hivyo unavyosema, inawezekana kweli mikutano ilifanyikia nyumbani kwao si wao waliokuwa Mastermind wa kui transform TAA...ni jina la TANU ndio walikuja nalo kina Sykes.

Historia ipi ilifutwa, na iliandikwa wapi? ili hali ulishasema Abdul alijitoa kwenye maradi, hivyo kama haikuwahi kuandikwa basi haikufutwa.
 
Kinyungu,
Ili uelewe Vita Vya Maji na matokeo yake katika historia ya Waafrika wa Tanganyika katika kupambana na ukoloni inabidi nikuchukue hadi Mahenge, Songea kwenye Makumbusho ya Vita Vya Maji:

''Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa.

Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam.

Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo.

Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni?

Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi.

Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka.

Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano.

1572979444665.png

Abdulrauf Songea Mbano

Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija.

Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k.

Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni: “Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k.

Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.
Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.''

1572979353103.png

May Day,
Mimi nimeandika historia ya wazee wangu na ikiwa wewe huamini na unaona nimetunga uongo si neno.

Wengi waliamini historia ya Chuo Cha CCM Kivukoni kwa miaka mingi na haikuwa kitu.
 
Laki...
Rashid Kawawa nitakupa historia yake ili umfahamu.

1950 Kawawa alikuwa katika uongozi wa Tanganyika African Government Servants Association (TAGSA)pamoja na Ally Sykes, Dr. Wilbard Mwanjisi, Steven Mhando na Thomas Marealle.

Alikuja baadae sana katika harakati hizi.
Umenichekesha.

Ati Abdul "akaondolewa."

1953 baada ya ule Uchaguzi wa Arnautoglo Hall, Nyerere alichaguliwa President Vice President Abdul Sykes.

Chama kilikufa.

Tatizo linalokukabilieni wengi ni kuwa hamuijui historia ya TANU na Nyerere hakupata hata siku moja kueleza alifikafika vipi Kariakoo na nani walikuwa wenyeji wake.

TAA ilikufa si kwa kuwa Mwalimu alikuwa kiongozi dhaifu la hasha.

TAA ilikosa yale ambayo Executive Committee yalizoea kupata kutoka kwa Abdul kila alipoitisha mkutano.

Ilibidi kwa muda Abdul amsaidie Nyerere ili kurejesha imani ya wajumbe wahudhurie mikutano na chama kirejeshe nguvu na hadhi yake.

Tatizo linalokukabilieni wengi ni kuwa hamuijui historia ya TANU na Nyerere hakupata hata siku moja kueleza alifikafika vipi Kariakoo na nani walikuwa wenyeji wake.
Mwalimu alishaeleza mara kadhaa tena kwenye hadhara jinsi alivyofika Dar, alivyopokelewa na kupelekwa kwa kina Sykes, Dosa n.k.

Wewe ni Mwandishi wa historia kitaaluma hivyo fanya tafiti za kutosha kabla ya kuandika.

Mwalimu alieleza tangu jinsi alivyoambiwa habari za TAA akiwa Makerere, na amewataja waliokuwa wanawasiliana nae na barua tangu akiwa Makerere....sasa kama hukusikia kwa nini unathibitisha kwamba hakuwahi kusema?

Na tofauti na maandiko yako, Mwalimu anawataja Wazee wa Dar Es Salaam kwa ujumla wao, namna walivyompokea na kumuamini ndani ya kipindi kifupi, sipingani na ukweli kulikuwa na nafasi ya kina Sykes na wengine lakini bado kulikuwa na kundi kubwa nyuma ambalo huonekani kabisa kujishughulisha nalo kwenye maandiko yako zaidi ya kujikita kwa kina Sykes brothers.

Na sidhani kama kina Sykes walikuwa wanaishinda nguvu ya Wazee wale wa Dar Es Salaam.

Si vibaya kuelezea mchango wa kina Sykes, ila kiukweli Mzee Said unapotosha sana historia, na huo ndio ukweli.
 
Kinyungu,
Ili uelewe Vita Vya Maji na matokeo yake katika historia ya Waafrika wa Tanganyika katika kupambana na ukoloni inabidi nikuchukue hadi Mahenge, Songea kwenye Makumbusho ya Vita Vya Maji:

''Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa.

Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam.

Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo.

Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni?

Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi.

Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka.

Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Abdulrauf Songea Mbano.

View attachment 1254996
Abdulrauf Songea Mbano

Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija.

Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k.

Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni: “Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k.

Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.
Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.''

Mzee Mohamed nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa lakini siafiki kusema vita ya maji maji haikuwa vita ya kizalendo. Vita ile ilikuwa ya kizalendo ima Wenyeji walikuwa Waislam, Wapagani au Wakristu. Ukweli unabaki vita ilikuwa ya kizalendo, wazalendo wazawa wakipigania nchi yao dhidi ya uvamizi uliokuwa ukiendelea wa Kijerumani.

Kwa vyovyote Wajerumani wasingekosa wenyeji wa kushirikiana nao na miongoni mwao walikuwapo waislam, wakristu na wapagani japo kwa uchache. Tunapozidi kuisemea vita hii kwa mrengo wa kidini hatuisaidii nchi yetu wala hao tunaotaka wapate historia sahihi kama tunavyodhani
 
Mwalimu alishaeleza mara kadhaa tena kwenye hadhara jinsi alivyofika Dar, alivyopokelewa na kupelekwa kwa kina Sykes, Dosa n.k.

Wewe ni Mwandishi wa historia kitaaluma hivyo fanya tafiti za kutosha kabla ya kuandika.

Mwalimu alieleza tangu jinsi alivyoambiwa habari za TAA akiwa Makerere, na amewataja waliokuwa wanawasiliana nae na barua tangu akiwa Makerere....sasa kama hukusikia kwa nini unathibitisha kwamba hakuwahi kusema?

Na tofauti na maandiko yako, Mwalimu anawataja Wazee wa Dar Es Salaam kwa ujumla wao, namna walivyompokea na kumuamini ndani ya kipindi kifupi, sipingani na ukweli kulikuwa na nafasi ya kina Sykes na wengine lakini bado kulikuwa na kundi kubwa nyuma ambalo huonekani kabisa kujishughulisha nalo kwenye maandiko yako zaidi ya kujikita kwa kina Sykes brothers.

Na sidhani kama kina Sykes walikuwa wanaishinda nguvu ya Wazee wale wa Dar Es Salaam.

Si vibaya kuelezea mchango wa kina Sykes, ila kiukweli Mzee Said unapotosha sana historia, na huo ndio ukweli.
May Day,
Naona unapenda tuendelee na mjadala huu licha kukuambia kuwa ikiwa unaona mimi nimeandika uongo si neno.

Nilitegemea hapo ndiyo utakuwa mwisho wa mjadala wetu.

Kuwa Mwalimu kusema mara kadhaa jinsi alivyopokelewa Dar es Salaam hili si kweli na kama una ushahidi uweke hapa tunufaike sote.

Ukweli ni kuwa Mwalimu kawaadhimisha waliompokea mara moja tu katika hotuba yake ya Ukumbi wa Diamond na alipomtaja Abdul Sykes akasema ''anadhani,'' Abdul alikuwa katibu wa TAA.

Mwalimu hakuwa na uhakika wa nafasi ya uongozi wa Abdul Sykes katika TAA.

Mimi nakuwekea uongozi wa TAA Mwalimu alipoingia madarakani katika uchaguzi wa tarehe 17 April 1953 uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo:

''In June, TAA headquarters announced its executive committee with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.''[1]
[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

May Day,
Naona anaehitaji kufanya utafiti kabla ya kuandika ni wewe si mimi.

Mimi nimesoma kila kitu unachokifahamu wewe kuhusu Julius Nyerere ni vichache sana vimenipita lakini kubwa na muhimu sana ni kuwa nimemsoma Nyerere katika Nyaraka za Sykes.

Ukimtoa Ally Sykes mimi nimezungumza na watu waliokuwapo katika harakati za TAA kabla hata Nyerere hajafika Dar es Salaam.

1573009391478.png

Dome Okochi Budohi TANU card no, 6 na Mwandishi Nairobi 1972

Mwalimu sitamsemea kwa yeye kuwajumuisha Wazee wa Baraza la TANU bila ya kuwataja majina yao angalau wazee kama Mshume Kiyate na Sheikh Suleiman Takadir aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la TANU.

Nadhani hujasoma kitabu cha Abdul Sykes kwani kama ungesoma ungewakuta wazalendo wengi ambao nimewaeleza kwa kirefu sana.

Nimeeleza historia ya Iddi Faizi Mafungo na nduguye Iddi Tosiri na kaka binamu yao Sheikh Mohamed Ramiya.

Hawa ni kutoka Dar es Salaam, Eastern Province.
Nimeeleza historia ya Haruna Taratibu na Omari Suleiman kutoka Dodoma, Central Province.

Nimeeleza historia ya Yusuf Chembera na Salum Mpunga kutoka Lindi, Southern Province.

Kitabu cha Abdul Sykes kimejaa wazalendo ambao wewe hukupatapo kuwasikia hata siku moja lakini ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika katika maeneo yao.

Kuhusu wazee wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee alikuwa Shekh Suleiman Takadir (1954 - 1958) baada ya ugomvi wa Sheikh Takadir na Nyerere mwaka wa 1958, Sheikh Takadir akafukuzwa chama na nafasi yake ikachukuliwa na Iddi Tulio hadi 1963 Baraza la Wazee lilipovunjwa kwa shutuma ya kuchanganya ''dini na siasa.''

Juu ya hili Baraza la Wazee wa TANU alikuwapo kiongozi mkubwa wa hao wote - Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Sheikh Hassan bin Ameir mwaka wa 1950 alikuwa mjumbe katika TAA Political Subcommittee pamoja na Hamza Mwapachu, Abdul Sykes, Steven Mhando, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Said Chaurembo na John Rupia.

Nyerere alijulishwa kwa Sheikh Hassan bin Ameir na Abdul Sykes alipompeleka kwenye Madras yake Mtaa wa Amani.

Hao wote wazee ndani ya Baraza la Wazee wengi wao Nyerere aliwafamu kupitia mgongo wa Abdul Sykes.

Sheikh Hassan bin Ameir na wale wote waliokuwa nyuma yake walimuunga mkono Nyerere hadi uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.
 
Mzee Mohamed nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa lakini siafiki kusema vita ya maji maji haikuwa vita ya kizalendo. Vita ile ilikuwa ya kizalendo ima Wenyeji walikuwa Waislam, Wapagani au Wakristu. Ukweli unabaki vita ilikuwa ya kizalendo, wazalendo wazawa wakipigania nchi yao dhidi ya uvamizi uliokuwa ukiendelea wa Kijerumani.

Kwa vyovyote Wajerumani wasingekosa wenyeji wa kushirikiana nao na miongoni mwao walikuwapo waislam, wakristu na wapagani japo kwa uchache. Tunapozidi kuisemea vita hii kwa mrengo wa kidini hatuisaidii nchi yetu wala hao tunaotaka wapate historia sahihi kama tunavyodhani
Kinyungu,
Una uhuru wa kuamini upendavyo.

Mimi nakueleza historia kama ilivyokuwa ili ujue yale ambayo hayaelezwi kwenye historia rasmi na hujayasoma popote.

Usingemjua Songea Mbano kuwa jina lake ni Abdulrauf hadi nilipokueleza.
Hii imeongeza elimu yako.

Kwa nini jina alilopewa na baba yake halitajwi huo utafiti nakuachia wewe.
 
Sheikh Mohamed Said na mm siyo mchache wa historia ya hawa Mashujaa wa Maji maji kiivyo. Mtemi Abdulrauf na wenzake nimezisikia habari zao miaka zaidi ya kumi iliyopita na kwa maelezo niliyopata naridhika kwamba walikuwa Waislam. Hilo nafahamu vyema. Lakini nakukatalia unavyotia chumvi na kutaka kuonesha kana kwamba hawa mashujaa walipigana vita kwa mrengo wa dini tu na siyo katika kutaka kulinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Wazungu wa Kijerumani.

Kumbuka hata Waarab na Washiraz walipokuja walitawala maeneo ya wenyeji. Hatujui ni kwa kiasi gani wenyeji waliwapinga hadi pale walipokubali utawala wao na hatimaye kusilim. Hilo nakuachia maana hili unalotaka kulisisitiza lina pande mbili. Tutarudi hadi 1000AD kutaka kujua wenyeji waliwapokeaje wageni toka Arabia kwenye pwani ya nchi yetu
 
Sheikh Mohamed Said na mm siyo mchache wa hisyoria ya hawa Mashujaa wa Maji maji kiivyo. Mtemi Abdulrauf na wenzake nimezisikia miaka zaidi ya kumi iliyopita na kwamba walikuwa Waislam nafahamu vyema. Lakini nakukatalia unavyotia chumvi na kutaka kuonesha kana kwamba hawa mashujaa walipigana vita kwa mrengo wa dini tu na siyi katika kutaka kulinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Wazungu wa Kijerumani.

Kumbuka hata Waarab na Washiraz walipokuja walitawala maeneo ya wenyeji. Hatujui ni kwa kiasi gani wenyeji waliwapinga hadi pale walipokubali utawala wao na hatimaye kusilim. Hilo nakuachia maana hili unalotaka kulisisitiza lina pande mbili. Tutarudi hadi 1000AD kutaka kujua wenyeji waliwapokeaje wageni toka Arabia kwenye pwani ya nchi yetu
Kinyungu,
Sina ninachosisitiza.
Naeleza historia kama ninavyoifahamu na si lazima ukubaliane na mimi.

Wewe umamjua Abdulrauf Songea Mbano miaka 10 iliyopita.
Mimi nimemtaja katika kitabu cha Abdul Sykes miaka 21 iliyopita.
 
Yapo mengine hapo chini ambayo huenda hukuwa unayajua:

SULTAN ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
JINA LAKE NI ABDULRAUF SONGEA MBANO SIYO SONGEA MBANO SULTANI WA WANGONI WAKATI WA VITA VYA MAJIMAJI 1905 - 1907
 
ABDULWAHID SYKES KATIKA "THE MAKING OF TANGANYIKA" NA JUDITH LISTOWEL
Maggid Mjengwa:
Judith anaeleza pia kushindwa kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa T. A. A. Jambo hili ningependa Mwalimu wangu Mohamed Said alitolee maoni yake juu ya tafsiri ya jambo hilo.

Mwenyekiti,
Maggid Mjengwa Mwenyekiti kuna kitu kidogo umekosea katika swali lako.

Ulitakiwa uulize hivi, ''Judith anaeleza pia kushindwa kwa kura chache kwa Abdul Sykes kwenye kugombea urais wa TAA."

Ungeuliza hivi swali la kwanza kwa msomaji angejiuliza kwa nini Nyerere alishinda kwa kura chache?

Abdul laiti angegombea uchaguzi ule kwa nia ya kushinda angeshinda bila wasiwasi wowote.

Abdul angeshinda kwa kuwa Nyerere hakuwa anajulikana na mtu yoyote ukimtoa yeye mwenyewe Abdul, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Ukiangalia vipi uongozi wa TAA ulibadilishwa mwaka wa 1950 utaona Schneider ndiye aliyesimama kumwondoa kaka yake Thomas Plantan kwenye uongozi na akawaingiza Abdul na Dr. Kyaruzi.

Kabla ya uchaguzi ule wa April 1953 Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe alikwenda Nansio,

Ukerewe kwa Hamza Mwapachu ili apate kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu Nyerere, kuwa bado ana fikra kuwa Nyerere atiwe katika uongozi wa juu wa TAA na 1954 waunde TANU na Mwalimu aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika?

Jibu la Mwapachu lilikuwa Abdul amsaidie Nyerere kuingia katika uongozi wa juu wa TAA na amsaidie kupata ushindi na mwaka unaofuatia TANU iundwe na Nyerere awe kiongozi wa harakati za uhuru.

Sababu aliyotoa kumpa Abdul ni kuwa yeye alikuwa anaona Nyerere anafaa zaidi kwa uongozi wa TANU kuliko Abdul lakini akaongeza kueleza kuwa Abdul kama Muislam kuongoza harakati za uhuru zitawazidishia Waingereza ukaidi kwani wanaweza wakachukua harakati za uhuru kama vurugu nyingine za Waislam mfano wa Vita Vya Maji Maji vya 1905.

Kwa siasa za nyakati zile bila ya Nyerere kukubalika na wenyeji wa Dar es Salaam Abdul akiwa mmoja wa hawa wanamji, Nyerere asingeweza kushinda uchaguzi ule.

Hivyo basi ndani ya ile ''inner circle ya inner circle,'' ya TAA ndani ya TAA Political Subcommittee uamuzi ulipitishwa kuwa Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule.

Laiti viongozi hawa wangefanya khiyana ya kumkataa Nyerere kwa sababu yeyote ile wangekuwa wamefanya kosa kubwa sana.

Nyerere aliiongoza TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika kwa ustadi na ufanisi mkubwa sana.

Abdul Sykes hakumueleza Listowel haya na kwa miaka mingi historia hii hakuna aliyekuwa anaijua hata Nyerere mwenyewe hakupata kusema kuwa kwanza alipokelewa na Abdul Sykes na pili kuwa alipata kugombea urais wa TAA dhidi ya Abdul Sykes.

Siku Mwalimu alipotaja jina la Abdul Sykes hadharani katika hotuba yake ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond mwaka wa 1985, Mwalimu alisema ''anadhani'' Abdul Sykes nafasi yake katika TAA alikuwa Katibu.

Mwalimu hakuwa na uhakika na historia ya uongozi wa Abdul katika TAA ilibidi adhanie.

Ningependa kuhitimisha kwa kusema kuwa aliyemweleza Listowel historia ya uchaguzi ule baina ya Abdul Sykes na Julius Nyerere alikuwa Denis Phombeah ambae ndiye alikuwa Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo ulipofanyika uchaguzi ule na yeye akawa ndiyo Returning Officer.

View attachment 1253270
Denis Phombeah
Hakika historia ni nzuri. Nimefurahi na kufarijika baada ya kuupitia kwa makini uzi huu. Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom