Abdallah Mwinyi ni kiongozi makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abdallah Mwinyi ni kiongozi makini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Aug 8, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Huku viongozi wazalendo na makini wakiwa wanapungua siku hadi siku katika chati za uongozi wetu wa kitaifa inatia moyo pale tunapoona viongozi vijana wakiwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya taifa katika nafasi zao mbali mbali.

  Katika bunge la Afrika Mashariki, mbunge wetu Abdallah Mwinyi, amekua mstari wa mbele katika kutetea maslahi yetu ya taifa ukijumlisha michango yake ya mara kwa mara ndani ya bunge hilo (ambapo wabunge wetu wengine wamekua siyo wachangiaji wazuri).

  Kutoka kutetea kasi yetu ya kujiunga na soko la pamoja ndani ya bunge hilo ambapo nchi za jirani haswa Kenya na Rwanda walikua wanatukaba shingo kufungua mipaka yetu kwa bidhaa zao, hadi kutetea ongezeko la vibali vya kazi kwa wafanyakazi wageni nchini na kusema kua vibali hivyo ni kwa wafanyakazi wote wakiwemo wa nchi wanachama wa EAC huku akijibu kwa umakini mzuri lawama za wabunge wa nchi hizo jirani ni mfano mzuri wa umakini wa huyu mheshimiwa.

  Ni vizuri tuanzishe utamaduni wa kuwapa pongezi viongozi wetu wachache wa kitaifa wanaposimamia kazi zao kwa umakini na uzalendo. Pongezi kwa kazi nzuri Mh. Mwinyi, tunategemea kuona mchango wako zaidi katika uongozi wa taifa letu miaka ijayo baada ya kumalizia muda wako EALA hapo 2017.


  Mharakati
   
 2. DONNYANGAKA

  DONNYANGAKA JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 331
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Unaweza kutunukulia alichokisema kabisa ili tufurahi na kumpongeza pamoja!
   
 3. N

  NOD JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 80
  Abdallah hajawahi hata siku moja kuwa mtetezi wa Tanzania zaidi ya kuwa kibaraka wa Speaker aliyepita wa Bunge la Afrika Mashariki. Ki ukweli hao walioachwa ndio walikuwa watetezi wazuri wa Tanzania na wachangiaji pia. Tembelea Arusha na uongee na watu was EAC wakwambie ukweli. Mama Mmari na Mzee Masha na wengine ndio wangesistahili sifa hizi. Aliyosema Mwakembe ni siasa tu na zitatu-cost.

  I stand to be stoned kama hii team mpya itakuwa na uwezo zaidi ya hao waliopita!
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hivi mleta maada ndio kaleta akiwa chakari nini au ndio ujiko wa bure anataka kumpa mtoto wa mzee Ruksa,kwani huo uzalendo ni upi ambao huyo mheshimiwa anaufanya kwenye hilo bunge,tuache porojo za kusifiana hapa JF,ni aibu kwa mtu na akili zake kuja hapa na kujenga hoja hasi kuwa mtu fulani ni mzalendo bila kutwambia hilo jambo alilolifanya na kulifanikisha kwa maslahi ya TZ,kama kampeni semeni tu mumeanza,kwani wenye haki na uongozi wa nchi hii ni baba na watoto wa vigogo wa serikali,kuanzia tunazaliwa tunazisikia koo zenu tu zikijirudia rudia kwenye uongozi mmekuwa machifu
   
 5. m

  mharakati JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kaka taratibu unaonekana una jazba na kitu kingine kabisa na unaunganisha na thread yangu..kama huna cha kuchangia kuhusu niliyoandika moja kwa moja jaribu kukaa pembeni kama wenzako wengi waliosoma na kuacha uchangiaji kwa sababu zao. haikua lazima kuchangia kaka
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  angalia gazeti la daily nation la kenya at least online version
   
 7. m

  mharakati JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mwinyi amekua ngangari na mambo haya muhimu ya economic integration ndiyo maaana namuangalia kwa karibu...wengine wanapiga kelele hapa na pale kuhusu hili au lile huyu jamaa amekua na mwelekeo mmoja na amejikita kuutetea kwa kila hali bungeni pale hata akiwa analobby wenzake huku tz wasapoti msimamo fulani anaohisi hawaujui au hawaupi kipaumbele sawa sawa
   
 8. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Toa specific instance ametetea economic integration. Kila kukicha uongozi Tanzania unazidi ku isolate nchi, mfano juzi tu wameongeza kiwango cha work permit fee.(Kenya ili waiver/ondosha malipo work permit kwa raia wa EA tangu 2011 kupitia gazzete notice). Tanzania commitment to integration is suspect and cause of inconvinience kwa watanzania wengi ambao tumeuamua kuchangamkia fursa za soko la pamoja EA.
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama ni wewe mwenyewe/au amekutuma basi mjue kuwa mnabebwa kwasababu ya majina ya baba zenu na wala sio uwezo wenu!! Hilo liko wazi hata kwa kaka yake Hussein ambae ameshindwa kuongoza wizara zote alizopangiwa ila anabebwa na mkweree kulipa fadhila alizopewa na babae!! Hawa wabunge wa EA waliopo sasa hivi ni aibu kwa nchi yenye wasomi wazuri lakini inaathirika na mizengwe ya chama cha magamba!!
   
 10. m

  mharakati JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Work permit kwa EAC members hazipo Kenya na Rwanda kwa sababu wenyewe ndiyo member states wenye national id system. Uganda,burundi na tz hawana hii kitu na wakenya na rwanda wanalalamikia kwa nini tz inaweka na kuongeza hizi permits. Hii moja ya economic integration issues yaani free movement of labor na yeye ametetea juwepo kwa permits hadi pale tutakapokua na system nzuri ya ID nchini. Katika bunge lililopita Mwinyi alikoa vocal zaidi kwenye floor ya bunge katika mapendekezo ya secretariet kuhusu mambo mengi ikiwemo common external tarrifs huku wabunge wetu wengi wakiwa mute.

  siwezi kumtetea kama ni anakwamisha integration kwa sababu hiyo ndiyo policy ya tz kwa ujumla, hatuwezi kujiingiza kwenye mambo ya ushirikiano zaidi wakati nyumba yetu haijakaa sawa. na siipingi kabisa hii policy. its tye right policy na wabunge wetu makini inabidi waitetee vilivyo na ndivyo Mwinyi anachofanya tofauti na wengine walioenda kupumzika kwenye bunge
   
 11. m

  mharakati JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  La hasha ungejua mimi nasimama wapi usingesema haya, ila unaonekana ni mtu subjective sana wewe na hapa hatuwezi kuelwana zaidi ya kuanza personal attacks..jazba na ushabiki umekujaa na hii thread si ya aina hiyo.
   
Loading...