kumbe ndo huyu mwamba.
nakumbuka Ally choki alikuwa anampaisha sana"bitembo air ka"
Sent using Jamii Forums mobile app
Abdallah Bitembo ni mchezaji aliyeichezea timu ya CRDB FC Arudha ilipokuwa daraja la kwanza na hatimaye Meru FC,alicheza ligi enzi kukiwa na timu 16 kwenye ligi kuu,anaelezea kwamba hakuweza kwenda kucheza simba au Yanga maana kule kulikuwa na vipaji vikubwa wakati huo kama kina Lunyamila.
Anaelezea mpira haukumpa maisha mazuri hivyo aliamua kwenda kufanya kazi kwenye saloon ya kaka yake dar ,wakati huo mashine za kunyoa hazitoka ,na wateja wake wengi walikuwa wachezaji kwa sababu alikuwa anawanyoa walipokuwa kwenye ligi na hivo akafungua saloon yake mwenyewe "BITEKO SALOON".
Kwa sababu saloon yake ilijulikana kwa wachezaji basi aliweza kupata wateja ambao ni masters wa bongo kama kina Alichoki,Nyoshi El Sadat na pia walimrusha kwenye nyimbo zao na kujulikana zaidi.
Kwa wasanii waigizaji msanii wa ambaye ni mteja wake wa kudumu ni Vicent Kigosi ,kigosi akamleta kanumba na sasa hivi wasanii wengi wa bongo fleva wananyoa kwakwe.Pia alimnyoa Koffi Olomide alipokuja bongo.
Kwenye miaka ya 2000 mwanzoni alipelekwa Dubai na mchezaji wa Coastal Union ambaye ana asili ya kiarabu ,alienda kunyoa Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka 3 na kusomea mambo ya urembo wa nywele (certificate).
Kwa sababu enzi hizo Geogre Weah alikuwa anacheza falme za kiarabu na kati ya saloon za kiafrica saloon aliyokuwa anafanyia kazi ilikuwa na jina basi alikuwa anamyoa George Weah ambaye kwa sasa ni Rais wa Liberia.View attachment 1458955View attachment 1458956
Alienda Abu Dhabi na si Saudi Arabia. Btw jamaa alijua anachotaka. Sikupoteza muda jana kwa kweli kutizama The Mboni Show kwa siku ya jana. Kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa jamaa
Sent from my iPhone using JamiiForums
nakumbuka miaka ya nyuma mitaa ya koma koma kulikuwa na babashop imeandikwa jina kama hili kati ya "bitebo" au "bitembo" ila sikumbuki vizuri ila nishawai kuona karibu na kituo cha daladala.Ndo mwenyewe aisee
Ni Bitebo labda mambo ya keyboardnakumbuka miaka ya nyuma mitaa ya koma koma kulikuwa na babashop imeandikwa jina kama hili kati ya "bitebo" au "bitembo" ila sikumbuki vizuri ila nishawai kuona karibu na kituo cha daladala.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi leo ipo ya kwake ile!nakumbuka miaka ya nyuma mitaa ya koma koma kulikuwa na babashop imeandikwa jina kama hili kati ya "bitebo" au "bitembo" ila sikumbuki vizuri ila nishawai kuona karibu na kituo cha daladala.
Sent using Jamii Forums mobile app
kumbe.jamaa mpambanaji sana.vijana kama hawa ni mfano mzuri wa kuiga kwa mtu kama mimi.mwenye akili ya kupiga pumbu tu sina mbele wa nyuma.
Stori yenyew ilikuwa ya Jana kwenye kipindi cha the mboni show,,, na alisema anakaribia 50Jamaa alicheza na kina Lunyamila lakini wachezaji wa enzi hizo lakini ukimwangilia kwa sasa umri wake ni kama kwenye 40+
Yupo lango la jiji magomen kondoaNi Bitebo labda mambo ya keyboard