Aadhibiwa kwa kusujudu uwanjani

Aadhibiwa kwa kusujudu uwanjani

Status
Not open for further replies.

shortlisted1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
352
Reaction score
128
Hii imetokea huko amerca kwenye mchezo wa american football. Mchezaji huyo muislamu alishangilia kwa kusujudu baada ya kufunga bao kwenye mchezo huo. Tukio hili limeacha sintofahumu kubwa kwa mashabiki wa mchezo huu kwani kabla ya tukio hilo wapo watu walishangilia kwa ishara za KINASWARA(KIKRISTO) lakini referee hakuwachukulia hatua yoyote watu hawa, hii imeonyesha jinsi gani watu walivyo na ubaguzi mkubwa na chuki dhidi ya dini hii ya haki.

Chama hicho cha mpira kimetakiwa kuweka wazi kanuni zake za mchezo maana haiwezekani wakifanya wakristo iwe sawa lakini kwa waislamu isiwe sawa(double standards). Mwisho napenda kuwaa angalizo wamerekani kwamba uislamu unasmabaa kwa kasi sana huko kwenye nchi yenu kwa kuwa ni dini ya Alaah na ni dini ya haki.......MAHALI INAPOFIKA NURU LAZIMA GIZA LIPOTEE.
=============

Mchezaji wa Kansas City Chiefs Husain Abdullah aliadhibiwa vikali na refarii baa da ya kupiga sijida baada ya kufunga bao katika mchezo wa soka ya Marekani Kansas walipoinyuka New England Patriots 41-14. Refarii alimwadhibu papo hapo Abdullah alipoinuka baada ya kusheherekea kwa kupiga sijida. Aliyekuwa refarii wa zamani wa NFL Mike Pereira alisema kuwa sio hatia mtu kupiga sijida.
Tukio hilo linawadia wakati ambapo ligi hiyo inapigwa msasa kufuatia utovu wa nidhamu mbali na tuhuma chungu nzima kuhusiana na wachezaji wa ligi hiyo.

Tayari wandani wa NFL wanadai kuwa kuna upendeleo kwani mchezaji mwengine nyota Tim Tebow hakuadhibiwa baada ya kuonesha ishara yake al maarufu "Tebowing" msimu wote wa mwaka wa 2011.
Abdullah amejitokeza kutetea dini yake ya Uislamu sawa na vile Tebow huonesha wazi kuwa ni Mkristo.

Aidha Abdula alihiji mwaka uliopita alipoambatana na kakake Hamza,kuenda kwa hajji huko Mecca.
Kwa mujibu wa washika dau wanaishauri NFL itangaze wazi msimamo wake kuhusiana na ishara za kidini ilikutoa utata unaoibuka .
Chanzo:BBC
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom