Aaaaaaa natamani kupata ndio kikwazo nifanyejeeee?

Aaaaaaa natamani kupata ndio kikwazo nifanyejeeee?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
1. Niliondoka nyumbani, kwa hali ya kunyatia,
Na bunduki mkononi, na risasi nimetia,
Nikajitosa mwituni, nyama kujitafutia
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

2. Nilikua na yakini, minofu ntajipatia,
Kwani bunduki jamani, najua kuitumia,
digidigi vichakani, wote wananitambua,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia

3. Nilipopita mbugani, nipate kuangalia,
wanyama walibaini, swala na pundamilia,
nikaiunda plani, nipate kuwafikia,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

4. Mara yakatabayani, nisiyoyategemea,
askari wa porini, ngumu akanitilia,
kasema itue chini, bunduki nakuambia,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

5. Japo nyama watamani, siwezi kukuachia,
kumbuka kuna kanuni, ukweli tunaujua,
budi ukate leseni, ya hao ulochagua,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

6. Nikajiinamia chini, hali nikifikiria,
sasa nirudi nyumbani, bunduki sijafayatua?
Hii ni balaa gani, mwindaji yanifikia,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

7. Kutundika ukutani, bunduki yaning'inia,
Ninakua mashakani, kutu isijeingia,
nisijekwenda windoni, ikashindwa kufyatua,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

8. Swala namwona porini, kulenga wanizuia?
sasa pesa za leseni, nani atanigawia,
si mia wala miteni, ni nyingi yahitajia,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

9. Askari mhisani, nakuomba fikiria,
hizo siku za mbeleni, nashindwa kuzingojea,
bunduki i hatarini, itajashindwa kulia,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

10. Nami sipendi utani, kuwinda nikinuwia,
Na hasa risasi ndani, ikiwa nimeshatia,
Ningali najiamini, swala wengi ntatungua,
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.

11. Kalamu natua chini, pasipo kujizuia,
Na mikono mashavuni, ambayo naegamia,
Nitumie hila gani, tatizo kulitatua?
Askari wa mwituni, kuwinda kanizuia.
 
:typing::typing::typing::typing:......................................
 
Denotative vs conotative meaning!!!! Where to stand for?
 
Back
Top Bottom