A220-300 / CS 300

Sijazungumzia mashoga wala mabeberu mkuu kwa sababu mimi sio shoga wa jike(la mbuzi).

Concern ni kama hiyo ndege ilishawahi kumilikiwa na airBaltic ama walicancel order tukaichukua?
Mkuu kuna nchi tayari zinamiliki hizi kitu!
 
Hizo nadhani ni Letter Codes za usajili kiwandani zinazotolewa mara ndege inapofikia hatua za kuunganganishwa na baadaye kuruka kwa mara ya kwanza. Inawezekana zikawa zinajirudia kulingana na matoleo ya ndege kwa mwezi, kwa sababu C-FOWU iliishawahi kuandikwa kwenye ndege ya Korea CS300 yenye msn 55022 iliyotolewa tarehe 25-01-2018 pamoja na ile ya Air Baltic msn 55005 C-FOWU iliyotolewa tarehe 31-3-2017.....

Inayofuata kwenye mtiririko huo ni Air Tanzania. Ile ya pili msn 55048 imepewa herufi za usajili C-FOUY ambayo tayari iliishatumiwa na msn 55034 CS300 ya Air Baltic iliyotolewa 16-06-2018.

Huko nyuma zaidi hizi codes mbili za C-FOWU na C-FOUY ziliishawahi kutumika kwa ndege za kampuni-mama: Bombardier Aerospace katika matoleo ya CS300 za mwanzo. Naamini huu ni utaratibu wa kiwandani ambao unakuja kurithiwa na namba halisi za usajili kama ilivyo 5H-TCH. Mimi sio msemaji wa kampuni husika, nimejaribu tu kushirikisha wengine kwa kile ninachokijua.
bingwa umechambua kisomi sana pasipo shaka upo ktk sekta ya aviation
 
bingwa umechambua kisomi sana pasipo shaka upo ktk sekta ya aviation
Hapana mkuu, mimi ni mpenzi tu wa mambo yote yanayohusu usafiri wa anga, anga za juu na vyombo vya angani. Napenda pia kujifunza mengi yanayo tuzunguka..
 
Back
Top Bottom