A shameful battle field

Lukuvi aliuliza Makondakta ni nani katika serikali hii? Sasa yako wapi? Hapa tunamtaka waziri wa elimu atende haki! Hapa tunamtaka Rais wa JMT atende haki! Inaniuma sana ninavyomkumbuka rafiki yangu Mwl. Robert alivyotimua mbio kukwepa mkono wa sheria kutokana na kutumia cheti cha mtu mwingine kujipatia ajira mpaka akawa mwalimu mkuu!! RC naye aoneshe vyeti vya Bashite hapa! Na Paul Christian kule aliko anyamaze kabisa maana na yeye anaweza kuingia kwenye mkono wa sheria, bora ajikalie kimya ili siku akihitajiwa mahakamani akaseme alibiwa cheti chake!
 
Huku kwetu ya Makonda hayatuhusu.
Yanawahusu nyinyi wa kutwa kucha mitandaoni.
Na siamini kama mnafika hata robo yawatanzania
Mkuu umejiunga baada ya tuhuma za mkulu wako ili uje kuongeza nguvu za kutetea?...kama wanaomkosoa hawafiki robo kinachomliza ni nini?...Inaoenekana huguswi na hali ya watumishi makazini sasa ivi kwa matatizo haya haya ya vyeti...
 
Who ever go to the equity must go with clean hands
 
Naguswa na nguvu kazi yataifa inayopotea kwa dawa za kulevya
 
Ila kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba hakuna aina ya elimu inayohitajika ili kuteuliwa kuwa RC, nikikumbuka vizuri hata Baba wa taifa aliwahi kumteua Mkuu wa Mkoa wa Dar ambaye alikuwa Dereva Taxi pale Magomeni....Hivyo ningekuwa mimi ndo Mkuu wa Nchi hii, hakika nisinge Mwajibisha Mh. Makonda kwasababu hizo na ukizingatia kama kila ninalomuagiza anatekeleza basi huyo kwangu anafaa
 
Rationaliser kimsingi umefafanua kila jambo kwa hekima na busara sana. Shida ya yule dogo aliona njia nyeupe kwake kusonga mbele. Hakuuona hata utelezi alipokuwa akipita kwenye tope litokanalo na mvua. Hakujua kwamba kosa namba moja ilikuwa ni kumcharaza yule babu yake pale ubungo plaza. Hakujua kama hakuna adhabu mbaya kama itolewayo na Mungu pale muumizwaji anapo surrender hukumu ile kwa Mungu. Hata hivyo adhabu alokwishapata inamtosha. Ushauri wangu wa bure a jipe ujasiri wa ku confess tu. Watanzania ni watu wenye huruma sana watamsamehe tu. Ila akishasamehewa ajifunze
 
Endeleeni kutoa povu, na bahati mbaya watanzania wamewapuuza. Makonda anawalaza na viatu.
 
Wacha u naibu waziri mmfanye vice Presidwaa kabisa. Lakini vyeti mezani kwanza. Halafu inaonyesha ulivyo mbumbumbu wa sheria. Bila kuwa mbunge hawezi kuukwaa u naibu waziri. Labda ateuliwe kwenye ile nafasi ya mwisho iliyobaki. Otherwise itabidi kamanda Siro akusake kwa viroba. Sijui umevipata wapi?
 
Moja ya upumbavu ni kuchukulia kila mtu anaye taka ukweli uwekwe wazi dhidi ya tuhuma hizi za RC kuwa ni upinzani. Basi kama ni kweli,wapinzani wana hoja ya msingi kuliko wewe na wenzio team Lumumba.
 
Mange Kimambi kasema Maombi kwa rc ni sawa lkn yaelekezwe kwa nani?. Manake tuna Daud Bashite na Paul Makonda, na ktk maombi lazima utaje jina halisi la mlengwa. Rc taja jina uombewe nalo.
Inawezekana ndo maana vyeti havibadiliki majina. Wrong diagnosis wrong prescription
 
Huelewi hata kinachoongelewa.

Hawazungumzii ufaulu au kiwango cha elimu, hapa kinachoongelewa ni kukosa uaminifu, kughushi, kudanganya, na kisha kusoma kwa kutumia cheti kisichokuwa chake. Kama ni kweli, hii ni jinai.

 
Gazeti la mwanahalisi la leo ndio habari ya mjini. He can choose to give up or live in a great shame for the rest of his regime.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…