Kwanza, sina uhakika kama roho inaongeleshwa mara nyingi hivyo kama ulivyosema, ila ninachofahamu ni kuwa nafsi huweza kusemeshwa, kuzungumza na kupigana katika ulimwengu usioonekana.
Roho inabaki kuwa chanzo kikuu cha nishati cha mwili, kinachoupa nguvu na UHAI. Wapo wanaoamini kuwa roho ndio njia kuu ya kuwasiliana na muumba kwa maombi, sala, kufunga, n.k.
Bila roho, hakuna uhai.
So, yah, mtu akifa roho hurudi kwa muumba wake, (creator) mwili unabaki ardhini kwa sababu ni makapi, hauna maana tena, unaoza.
Nafsi ndio huendelea kuishi, na huweza kutafuta au kutafutiwa mwili mwingine kwenye ulimwengu huu huu au mwingine.
Wanaoamini kuna multiverse (malimwengu) wanalijua hili, au wale wanaoamini namna ya kusafiri kiimani kutoka galaxy moja hadi nyingine wanayajua haya zaidi yangu.
Mwili, Nafsi na Roho ndio vinavyomfanya binadamu aendelee kuishi.
NB: ukionaa mnyama ana tabia za utashi, kama mwanadamu, kuwa makini, huenda ni mnyama husika ila ameingiliwa na nafsi ya kiumbe mwingine kutoka ulimwenguni anayetamani kuishi katika dunia au ulimwengu wetu huu.
Kuwa makini.