7 Eleven: Duka lisilofungwa

7 Eleven: Duka lisilofungwa

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
ce2c7f3532eaed065d1f3c0b9f270373.jpg

Ni maduka ya kimataifa. Hata Tanzania yanaweza kuanzishwa.

Ni maduka yasiyofungwa iwe mchana iwe usiku, iwe jumapili iwe sikukuu. Yako wazi 24/7

Yanaitwa Seven Eleven kwa sababu mwanzoni maduka ya Seven Eleven yalikuwa yakifunguliwa saa moja asubuhi mpaka saa tano usiku.

Wazo la kutofunga maduka ya Seven Eleven lilikuja baada ya gemu ya mpira. Wateja walikuwa wengi sana usiku wa siku hiyo.

Ni maduka yanayopatikana karibu na makazi ya watu. Kwa wenzetu hakuna maduka ya rejareja mitaani (kwa mangi)

Ni maduka yanaouza bidhaa za aina nyingi sana ikiwemo chakula, vitafunio, dawa za miswaki, dawa, sabuni, sigara, mpaka oil za magari.

Polisi hawachezi mbali na maduka haya kwa sababu maduka yake yana historia ya kuvamiwa na majambazi. Kwa upande mwingine ni heri kwa sababu polisi wanakuwa karibu na nyumba za watu wakati wa usiku.

Maduka ya Seven Eleven hutoa ajira hasa kwa wanaotafuta kazi ya pili.

Ni maduka yanayotambulika kiserikali hivyo ukusanyaji wake wa kodi ni wa uhakika.

Ni maduka yanayochangamsha miji. Sio Bongo muuza chipsi wa mwisho akifunga kibanda chake saa tano na nusu usiku mji mzima umezima.
 
Hebu kamilisha hbr yako vzuri..!hayo maduka yanapatikana wapi..?nani mmiliki..???kwann wafanyakazi wake ni wale wanaotafuta kazi ya pili...???
 
Hebu kamilisha hbr yako vzuri..!hayo maduka yanapatikana wapi..?nani mmiliki..???kwann wafanyakazi wake ni wale wanaotafuta kazi ya pili...???

Ni franchise kama McDonald. Infact kwa sasa wameizidi McDonald kwa kuwa na maduka mengi duniani.
Wengi wa wafanyakazi wanafanya part time. Ukitoka benki kama mshahara haufiki mwisho wa mwezi jioni unaingia Seven Eleven kuongeza kipato chako.
 
Ni njia moja ya kuiweka Tanzania itambulike katika uchumi wa Dunia. Na bombadia zetu zitakuwa hazikamatwi kwa sababu tutakuwa tunahesabiwa tumo katika uchumi wa dunia.

Now this is a news alert!
 
Tatizo la watanzania hasa viongozi ni kwenda nje kutizama magorofa. Hawarudishi nyumbani chochote wanachokiona nje. Ndio maana hata demokrasia yetu ni ya hovyo hovyo. Hatujifunzi kwa wanaoijua.
 
a292ffc51dbde51301ab73f5e8424160.jpg

Hapo sherrif hapo. Usifikiri ni yule sharifu wa kuombea watu dua. Kwa hawa jamaa sheriff ni bonge la polisi
 
Tatizo la watanzania hasa viongozi ni kwenda nje kutizama magorofa. Hawarudishi nyumbani chochote wanachokiona nje. Ndio maana hata demokrasia yetu ni ya hovyo hovyo. Hatujifunzi kwa wanaoijua.
Kabla ya kulaumu viongozi je unafikiri sie wananchi tupo sawa na wananchi wa hizo unazotaka viongozi wetu wajifunze?
 
Ngoja kwanza wale walio mpiga Lissu risasi wapatikane kwanza, maana tunaweza kufungua duka kama hili ndani ya mwezi ikapigwa bonge moja la uvamisi na watu wasiojulikana na ikwa ndiyo mwasho wa hilo duka

Tatizo siyo viongozi wa ndani kusafiri nje na kurudi watupu, wakuwalaumu ni mabalozi wenu wanao iwakilisha nchi huko ulaya wao mda wote hakuna cha muhimu wanacho kifanya huko kutudokeza ni fursa gani za kiuchumi zinapatikana huko watu wajilipue..

Angalia kama balozi wa china hapa nchini anavyo waleta wachina wenzake kuja kupiga hela kwenye fursa ambazo wabongo hawazioni
 
Ni franchise kama McDonald. Infact kwa sasa wameizidi McDonald kwa kuwa na maduka mengi duniani.
Wengi wa wafanyakazi wanafanya part time. Ukitoka benki kama mshahara haufiki mwisho wa mwezi jioni unaingia Seven Eleven kuongeza kipato chako.
Ok poa nimekuelewa.
 
"Hata Tanzania yanaweza kuanzishwa..."

Anzisha basi...

Diaspora bana... Totally out of touch and clue.
 
Ni franchise kama McDonald. Infact kwa sasa wameizidi McDonald kwa kuwa na maduka mengi duniani.
Wengi wa wafanyakazi wanafanya part time. Ukitoka benki kama mshahara haufiki mwisho wa mwezi jioni unaingia Seven Eleven kuongeza kipato chako.
Nimejikuta napakumbuka Hong Kong...

Ngoja nifanye mchakato...
 
Back
Top Bottom