Watu watatu wamenusurika kifo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya trekta walilokuwa wamepanda kukatika tella na kuanguka.
Tukio hilo limetokea kata ya Namelock Wilayani Kiteto wakati watu hao wakitoka shambani kwenda Kata ya Dongo.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Tumain Magesa akizungumza na majeruhi hosp ya Wilaya ya Kiteto pamoja na kuwapa pole ametoa wito kwa jamii kutotumia trekta kama chombo cha usafiri.
Maeneo mengi Wilayani Kiteto yanatumia trekta kama chombo cha usafiri kubeba abiria na mizigo hivyo wamiliki na madereva hao wametakiwa kutopakia abiria kwenye tella.