3 Idiot : Indian movie

3 Idiot : Indian movie

Halafu ukishamaliza kuangalia movie za ukweli kama hizi uje uniambie niwaelewe BANGE Movie, thubutuu
 
Halafu ukishamaliza kuangalia movie za ukweli kama hizi uje uniambie niwaelewe BANGE Movie, thubutuu

Hahaaaa duh. Mkuu upo kama mimi sizipendi bange movie na sifikirii kupoteza hela yangu kuangalia maigizo yao
 
3 idiot niliipenda pale jamaa walipoenda kumtafuta Rancho mwishoni mwishoni then mshkaji akaenda chobi kumwaga kojo alipigwaje shotiiiiii!!!!
 
Hhhhaaaa nendeni na wakt bhana movie ya muda hyo.
 
Huyu kiumbe huyuuuu
 

Attachments

  • 1422299917972.jpg
    1422299917972.jpg
    9.8 KB · Views: 392
Hahaha muvi za aamir khan ni nzuri sana jamaa huwA hakosei saiv kuna mpya inaitwa PK tafuta uione
 
nlichojifunza katka hii movie ni kwamba sio kila anaepita na cheti kina A za kumwaga ni za kwake!! rancho alikuja kuwa the biggest scientist in the world na wala hana cheti bt experience.

Rancho alisoma kwa ajili ya mtoto wa tajiri ambaye alikuwa anahitaji cheti kwa ajili ya mwanae. Hata jina alilosomea Rancho ni la mtoto wa tajiri. Kwahiyo jamaa alipomaliza chuo akapeleka cheti kwa mtoto wa Tajiri. Ndio maana wakina Raju waliingia ndani ya ile nyumba wakijuwa wamefika kwa jamaa yao. Walikiona cheti na picha lakini si jamaa yao aliyekuwemo kwenye picha !
Producer wa sinema ili kuonyesha kijana ni mjinga, kumbuka lile tukio la kutaka kumwaga vyungu chooni lilofanywa na Raju. Ile sehemu ni nzuri sana
 
Mi nilicheka pale walipopeleka a pee mail kwa viru!!
 
Naipenda sana hii movie, nilikuwa siyo shabiki sana wa movie za kigabachory lakin hii ndo ikafungua pazia ,na tangu hapo nimekuwa nazifuatilia kila napopata nasafi.

Ni movie Nzuri inayoquestion status quo, ikijaribu kuchallange mfumo wa elimu ,wazazi kuingilia maamuz ya watoto katika masomo na mapenz pia.

Kama haujaiona itafute ,u will learn something I guarantee.

Kitu nilichopendea hii movie ni kwamba imelenga hali halisi ya kielimu duniani hasa katika fani ya uhandisi, jamaa (actor) alikua genious aisee kila siku walikua wana kurupushana na prof virus, nilisikitika jamaa alipojinyonga kisa hajafanikisha research yake!! nlipenda zaidi mwishoni pale jamaa (actor) alipotumia elimu ya kihandisi kumsaidia mama flani hivi kujifungua na hapo ndipo prof virus alipomkubali actor japo walikua hawapatani!!

Hii movie ningeshauri sana vijana ambao wanajiandaa na elimu ya chuo kikuu hasa katika fani ya engineering maana itawafungua akili, engineering sio kukariri ma theory tu ila ni kujifunza ni jinsi gani utazitumia hizo theories kutatua matatizo katika jamii, na hili niliona jamaa(actor) alipomaliza na kwenda kufungua shule/academy ya kufundisha engineering kwa vitendo...

Kinngine ambacho ni so interesting ni company ya jamaa na jinsi walivyopendana na kusaidiana!!!Niliipenda na ntaendelea ipenda na kamwe sintaifuta kwenye pc yangu!!! 3 ------ the best...
 
Ndugu post yako imenifanya niirudie tena kuicheki hii movie jana.

Movie nzuri kwa kipindi chote, Amir Khan, Virus, walinifanya nicheke muda

wote nilivyokuwa naitazama. All is well.
 
Back
Top Bottom