2015-Tutarajie Mengi Kuona na Kusikia "Makada CCM wamfuata James Millya Chadema" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015-Tutarajie Mengi Kuona na Kusikia "Makada CCM wamfuata James Millya Chadema"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchokozi, Apr 19, 2012.

 1. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Arusha kimezidi kutikisika baada ya viongozi wake kuendelea kujiondoa na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Siku mbili, baada ya Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James Ole Milya, kujiunga na Chadema, Diwani wa CCM, kata ya Sombetini mkoani humo, Alfonce Mawazo, naye amejiondoa na kujiunga na Chadema.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana akiwa ameongozana na Katibu wa Chadema Kanda ya Dar es Salaam, Handry Kileo, diwani huyo alisema amekuwa akipingana na sauti ya Mungu siku nyingi iliyokuwa ikimwambia ajiondoe katika chama hicho, lakini alikuwa akikaidi.

  “Leo nimeamua kuitii sauti ya Mungu kwa kuwa unafahamu siku zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, ninafurahi nimetimiza hilo leo (jana) niko tayari kujiunga na wanasiasa wenye uchungu na nchi kwa ajili ya mapambano ya kudai haki na usawa katika jamii,” alisema Mawazo.

  Alisema Tanzania ni nchi yenye ardhi yenye rutuba nyingi na pia mito mingi, lakini bado ni masikini huku wananchi wake wengi wakishindwa hata kupata mlo wa kila siku.

  Alisema ndoto za mababu waliopigania uhuru wa nchi kutoka kwa mkoloni ni kuona Watanzania wakivaa viatu, mashati na wanapata milo yao yote ya kila siku, lakini kwa hivi sasa sivyo.

  “CCM hivi sasa imebaki kama mwangwi na kivuli, nawasihi wenzangu ambao bado wamo ndani ya chama hicho wajiondoe wasiogope kwa sababu hicho sio chama tena, CCM kimebaki kwa nadharia tu si kwa vitendo,” alisema.

  Alisema CCM imekuwa ikipuuza wananchi wa chini na hivyo kupoteza mwelekeo wake.

  Kwa mujibu wa Mawazo, CCM hivi sasa wamebaki na madiwani wanane huku Chadema wakibakia na viti vine mkoani Arusha.

  Hali hiyo inatokana na viti sita kubakia wazi, vitano kati ya hivyo ni vilivyokuwa vikishikiliwa na madiwani waliotimuliwa na Chadema, kiti kimoja kilibakia wazi baada ya diwani mmoja wa CCM kufariki dunia na Mawazo kujiondoa.

  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...