2015 Raisi Mbepari aliyebobea! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2015 Raisi Mbepari aliyebobea!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Petu Hapa, Jan 18, 2012.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa tunawataja maraisi watarajiwa kwa majina. Lakini nadhani turudi nyuma kidogo, tujiulize Je ni raisi mwenye sifa zipi atakaye uondoa umasikini Tanzania.

  Labda tunahitaji mbepari aliyekubuhu, mwenye uelewa mpana wa unyonyaji, atakayeweza kufanya biashara ya rasilimali zetu kuendana na bei ya soko. Huyu hawezi kuuza ardhi kwa million atauza kwa billions, na atawekeza na kufanya tabaka la matajiri lipate nguvu bila kujali rangi wala uraia wa mtu - swala la msingi hapa ni uzalishaji na faida tu. Maswala ya elimu, huduma za jamii yote hayo yanakuwa binafsi zaidi - ndio!- iliwatanzania wasiwe wavivu na kujua umuhimu wa kujitegemea. Na labda tutatengeneza "ndoto ya Tanzania"

  Ama tunataka bepari mwenye utaifa, ambaye nia yake ni kujenga tabaka la mabepari wa kitanzania - hivyo atavutia uwekezaji wa nje na ndani unaotoa nguvu kwa watanzania - sio wote lakini majina ya Bakhresa, Mengi yataongezeka. Kiongozi huyu atahimiza, kuongeza ushuru kwa wawekezaji, mashariti ya kuajiri watanzania, na umiliki kwa watanzania. Swala hapa ni kukuza uchumi ili kuwapa wananchi wachache wamiliki njia za uchumi. Na yawezekana middle class ikaimarika hapa na working class ikatokea.

  Ama tunataka kiongozi mwenye ndoto, ambaye anadhani - uchumi wa tanzanai utainuliwa na kilimo na madini yake - hivyo kuwekeza zaidi kwenye kilimo, miundo mbinu, na huduma za jamii - haswa elimu na afya. Raisi, atakaye wati Mori wananchi na kuwaaminisha tena kwamba nchi ni yao!
   
Loading...