MJENGA
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 883
- 852
Bila ubishi watanzania wengi wameichoka CCM. Wapo wenye sababu ya kuichoka kwa kusema kuwa ni chama kikongwe hivyo wanataka chama kipya chenye mawazo mapya. Wapo pia wenye sababu ya kwamba CCM ni chama chenye kashfa nyingi za ufisadi na mengine mengi. Ndani ya kashfa hizo wapo wanaozielewa kwa upana wake lkn pia wapo waliolishwa vichwani mwao na hao wanafuata tu upepo. Lakini wapo wanaosubiri maamzi ya wengi ndiyo wabadili maamzi yao.
Wapo wasiopenda kuiondoa CCM madarakani kwanza kwasababu ya historia ya amani na utulivu ambayo misingi yake imejengwa na CCM. Kundi hili linaona kuwa kuiondoa ccm madarakani ni kukaribisha serikali ya kihuni ambayo haitazingatia misingi ya amani bali uholela na vurugu.
Kundi hili kubwa ni la wazee na akina mama ambao aghalabu wameshuhudia mapito mbali mbali ya taifa na changamoto ambazo hawataki kuziona Zikijirudia. Hili ni kundi lisilowaamini wapinzani. Linawaona kama watu wenye nia mbaya na taifa na kwamba si bure wanatumika na watu wa nje kuvuruga nchi.
Yote kwa yote, iwe CCM ama CHADEMA watanzania lazima tujiulize kwamba tunapofanya maamuzi 2015, tunayafanya tukiwa ktk hali ya jazba ama chuki, ama kwa kutumia hekima na busara?. Huenda kila mtu ana maslahi na chama atakachokichagua lkn je chama hicho kina utaifa ndani yake? Ni lazima tujiulize. Uchaguzi 2015 hauhitaji jazba wala hasira. Tuamue kwa kuzingatia umoja wetu, amani yetu, utaifa wetu na wala si kwa msukumo wa dini, kabila, wala rangi.
Maamuzi yetu yasibebwe na matarajio makubwa ili kuepusha nchi kumwaga damu katikati ya safari ya serikali itakayochaguliwa. Yapo mambo yatakayowezekana kufanyika lkn tusitembee na vivuli vya yelusalemu takatifu vichwani mwetu. Tusipoiona tutachinjana. Tuwapime wanasiasa kwa kauli, matendo na udhati wa dhamira zao katika kulitumikia taifa. Tuzibaini na kuzitambua ngozi za mbwamwitu kwenye miili ya kondoo ili tusijutie baadae.
Mimi na wewe na yule tujiulize kama ni CCM itatufanyia nini na kama ni CHADEMA itatufanyia nini?. Tuongozwe na utashi wa kiroho ktk kuamua badala ya jazba na chuki. Tukiamua kwa hisia itatugharimu na iko siku thread hii itarejeshwa jamvini na kugombaniwa na wanajamvi kama njugu.
NI UNABII TU!!!.