Wadau,
Nimecheki highlights za mechi za majaribio za Mexico, kuna yule dogo aliyesajiliwa na SAF, anaitwa Javier Hernandez a.k.a Chicharito, dogo ni noma. Jinsi hali niionavyo ktk muktadha wa maono naona Tarehe 11 June itakuwa majonzi kwa wenyeji. Halikadhalika wale wapenzi wa France hali inaeza ikawa hiyohiyo, maana timu yachechemea na timu ya Uruguay ilishawang'ang'ania ktk fainali za 2002 France ilipoangukia pua ktk hatua za makundi. Pia ikizingatiwa fomu ya straika mahiri wa Uruguay, Diego Forlan.