2010 BMW 320i vs Mercedes Benz C Class

Mkuu kuwa serious kidogo. Wakati grs180 inatoka S class iliopo sokoni ni W220. Huwezi kulinganisha chochote Kati ya hizo gari.
Btw Grs180 wameiga shape ya hio W220. Kuanzia grille hadi shape ya taa. Cheki picha zake utanielewa.
S class ikitoka inakuwa mbele 10yrs ya gari nyingi za kawaida. Unafikiri VIps wengi duniani kwanini wanatumia s class?
images (6).jpeg
Lexus_LS_400_model_year_2000_interior.jpg
 
Hata mimi huwa najiuliza inakuwaje gari ya miaka 10 iliyopita kuwa imetembea kms 38k peke yake? Extrovert hebu njoo utusaidie

Inawezekana mkuu, Wenzetu hawamiliki gari moja
Anachagua leo atembelee gari ipi, plus advanced public transport.
Mimi niliaagiza ALLION 2003
IMG_4486.jpg

ilikuwa na km 23,791
Ukiiona ndani, haikuwa hata na chembe ya mkwaruzo, ukifungua bonnet nyeusi mng’ao kama imetoka TOYOTA TANZANIA
Nilienda Carwash moja kila mtu anashangaa, ukiiwasha muungurumo hausikiki kabisa,
Kwa ushamba wangu mara ya kwanza, nilikuwa napiga starter wakati gari iko inaunguruma (kwa vile nilikuwa nahisi haijahawaka engine iko very silent)
Ukitaka kujua kuwa makampuni mengi ya kuuza magari japan wako na uwazi sana, ndiyo maana picha unaoneshwa kila angle, hata kama kuna mchubuko kidogo unaoneshwa.
Ndiyo maana ukiingia Befoward leo Kuna magari mpaka yana km 500,000 na ukiliona bado liko vizuri ( wangekuwa wa kurudisha nyuma km kwa nini wasiweke km chache ili wauze? Kama wanavyofanya Madalali wa hapa kwetu?)
Wenzetu wanachotuzidi kwenye biashara ni UWAZI
IMG_1868.jpg


IMG_4487.jpg

IMG_4491.jpg
 
Mfano hapa,
Wajapan wameshindwa kuweka km 50k?
Ngoma kama hii akiinunua dalali wa bongo anafuta namba moja inabaki 50k

Hivyo kuna asilimia kubwa magari mengi yanauzwa kwenye uhalisia wake, ila ukinunua hapa bongo jua ni kubahatisha.
IMG_1869.jpg

IMG_1870.jpg
 
Hata mimi huwa najiuliza inakuwaje gari ya miaka 10 iliyopita kuwa imetembea kms 38k peke yake? Extrovert hebu njoo utusaidie
Kuna gari ilinunuliwa km 32,000 namba C. Mpaka leo haijafikisha hata km 90,000 na ukiiona ni nzima kuliko hata namba E za juzi.

Sema haikununuliwa kwenye website, ilifuatwa mnadani na mtu na ikatumwa moja kwa moja.

Magari ya bei ya chini yapo mengi sana, sema huwezi yaona kwa wingi kwenye mitandao.
 
Kuna gari ilinunuliwa km 32,000 namba C. Mpaka leo haijafikisha hata km 90,000 na ukiiona ni nzima kuliko hata namba E za juzi.

Sema haikununuliwa kwenye website, ilifuatwa mnadani na mtu na ikatumwa moja kwa moja.

Magari ya bei ya chini yapo mengi sana, sema huwezi yaona kwa wingi kwenye mitandao.

Sure mkuu,
Tena ukiwa na Connection Japan, haina haja ya kununua kwenye mitandao, unanunua mnadani moja kwa moja inakuwa bei nafuu zaidi.
Kuna watu wengi wenye showrooms za magari hapa bongo, wanafunga safari kununua wenyewe kule kwenye minada,
Sisi wa gari moja au mbili ndiyo tunang’ang’ana mitandaoni.
 
BMW 3 series naona inauzwa sana kwenye magari used ya bongo .sijui ni kwamba zinashida au wamiliki wameshindwa kuzihudumia
 
Back
Top Bottom