2009 imepita, tumefanya nini?

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Kwa watanzania walio wengi tumekuwa hatuna utamaduni wa kujiwekea malengo na kufuatilia utekelezaji wa malengo yetu. Inapendeza sana kama mtu anajipangia mambo anayotaka kuyatimiza ndani ya muda fulani (malengo ya muda mfupi na mrefu) katika nyanja mbali mbali kama:

1. Kiuchumi (kuboresha miradi, kuanzisha miradi mipya n.k)
2. Elimu (kujiongezea elimu n.k)
3. Kazi (kuboresha utendaji, kutafuta kazi inayolipa zaidi n.k)
4. Kijamii/kifamilia (kuboresha mahusiano na jamii/familia)
5. Kidini (kumkumbuka Muumba japo mara moja kwa wiki, sadaka n.k)
6. Masuala ya kimaendeleo kwa ujumla (kununua kiwanja, kumalizia nyumba n.k)

Si lazima kuwa na ndoto kubwa zisizotekelezeka lakini ni vema kuwa na malengo yanayokupa mwelekeo wa maisha yako kwa mwaka mzima. Tujaribu kutathmini tumefanya nini 2009 na tuweke malengo mapya ya 2010 na kuyasimamia kwa makini ili itakapofika Disemba 2010 tufanye tathmini. Kama kuna matatizo au changamoto zilijitokeza zisitukatishe tamaa bali tuzichukulie kama opportunities na tufanye kazi kwa bidii kufikia malengo yetu 2010.

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom