200/= Itapendeza kwa Vibanda Umiza.

Puyugu 01

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
573
455
Niende kwenye point kabisa.
Nazani hakuna ubishi kuwa linapokuja suala la Uzarendo, wazarendo sahii huweka kando tofauti zao na kuendelea na Uzarendo wao juu ya jambo lao.

Siku mbili zilizopita kama sijakosea, Chama Cha Soka nchini TFF kimetangaza viingilio vya kuingia ktk kuiona timu yetu ya taifa, Taifa Stars itakayomenyana na timu ya taifa ya DRC ktk uwanja wa taifa utakaofanyika siku ya 27/03/018, mchezo huo nimepata kusikia kama sijakosea, kuwa kiingilio cha juu kabisa ni Tsh.5,000/= na cha mwisho kabisa ni Tsh.1,000/=, lengo la tff hapa ni kupata watz wengi wa kuisapoti team yao ili kuwatia morali wachezaji wetu wa kuichapa vilivyo team ya taifa ya DRC, kwa muktadha uo wa tff kuna haja pia nanyi wamiriki wa vibanda umiza mkatoza Tsh.200/= kuangalia mechi hiyo badala ya Tsh.1000/= kama mfanyavyo siku zote ili kujaza hivyo vibanda vyenu kwa lengo la kuwashangili vijana wetu, najua kuna watu mtakuja na maswali yenu hapa ya, mala hoo!, ukiwashangilia kwenye TV watakusikia hao wachezaji?!, jamani Uzarendo ni popote bila kujali unaemzarendo anakusikia au laa.

Tsh.200/= itapendeza kwa vibanda umiza.
 
sasa mkuu watu wakijaa vibanda umiza itaathiri vipi mechi? wakishabikia vibandani uwanjani wachezaji watapata hamasa?
 
Back
Top Bottom