!!!;.,

zakaria ramadhani

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
228
163
Habari wana jamvi; kwa mara ya kwanza leo nimejitokeza kwenu nikiomba ushauri ktk hili munisaidie,
Ninaishi na mwanamke ambae kiimani hatutafautian bali dhehebu ndio tunatofautiana, yy msabato na mm kkkt sasa changamoto nilionayo kwa huyu mwanamke ni kwamba nimemuomba na kumshauri abadili dhehebu tuwe kitu kimoja ktk familia lkn alikataa

Zaidi ya kukata hata kusali kanisan kwake pia amesitisha ukimuuliza anakwambia heri kua mpagani lkn sio kusali dhehebu tofauti na la kwake na sisi wote ni watumishi jambo ambalo hata kufunga ndo linaniwia gumu;

Kwaio naombeni ushauri wenu nifanyaje! Japo tunamtoto mmoja ambae wakati tunatongozana alikua na mimba ya huyo mtoto ambae sio wangu kwa maana ya kumzaa bali kwa maana yakumlea akiwa tangu tumoni.
 
Kuna vitu wazungu wanaita 'deal breakers', nimeogopa kutafsiri hilo neno nisijepoteza maana yake ila ni vitu ambavyo kwako huwezi kuendelea na mahusiano kama mwenza wako akiwa navyo.

- hizi deal breakers unatakiwa kuwa nazo toka mwanzoni. Yaani unaweza kumuona binti na ukavutiwa naye sana lakini kama suala la imani ni la muhimu sana kwako na nyinyi ni wa imani tofauti basi usiendelee kumfuatilia wala hata kuanzisha mahusiano.

- kosa letu kubwa ni kuanzisha mahusiano huku tukitegemea mtu atabadilika. Au tunaiweka ile deal breaker kama akiba. Siku ukimchoka ndiyo unaitoa kama kadi ya kumuacha.

- Kwa maelezo yako mafupi nahisi na naamini kuna zaidi ya 'dhehebu' kwenye hayo mahusiano yenu. Fanya jambo la kiungwana na msiendelee kupotezeana muda.

- wahenga walisema, "IT TAKES MORE THAN LOVE FOR TWO PEOPLE TO BE TOGETHER."

NB: Swali la kizushi - baba wa mtoto yuko wapi?
 
KAMA HATAKI, MUACHE UKATAFUTE MWINGINE WA DHEHEBU LAKO NA BY THE WAY ANA MTOTO AMBAYE SIO WAKO KWA HIYO UKIMUACHA SIO MBAYA
 
Dah Kama cjakuelewa vizuri....

Alikuwa na mtoto ambae sio wako kwa maana ya kumzaa Bali kwa maana ya kumlea?????

Hapo cjakuelewa kidogo................
 
heading yako ipoje? ila maudhui nimeyaelewa.
lakini kwanini msianzage na kujuana dini ukabila n.k ndo mtakane mengine.

sasa badili wew apo ulie puuza na ukiingia huko uzame kijumlajumla.
 
Kuna vitu wazungu wanaita 'deal breakers', nimeogopa kutafsiri hilo neno nisijepoteza maana yake ila ni vitu ambavyo kwako huwezi kuendelea na mahusiano kama mwenza wako akiwa navyo.

- hizi deal breakers unatakiwa kuwa nazo toka mwanzoni. Yaani unaweza kumuona binti na ukavutiwa naye sana lakini kama suala la imani ni la muhimu sana kwako na nyinyi ni wa imani tofauti basi usiendelee kumfuatilia wala hata kuanzisha mahusiano.

- kosa letu kubwa ni kuanzisha mahusiano huku tukitegemea mtu atabadilika. Au tunaiweka ile deal breaker kama akiba. Siku ukimchoka ndiyo unaitoa kama kadi ya kumuacha.

- Kwa maelezo yako mafupi nahisi na naamini kuna zaidi ya 'dhehebu' kwenye hayo mahusiano yenu. Fanya jambo la kiungwana na msiendelee kupotezeana muda.

- wahenga walisema, "IT TAKES MORE THAN LOVE FOR TWO PEOPLE TO BE TOGETHER."

NB: Swali la kizushi - baba wa mtoto yuko wapi?
Baba wa mtoto kwa maelezo ya mama ake baada yakua walipo kutana ikawa alimuacha na mimba bila kujua na baada ya mwez kama mmoja yule jamaa alifariki kwa ajali kwaio tukanuia pamoja tumlee awe wetu ila alipokuja kubadili gia kiivo sikutegemea
 
heading yako ipoje? ila maudhui nimeyaelewa.
lakini kwanini msianzage na kujuana dini ukabila n.k ndo mtakane mengine.

sasa badili wew apo ulie puuza na ukiingia huko uzame kijumlajumla.
Hiko lilifanyika na alikua wiling hadi kuniruhusu kwenda kwao japo kwao mzee wake alikua mgumu kutoa maamuzi kwakua hapendi watoto wake wabadilishwe dhehebu na pia wanajua kua mtoto ni wangu maana baada ya binti kupata mimba hakuwahi kuwaambia
 
Habari wana jamvi; kwa mara ya kwanza leo nimejitokeza kwenu nikiomba ushauri ktk hili munisaidie,
Ninaishi na mwanamke ambae kiimani hatutafautian bali dhehebu ndio tunatofautiana, yy msabato na mm kkkt sasa changamoto nilionayo kwa huyu mwanamke ni kwamba nimemuomba na kumshauri abadili dhehebu tuwe kitu kimoja ktk familia lkn alikataa

Zaidi ya kukata hata kusali kanisan kwake pia amesitisha ukimuuliza anakwambia heri kua mpagani lkn sio kusali dhehebu tofauti na la kwake na sisi wote ni watumishi jambo ambalo hata kufunga ndo linaniwia gumu;

Kwaio naombeni ushauri wenu nifanyaje! Japo tunamtoto mmoja ambae wakati tunatongozana alikua na mimba ya huyo mtoto ambae sio wangu kwa maana ya kumzaa bali kwa maana yakumlea akiwa tangu tumoni.

Mr. Zakaria Ramadhani....... KKKT plus Msabato plus Ramadhani nitarudi baadae
 
Hiko lilifanyika na alikua wiling hadi kuniruhusu kwenda kwao japo kwao mzee wake alikua mgumu kutoa maamuzi kwakua hapendi watoto wake wabadilishwe dhehebu na pia wanajua kua mtoto ni wangu maana baada ya binti kupata mimba hakuwahi kuwaambia

Janga lipo kwa huyo Mtoto Mkubwa na Wakwe zako wanajua Umezaa na Mtoto wao, Wakati wewe Unajua Mtoto siyo wako..

Haki Ya Mungu Duniani Kuna Viumiza kichwa na Kichwa Kuviuma
 
Baba wa mtoto kwa maelezo ya mama ake baada yakua walipo kutana ikawa alimuacha na mimba bila kujua na baada ya mwez kama mmoja yule jamaa alifariki kwa ajali kwaio tukanuia pamoja tumlee awe wetu ila alipokuja kubadili gia kiivo sikutegemea

- Kama mshkaji amefariki basi sawa. Nilidhani yupo hai ningesema uchunguze kama hilo lingeweza kuwa chanzo cha yeye kubadilika.

- kama mlikubaliana mwanzoni kuwa atabadili na kuja kwako kisha sasa amekugeuka ni dalili (SI LAZIMA IWE KWELI) ni dalili kuwa alikuhitaji kwa kipindi kile kama wa mpito

- tatu, kitu ambacho mimi kinanifanya nisiwe na mahusiano na binti asiye na imani sawa na mimi ni maneno aliyoniambia amam yangu 2002 nikiwa kidato cha sita. Nilimpata rafiki, binti mzuri wa Kiislamu, full adabu. Binti alikuwa tayari kubadili dini ili awe na mimi na alishaanza kusoma Biblia. Mama aliniambia, "Usibadili dini ili uweze kuoa/kuolewa na mtu. Mtu anatakiwa kubadili dini endapo TU ameshawishika kuwa imani ile ni sahihi sio ili awe na fulani."

Baada yamaneno hayo nimekuwa makini sana wadada ninaoanzisha mahusiano nao kwa maana kuwa tangu mwanzoni mwa urafiki unakuwa umeshapata majibu la sivyo mwanzoni kabisa mwa mahusiano yenu unaweka vigezo vyako vya muhimu ambavyo hautakuwa tayari ku-compromise. La sivyo mridhie kila mtu abaki na dini yake.

- ila kama unachosema ni kweli tupu kuwa mlikubaliana abadili mwanzoni, kisha hivi karibuni amegoma basi huenda (1) amechunguza na kugundua huko aliko ni sahihi zaidi kiimani kuliko huko uliko wewe (2) alikuwa kwako kwa sababu fulani na alikubaliana na matakwa yako ili kufanikisha adhma zake tu

- kama mmeshafanya mengi, mnapendana bado basi fikiria kila mtu ambaki na dini yake mkuu. Jengeni familia mzungumze juu ya watoto na kwamba watafuata imani ipi. Fungeni ndoa muishi kwa amani na furaha.
 
Nashukuru kwa ushauri braza! Japo ninaamin uwezekano wa yy binafs wakubadili angekua nao tu endapo kama mtoto angekua wangu kiuhalisia lkn nshis mebadilika kwakua pengine alishajiandaa kulea mwenyewe ukizingatia mimba niliikuta ina miezi 6, nakingine anawasikiliza mno ndugu zake.
 
Hiko lilifanyika na alikua wiling hadi kuniruhusu kwenda kwao japo kwao mzee wake alikua mgumu kutoa maamuzi kwakua hapendi watoto wake wabadilishwe dhehebu na pia wanajua kua mtoto ni wangu maana baada ya binti kupata mimba hakuwahi kuwaambia
zakaria ramadhani unatuchosha kujibu yaan ID yako tu km muislam vile any way.

fata moyo wako.
 
Back
Top Bottom