100% Original human hair


Ha ha haaa eti nina njaaa...sawa nina njaa ya mafanikio lakini siyo ya tumbo. Siwazi leo nitakula nini bali nawaza leo najisikia kula nini. Ndiyo nasema tena bila ya shaka yoyote kuwa kushonea weaving,wigs na kusuka misuko kichwani ni alama ya urembo kwani kwa mwanamke urembo namba moja ni nywele.

Pia nikuambie kuwa unarusha na kupiga ngumi ukutani...kwani huwezi kuwatenganisha wanawake na urembo...hasa urembo wa nywele! Na siyo Tanzania tu au Africa bali ni dunia mzima. Ila kama utashika fimbo au pistol mkononi na kuanza kuwapiga wauzaji wa maduka ya nywele, viwanda vya nywele vilivyopo Bongo,na wanawake wa Dar wote wanaopenda urembo wa nywele basi nitaamini hichi unachokisimamia...zaidi ya hapo naona kama unafurahisha nafsi yako tu ilihali unajuwa ukweli ni upi.

Karibu tuendelee
 
Ni aibu kwa mtt wa kike kuweka nywele bandia shame on u unapoteza uzuri wootee
 
Wewe ni me/ke? how old are you? i guess under 20. Hivi unaelewa tunajadili nini? sasa kunyoa nywele au ndevu kunahusiana vipi na kuweka minywele bandia? kwa hiyo kwa akili yako kunyoa kunaondoa sifa ya kuwa natural?
Siwezi kubadili muono wako kwa sababu wewe unaona kunyoa ni natural.
Kama ingekua natural si zingepukutika kama majani yanavyopukutika kutoka kwenye mti?
 


Mijitu ya hovyo ni mingi sana nchi hii.Wewe endelea na msimamo wako sikuzuii,Mungu akusamehe kwa maana hujui utendalo. I'll keep praying for you and your fake air- obsessed fellows. Say amen
 
Siwezi kubadili muono wako kwa sababu wewe unaona kunyoa ni natural.
Kama ingekua natural si zingepukutika kama majani yanavyopukutika kutoka kwenye mti?

Dogo hear me out. Does shaving make one's hair unnatural?
 
Unaposema "kuku wa kienyeji" unamaana wale confident women wasiokubali upuuzi wa wafanyabiashara njaa wanaowaambia kuwa kuvaa minywele ya bandia ndiyo urembo? If so Flaviana Matata ni "kuku wa kienyeji" kwa tafsiri yako siyo..?

Kuku wa kienyeji ni demu wa uswahilini maisha choka mbaya…kuku wa kizungu ni demu wa kishuwa a.k.a familia bora no matter anaishi Buguruni au Masaki.

Huyo Flaviani matata kama ni mrembo amewahi kushinda taji la miss Tanzania au Miss world akiwa natural? what i know huyo dada ni mwanamitindo (model)



Haya huyo hapo ndiye Miss World 2013…picha ya kwanza nimekuonyesha akiwa na hair extension kichwani alizotengenezewa salon, na picha ya pili akiwa ndani ya crown akifurahia kutawazwa mshindi.
Anaitwa Megan Young. Haya niwekee picha ya Miss Tanzania wa mwaka wowote ule ambaye alishinda hilo taji la urimbwende akiwa natural kama Flavian Matata wako.

Karibu tuendelee
 
Mijitu ya hovyo ni mingi sana nchi hii.Wewe endelea na msimamo wako sikuzuii,Mungu akusamehe kwa maana hujui utendalo. I'll keep praying for you and your fake air- obsessed fellows. Say amen

Tulia ikuingie vizuri na ikiwezekana ikatie na viuno…gaadem!

Hiyo duwa yako hebu kwanza anza kuviombea viwanda vyote vinavyotengeneza artificial hair,maduka yote ya dunia mzima yanayouza hizi nywele na mwisho hiyo duwa yako iwaendee wanawake wote wa dunia mzima wanaopenda urembo wa nywele…kisha ndiyo uje kwa sisimizi kama mimi.

Karibu tuendelee
 

Mbona umekazania sana Miss Tanzania,Miss blah blah. Hao si ndo wapuuzi walewale? Mungu akusaidie,haujajitambua bado. Hivi unafahamu Mwl. Nyerere alipiga marufuku huo uchafu wa miss blah blah? So never expect a person of my calibre to support such a bullshit
 

Tulia ikuingie…na ikiwezekana ikatie na kiuno.

Kama unatural ndiyo uzuri na urembo…kwanini hatujawahi kuona miss Tanzania yeyote aliyeshinda hilo taji akiwa natural kuanzia unyayoni hadi utosini? Na kama unatural ndio urembo na uzuri kwanini kila miss world aliyeshinda hilo taji alipitia kwanza salon ndipo akaenda kwenye event? Au ndiyo kusema unatural haulipi na hauuzi?

Au ndiyo tusema waandaji wa miss Tanzania na Miss World wote kwa pamoja hawana akili ila wewe ndiye unaakili nyingi kuliko waandaji wa mashindano haya yaliyotapakaa dunia mzima?

Karibu tuendelee
 


I'm amongst those who question and think critically. Kama wewe unafuata tu bila kufikiri uhalali au madhumuni ya kitu fulani you deserve nothing but POLE.Nadhani pia utakuwa one of the homosexuality supporters,si kwa sababu wazungu wameshakuambia kuwa ni sahihi?
 

Asilimia 80 mambo yote tunayoyafanya waafrica tumeletewa na hao wazungu zikiwemo dini…na wakatuaminisha ni sahii hadi leo tunaviendeleza, so urembo wa nywele nao uko umo umo kama tulivyozipokea hizi dini na vitu vingine kutoka kwao. Eti nyerere alikataza urembo! nani kakuongopea? hebu weka ushahidi hapa tuone…by the way niko very close na nyumba ya mwalimu Nyerere hapa msasani na nawaona baadhi ya watoto na wajukuu zake wanavyopenda urembo wa nywele na kucha.

Narudia tena naomba uniwekee picha ya miss world na miss Tanzania yeyote yule aliyeshinda hilo taji akiwa na vinywele vifupi aka kipili pili au akiwa natural kipara. Maana hao unaowasema kuwa ni wajinga au wapumbavu kwa vile wanashonewa weaving na kusuka misuko ndio wanaoshinda kwenye mashindano hayo na mengine yanayofanana na hayo.

Nasubiria picha. Karibu tuendelee
 


Una kichwa kizito kweli dada'angu nishakuambia achana kunipa mifano ya miss blah blah kwa sababu mimi siamini katika huo uchafu sawa? nitolee mifano ya watu wenye akili timamu siyo hao wapuuzi. Unajua ni kwa nini mashindano ya miss Tanzania yalifanyika mwaka 1961 then yakasimama hadi mwaka 1994? au haujui nikusaidie? usinichoshe
 
Merci brazilian hair kwa sh elfu 50? yenye urefu gani?.maana huuzwa kulingana na urefu.
 
Last edited by a moderator:
Wewe endelea kuwauzia wenzako hizo nywele za bandia uendelee kuishi na wahubirie kuwa kubandika nywele za bandia juu ya nywele halisi ndiyo urembo,waambie pia wabandike kucha,kope na hata kama kuna lips za bandia waambie waweke ila watawapata wajinga wenzao.Mimi sahau
 

Eti dada angu' nani kakuambia mimi ni dada? Mimi ni mwanaume tena lijari na muhangaikaji hasa…mimi ni moja ya wadau wa urembo hapa Bongo kama ilivyo kwa S.H Amon.

Naona unakwepa maswali magumu na badala yake unaleta majibu mepesi na yenye mipasho ya kike…sasa tulia ikuingie.
Kama tumeaminishwa kuwa Miss Tanzania wa kila mwaka ndiye msichana mzuri na mrembo…sasa inakuwaje hatujawahi kumuona miss Tanzania au Miss world aliyeshinda hilo taji akiwa kwenye muonekano wa Natural? Au ndiyo kusema unatural hauuzi na haulipi? Bado nasubiria picha kutoka kwako ili tufunge mjadala kuwa urembo wa nywele siyo dili.

Karibu tuendelee.
 

Hujui usemalo,
If i were you
Ningekojoa na kwenda kulala
Hahahahahahaha.
 

Kumradhi ndugu. The way unavyoandika,i thought you are she.I'm sorry never intended to demean you. Ila kama ni mwanaume nazidi kushangaa zaidi. can't you see anything wrong with those fake hairs? Umeaminishwa na nani kuwa miss Tanzania ndiyo msichana mzuri kuzidi wote? na wewe unaamini bila kujiuliza au kuweka vigezo vya kwako? Hii nchi ina watu wa hovyo wengi sana. Usiendelee kujaza server ndugu,najua unapigania kitumbua chako (si unakula kupitia minywele bandia and the like?)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…