masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 17,570
- 20,146
Ni kweli siyo original hizo ni human hair za kawaida tu. Ila kwa bei aliyotaja inaendana na thamani ya hiyo nywele.
Ukihitaji Unprocessed hair ni ghali sana tena kwa pc moja
Kanisome juu huko vizuri juu huko, wacha kubwabwaja.
Hizo nywele zenyewe ni maiti.
Kiungo cha binaadam ulichokitowa mwilini mwake kwa kum exploit kwa umasiki wake ni haramu kwa namna yoyote ile.
Hivi huoni uchafu hata kuzishika wacha kuzivaa?
Wewe unatetea kwa sababu ni biashara yako na hata muuza unga leo hawezi kusema unga ni mbaya kwa kuwa ni biashara yake. Isipokuwa kumbuka, hiyo biashara ya kuuza viungo vya binaadam ni mbaya zaidi ya biashara ya utumwa.
Ila pia nakubaliana na wewe kuwa baadhi ya urembo siyo inshu pamojakuwa mimi ni mdau katika mambo ya urembo lakini kuna baadhi ya urembo siutaki kabisa kuona mwanamke yeyote yule anaufanya awe mwafrica au mzungu.
*Urembo wa kuweka kope siufagilii kabisa
*Urembo wa kuongeza ------ siufagilii kabisa
*Urembo wa kujichubuwa siufagilii kabisa. Sivipendi kabisa hivyo vitu
kumbe urembo ni kuweka brazilian hair kichwani? duh basi mie siyo mrembo haaah!
Sasa wewe unapenda urembo upi? Kama hutojali ningependa kukuelezea hizo nywele impact zake
Ha ha haaa umenifurahisha sana Mkuu! Nimependa ulivyoniuliza napenda urembo upi…okay here we go
*Mimi naamini bila shaka yoyote urembo wa kusuka rasta na kushonewa weaving vizuri liwe fupi au ndefu ndiyo urembo namba moja hapa duniani.
*Pia naamini urembo wa kubandikwa kucha hasa za mikono (m-bandikaji awe professional) kupaka rangi za Gel,pedicure na manicure.
*Mwisho napenda huduma za skin care treatments au nisema Body treatments. Huo ndiyo urembo na usafi wa mwili ambao mimi ninaupenda na daima nitauendeleza kwa kuuza na kutoa huduma zake.
Asante sana...nafurahi zaidi kama kweli umefurahi
- Kusuka rasta hapo sawa...nakusapot....weaving nakusapot...lakini weaving au rasta liwe lile linalotokana na artificial fibres kama katani...Ila la nywele natural za mtu hapo naona haiko sawa.
- Kupaka rangi,Manicure,Pedicure sio mbaya hio nai support...lakini kubandika kucha bandia hapana....haiko sawa hiyo.
- Body treatments sawa hio nakusupport....i do it to someone...but kujichubua no...hio haiko sawa
Lakini kuna kitu nimekwambia kama hautajali haujajibu......
mie nabaki na nywele zangu za makumbi na huyu mumewangu ndio wale wa napenda nywele zako mke wangu lakini nadhani kwaufupi hapendi,niliongezwa kimkia siku ya harusi yani sisahau,tumetoka kwenye hall,tumeingia chumbani hata wageni walotusindikiza aliwambia misone vibaya naomba mda nataka kupumzika na mke wangu,watu wakaondoka yani kufunga mlango tuuuuu moja kwa moja anaanza kunipekura nywele kanambia mbona una msitu kichwani vipi? nikamwambia ni extension kanambia nnayo ijua mie ni extention ya wire hii ya nywele siiijui na staki kuijua,nimekupenda bila hayo mashaka ulotia kichwani,naomba ufumue tafadhali,nilichukuia na hatukulala ilibidi nimwite mtu kutoka home aje anifumue mpaka namaliza kufumuliwa asubuhi time ya sala ya alfajiri naenda kukoga nasali. uso mduchuuu..
we nae umetusemaaaa.
Hiyo username yako ni kqamba wewe ni fundi wa sex ama ticha?
Mi ni mtaalamu wa mapenzi..
Ahsante sana! Jibu lake ni moja tu na ni rahisi sana HUWEZI KUMTENGANISHA MWANAMKE NA UREMBO.
Siyo Tanzania,Kenya wala Uganda bali ni dunia mzima kuanzia Ulaya hadi America
Kwa hiyo kwako wewe kuvaa minywele ya mtu mwingine ndiyo urembo? i feel sorry for you and those with a pathetic thinking capacity like you. What's wrong with you women,was God wrong to create you the way you are? Repercussion ya hii kitu psychologically ni kubwa na kwa mtu mwenye fikra duni kama za kwako si rahisi kuiona,no wonder majority of women are with terrible inferiority complex. Hivi umeshawahi kusikia mwanaume anatafuta ndevu za kubandika,there are scores of men who are without beards and they would wish to have lakini you will never find them looking for an idiotic way to make them look the way they are not. Hii kitu inaanzia kwenye subconscious mind kwa hiyo hata wewe si rahisi kujijua kama una matatizo upstairs.
Mbona unanyoa ndevu na nywele au vuzi?Kwa hiyo kwako wewe kuvaa minywele ya mtu mwingine ndiyo urembo? i feel sorry for you and those with a pathetic thinking capacity like you. What's wrong with you women,was God wrong to create you the way you are? Repercussion ya hii kitu psychologically ni kubwa na kwa mtu mwenye fikra duni kama za kwako si rahisi kuiona,no wonder majority of women are with terrible inferiority complex. Hivi umeshawahi kusikia mwanaume anatafuta ndevu za kubandika,there are scores of men who are without beards and they would wish to have lakini you will never find them looking for an idiotic way to make them look the way they are not. Hii kitu inaanzia kwenye subconscious mind kwa hiyo hata wewe si rahisi kujijua kama una matatizo upstairs.
Mbona unanyoa ndevu na nywele au vuzi?
Si ungejiacha uwe natural? Half empty/half full kinda thang.
Acheni ushamba.
Daah! Naona umehamaki na kunishambulia sana. Vipi mkuu unaishi dunia ya ngapi? Sasa mwanaume abandike ndevu za bandia ili iweje? By the way narudia kukuambia tena kuwa huwezi kumtenganisha mwanamke na urembo hata ufanye nini.
Kwa hapa Dar katika wanawake kumi basi saba kati yao watakuwa wameshonewa weaving au misuko ya rasta...na watatu Kati yao utakuta ndio wako natural. Hivi una habari hapa Bongo tu kuna viwanda karibia saba ambavyo vinatengeneza weaving na rasta?...achilia mbali USA,UK na China? Mkuu mimi ni sisimizi tu! Kuna mitembo mikubwa mikubwa na sasa imekuwa mibilionea kwa ajili ya kuuza fake hair na hizi rasta. So jitahidi kuliangalia hili swala kwa jicho la tatu na siyo unaitizama hii industry kwa kibongo bongo tu.
Karibu tuendelee.
Mbona unanyoa ndevu na nywele au vuzi?
Si ungejiacha uwe natural? Half empty/half full kinda thang.
Acheni ushamba.
Mkuu, sometime nikisoma baadhi ya comment za watu hapa jamvini huwa nabaki mdomoni wazi...yaani mtu anataka kushindana na kitu ambacho anajuwa kabisa siyo rahisi kukizuia hata iweje...ila anaongea ilimradi aonekane na yeye kachangai kwa namna moja au nyingine.
Hivi jamani tuwe wakweli...hivi utamlinganisha kuku wa kienyeji wa uswahilini na kuku wa kizungu(mtoto wa kishua)kama huyu hapa pichani? Mtoto ni mzuri alafu ni mrembo...ha ha haaaa!