10% ya watanzania hawana ajira?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

10% ya watanzania hawana ajira??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kajuni, Jan 2, 2012.

 1. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Heri ya mwaka mpya!

  Kama kawaida nimekuwa napata mzio (allergy) pindi mkuu wa kaya anapo wahutubia wadanganyika!!! Kutokana na ushauri wa kitabibu nilishauriwa kuzima TV, Redio, Magazeti etc na kutokwenda kwenye mikutano ambayo mkuu wa nyumba anaweza kuhutubia.
  Hata hivyo kwa kuwa naipenda nchi yangu nimejikuta nikikaidi ushauri huu na safari hii nimepata mzio kweye hili!!! Hivi ni kweli kwamba ni asilimia 10.7% ya watanzania hawana ajira?

  Naomba kunukuu " inakadiriwa kuwa hapa nchini mwaka 2011, kuna watu wenye uwezo wa kufanya kazi 22,152,320 na kati ya hao 2,3968,672 au sawa na asilimia 10.7 hawana ajira" mwisho wa kunukuu. Hii ni hotuba ya mkuu wa kaya katika salamu za kufunga na kuukaribisha mwaka 2012.

  Jamani wana JF, ni mimi ndo naumwa? au mkuu wa kaya kadanganywa na magamba wenzake? kwa maoni yangu naona kama hizo takwimu ni sawa basi ingekuwa kinyume. Yaani asilimia 10.7% ndo wana ajira na asilimia 89.3% ndo wasio kuwa na ajira. Kwani naona kila kukicha tatizo kubwa ni ukosefu wa ajira, vijana wengi tupo mitaani hatuna ajira. Kilio chetu ni ajira.

  Je wana JF hizi takwimu ni sahihi? au ndo kama kawaida WADANGANYIKA!!!
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  10% ya watz ndio wana ajira
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnhh hii takwimu nimegooma
   
 4. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Kaka hujazoe 'fiksi' za siasa za bongo ? uwongo 89.3% Ukweli 10.7%. Bila kutikisa system kama walivofanya vijana Egypt,Tunisis,Morocco Libya Yemen ,vijana wengi tutadidimia kwenye dimbwi la umaskini wa kutupa. Serekali ya ccm haina mpango mahsusi wa kutatua tatizo la ukosefu ajira kwa vijana.
   
 5. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Heri ya Mwaka mpya mkuu!

  kama makadirio yanatokana na tafiti basi ni vizuri tujiulize huo utafiti kaufanya nani na kwa manufaa gani?
   
 6. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  9% ndo wenye ajira, tena ajira nyng zpo icu!. Ova!
   
 7. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,712
  Trophy Points: 280
  kila siku anazidi kuharibu
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nategemea Ambassador Sefue atarekebisha hizi kasoro kwenye speeches zijazo. Lakini pia ni vizuri rais aridhike na anachoandikiwa. Hivi yeye mwenyewe anaamini ni 10.7% ndio hawana ajira? hata hiyo number ya 22 millioni mgogoro!
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Km 35% ya waTanzania wanaishi katika umaskini uliokithiri, currently, agriculture alone contributes about 25 per cent of GDP but absorbs 74 per cent of the labour force. Data hizo kidogo ukijumlisha na yale mazungumzo yake na wazee wa CCM - Dar anaowaitaga wazee wa Dsm aliosema serikali ina wafanyakazi - 350,000 Tanzania nzima na take note ndio largest employer of the country, haingiii kichwani kusema eti 10% ya Watanzania hawana ajira.... JK = Malaria Sugu wa JF......
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,959
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kumbuka kwamba amesema 'inakadiliwa', hiyo maana yake ni kwamba hakuna taarifa sahihi au kumbukumbu kuonyesha idadi ya walioajiriwa.
  Pili, kwenye nchi kama yetu si rahisi kuwa na takwimu kama hizo kwa sababu hatuna mfumo maalumu unaoweza kutusaidia kutambua kama mtu ameajiriwa au la. Hakuna mfumo wala utaratibu unaowezesha kufuatilia na kujua iwapo mtu kaajiliwa, kajiajiri, kaachishwa kazi, nk. Siamini kama Idara ya Kazi wana takwimu halisi za watu walioajiriwa.
   
 11. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yaani hiyo number huwa wanaincllude bodaboda,bajaji,waokota chupa za prastiki,wakata majani,house girls and boys,wakulima jembe la mkono,machingas,and etc,then kama haufall hapo ndo hauna ajira sasa,I REPEAT Kufa hatufi ila sasa cha moto..............................
   
 12. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tatizo la vijana wengi ni masharobaro. Hivi ajira nilazima iwe serikalini? Au mashirika? Vijana ubunifu unahitajika,mambo ya kulalamikalalamika tu! Kukwenda shamba sio ajira? Tumia kaelimu kako kakufaidishe na sio kutembea na mavyeti kusaka ajira. Tatizo la masharobaro wanataka ofisi kali na mshahara mkubwa!
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mh,22,152,320?
  Imenigonga
   
Loading...