Dunia ya muziki wa Tanzania imekuwa ikipitia mageuzi makubwa kwa miongo kadhaa. Kila zama imezaa nyota zake – kuanzia wasanii, watunzi, waimbaji, hadi watayarishaji muziki (producers). Katika zama hizi za mitandao ya kijamii, kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kujianika hadharani na kujinadi...