Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Riziki Shemdoe, amechukua fomu kuomba ridhaa kugombea ubunge Jimbo la Lushoto, mkoani Tanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Profesa Shemdoe amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Lushoto, Miriam Kaaya.