olengurumwa

Onesmo Olengurumwa
Onesmo Kasale Olengurumwa ni wakili msomi, ambapo alizaliwa mwaka 1980, katika kijiji cha Sakala, Kata ya Ogosorock, Loliondo, Wilayani Ngorongoro.

ELIMU

Onesmo alisoma katika Shule msingi sakala, na badaye alisoma masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Arusha Catholic Seminary kwa kidato cha kwanza hadi cha 4 "O Level". Onesmo aliendelea na Elimu ya A level katika Shule ya Sekondari ya Dakawa Morogoro ambapo alisoma kidato cha 5 na 6 mwaka 2004

Onesmo Kasale Olengurumwa, ana digrii 2, ambapo ya kwanza ni digrii ya sheria toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na digrii ya pili ya uzamivu katika maswala ya utafiti na sera za umma (Masters in Research and Public Policy) chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Onesmo, kitaaluma ni wakili wa Mahakama kuu Tanzania baada ya kuhitimu katika Chuo cha mafunzo kwa Vitendo kwa wanasheria (Law School of Tanzania). Lakini pia amesoma kozi mbalimbali za haki za binadamu, sheria na utawala ndani na nje ya Tanzania.

FAMILIA na MAKAZI

Onesmo, ana familia, mke na watoto, makazi yake kwa sasa yapo Jijini Dar es Salaam na kijijini Sakala Loliondo.

KAZI

Wakili Msomi Onesmo Kasale Olengurumwa, amekuwa akifanya kazi za utetezi wa haki za Binadamu toka akiwa Chuo kikuu ambapo alikuwa Rais wa Chama cha Haki za Binadamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Onesmo Olengurumwa aliwahi kufanya kazi katika Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) Kati ya mwaka 2010-2012.

Kwa sasa Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa ni Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

USHIRIKI KATIKA MASUALA YA KIJAMII

Onesmo Olengurumwa, amekuwa Mtetezi wa muda mrefu wa haki za binadamu hapa Tanzania, ambapo anafahamika sana kwa misimamo yake katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu na sheria. Amezunguka nchi nzima kusikiliza na kutatua changamoto za Watanzania wenye changamoto za haki zao.

Wakili Onesmo, ameshiriki na kujishughulisha kwa kiasi kikubwa katika kutetea haki za wanangorongoro hasa masuala migogoro ya ardhi. Amekuwa mstari wa mbele katika kuwaongoza na wakati mwingine kuwasemea wanangorongoro katika migogoro mbalimbali inayowakumba kwa miaka mingi.

SIASA na UONGOZI

Wakili Onesmo Olengurumwa amekuwa mwanachama na kada wa CCM toka 2005

Mwaka 2008 hadi 2012 alikuwa mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, kutokea Wilaya ya Ngorongoro,

Wakili Onesmo, pia aliwahi kugombea Uwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro.

Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, kwa sasa ni Mkurugenzi wa THRDC

Wakili Msomi Onesmo Olengurumwa, Aliachana shughuli za kisiasa toka Mwaka 2010 na kujikita katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu.

Hakuwahi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa baada ya kuacha UVCCM mwaka 2012, Hata hivyo Wakili Onesmo amekuwa karibu sana na siasa za Ngorongoro kama mshauri wakati wa uchaguzi na katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii.

Wakili Onesmo, ni mtu anayeipenda sana Wilaya yake ya Ngorongoro na watu wake, ambapo amekuwa msaada katika masuala mbalimbali ya kijamii na watu binafsi wanaopata changamoto za kisheria, ikiwa ni pamoja na kusaidia kwenye kesi mbalimbali.
  1. Mafyangula

    POTOSHI Olengurumwa: Katiba mpya inakwamishwa na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo

    Wakuu Je, Olengurumwa aliyasema maneno haya au amemezeshwa? kwamba Katiba mpya inakwamishea na CCM mtandao wanaonufaika na mfumo.
  2. DuaZaMama

    GE2025 Olengurumwa: Mfumo wa CCM unazaa wabunge waoga

    Anaandika Mkurugenzi wa THRDC Onesmo Kasale Olengurumwa kupitia ukurasa wake wa Instagram: ==== Sijajua tunataka wabunge wa aina gani - nilisifia hizi kanuni mpya za Chama Cha Mapinduzi CCM upande mmoja kuwa imeongeza watu wengi kupiga kura na kupunguza rushwa ila nikaonesha hatari ya...
Back
Top Bottom