Kama inavyosomeka hapo juu, jana na_scan kadi yangu pale Ubungo Maji naona 1000 imekatwa. Nauliza mhudumu inakuaje ananiambia nauli 1000.
Abiria mwingine naye ananiambia tangu usafiri umerudi ndio nauli wanayokatwa. Naambiwa hiyo haijawahi hata tangazwa.
Sasa Hawa LATRA wanafanya kazi gani...
Jumatatu mida ya saa moja na dakika 15 nipo gerezani nasubiria gari ya Mbezi picha linaanza watu niliowakuta ni wengi na gari hamna toka saa 19:15 hadi saa 20:40.
Gari zinazopita zinaenda Kimara au Muhimbili na Morocco ila Mbezi ndo kama umesahaulika saa 20:40 gari za Mbezi zinafika Gerezani...
Mimi nina kero moja hawa wahudumu wa mabasi ya mwendokasi wanatoza nauli zaidi tofauti na utaratibu wa nauli zilizowekwa kwa kisinginzio cha kukosa chenji.
Kwa mfano nauli ya kutoka Mbezi kwenda Gerezani ni Tsh 1,250 ukitoa noti ya 2,000 unarundishiwa 500 wakisema chenji hamna.
Naomba kupendekeza nauli ya mwendokasi iwe elf moja
Leo nimepanda mwendokasi mara 4 na hawakuwa na chenji
Sijui ni stlye au ni kitu gani, vituo almost vitatu hawana 250
Ni Jambo la Aibu Sana mbona Kwa vyombo vya usafiri wa binafsi hakuna haya mambo?
Mnashindwa kwenda bank na kupata change...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.