Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, ameeleza kuwa jumla ya vitongoji 1,997 sawa na asilimia 88.4 kati ya vitongoji 2,260 vimeshapatiwa huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iliyopita na inayoendelea...