Wapo wanaosema, kazi ndio kila kitu; wapo tayari kuipambania kazi zao kuliko familia, wakiamini familia ikiharibika kazi itamsitiri kwa kumpatia fedha na kuanzisha familia nyingine.
Je, wewe kwa mtazamo wako, kwako ni kazi kwanza au familia kwanza?
Kuna siku nilikaa na bibi yangu tukizungumza kuhusu maisha yake ya zamani.
Nilimuuliza swali ambalo lilinifanya nisikie simulizi ambayo hata baadhi ya wajukuu zake hawakuwa wamewahi kuisikia.
Niligundua kuwa zamani alikuwa amesomea na kufanya kazi ya uuguzi, lakini baadaye akaja kuwa mwalimu...