shadow recruit
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 1,844
- 384
KAFULILA AUMBUKA KWA KUSEMA SETH HATAKIWI KENYA
View attachment 186998
mmililki wa IPTL na mwakandege mwanasheria wa IPTL
KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung'aa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.
Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.
Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.
Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW
Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania.
Barua hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akithibitisha barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.
''Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,''alisema.
Hivyo, alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.
Kutolewa kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara nchini humo.
===================================
Chanzo: habarileo

KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayomiliki Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) itasambaza umeme wa megawati 2,000 kwa Kenya.
Hatua hiyo inatokana na kukamilika kwa mazungumzo baina ya kampuni hiyo na Serikali ya Kenya.
Katika kuthibitisha utekelezaji wa mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli wa Kenya, Joseph Njoroge amesaini barua ya makubaliano Agosti 19, mwaka huu kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa Pan African Power (PAP), Harbinder Sing Sethi.
Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A zinabainisha kuwa pande zote tatu yaani PAP, Tanzania na Kenya zikutane haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa PAP, Joseph Mwakandege alisema kampuni yao inamejizatiti kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi badala ya kuendeleza malumbano ya kisiasa ambayo hayaleti tija kwa taifa.
"Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhihirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati," alisema.
Pia amezishauri kampuni nyingine za kuzalisha umeme kuelekeza utaalamu katika kuwatumikia wananchi badala ya kupigana vijembe ambavyo huzaa chuki na kudhoofisha kasi ya maendeleo ya wananchi.
Chanzo: habarileo